Fanya Mambo Haya 20 Kila Siku Na Utakuwa Wa Kipekee Sana.

Fanya Mambo Haya 20 Na Utakuwa Wa Kipekee Sana.

Rafiki Yangu,

Vp Hali Yako?

Unauwezo Wa Kipekee Sana.

Na kama uamini jaribu kila siku ( Asubuhi na Usiku kabla ya kulala ) kujitamkia  Hayo Maneno Hapo Chini;

Mimi ni bora nimezaliwa kufanya mambo makubwa na kesho yangu ni bora kuliko leo”

Wewe jitamkie tu kila siku asubuhi baada ya muda utaona mabadiliko makubwa sana.

Na ukiweza kuchanganya na haya mambo 20 ambayo unaenda kuyaona sekunde chache zijazo yatakutofautisha haraka sana.

Wote tunajua kwamba,

Maisha ni magumu, ila huwa tunachagua kuyafanya kuwa magumu zaidi ya yanavyostahili.

Kuyarahisisha maisha yako mwezi huu, fanya mambo haya 20.

1. Jiwekee lengo moja kubwa ambalo utalifanyia kazi kila siku kwa mwaka mzima.

2. Ongeza kipato chako kwa angalau asilimia 20 ya kipato mwaka huu.

3. Kila siku kazana kuwa bora zaidi ya jana, shindana na wewe mwenyewe na siyo mtu mwingine.

4. Kwenye kila kipato unachoingiza, tenga asilimia 10 na weka pembeni kabla hujaana kutumia.

5. Asilimia 10 unayoiweka pembeni, iwekeze sehemu ambayo inazalisha zaidi.

6. Soma kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, kupata mwongozo sahihi kufikia uhuru wa kifedha. Kupata vitabu piga simu 0752977170.

7. Punguza sana au acha kabisa kutumia mitandao ya kijamii kama haikuingizii kipato.

8. Usianze siku yako kwa kufuatilia habari.

9. Soma angalau kurasa 10 za kitabu kila siku.

10. Amka mapema zaidi ya ulivyozoea, angalau saa moja na tumia muda huo kusali/kutahajudi, kujisomea na kufanya mazoezi.

11. Pangilia siku yako kabla hujaianza, tafakari siku yako kabla hujaimaliza.

12. Weka muda kwenye kujenga mahusiano yako, hasa ya wale wa karibu.

13. Weka juhudi zaidi kwenye kazi/biashara, nenda hatua za ziada kwa kila unachofanya.

14. Usitoe ushauri kwa mtu ambaye hajakuomba, usichukue ushauri kwa ambaye hujamwomba.

15. Usijisumbue kuwabadilisha watu, watu huwa hawabadilishwi.

16. Shukuru kwa kila jambo, pokea kila hali unayokutana nayo na igeuze kuwa bora.

17. Usilalamike wala kumlaumu yeyote kwa chochote, beba jukumu la maisha yako.

18. Fanya kilicho sahihi mara zote na siyo kilicho rahisi.

19. Jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA na upate vitabu na chambuzi zake mwaka mzima. Kujiunga fungua;

https://www.t.me/somavitabutanzania

20. Ianze kila siku yako kwa maarifa na hamasa kutoka AMKA MTANZANIA, fungua;

https://amkamtanzania.com

Ni Hayo 20 tu Rafiki Yangu,

Yafanye Kila Siku.

Kumbuka nipo na wewe kwenye safari hii ya mafanikio.

Nakupenda.

Rafiki na Shabiki Yako.

Bwana AmiriRamadhani|CopywriterOfSomaVitabuTanzania|

RUKSA; Kusambaza ujumbe huu kwa wengine ili nao waweze kubora zaidi ya jana.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post