Pokea Zawadi Yako Leo Siku Ya Wapendanao!…

Wakati wa uhai wake, na akiwa kwenye kilele cha mafanikio, John D. Rockefeller aliwahi kunukuliwa akisema; “uwezo wa kuendana na watu ni ujuzi ambao unaweza kununuliwa kama sukari au kahawa na niko tayari kulipa zaidi kwa mwenye uwezo huo kuliko kitu kingine chini ya jua.”

Pamoja na umuhimu huu mkubwa na thamani iliyopo kwenye uwezo wa kujenga mahusiano na kushawishi wengine, bado ni elimu ambayo imekuwa haitolewi kwenye mfumo rasmi wa elimu.

Kukabiliana na watu ni moja ya jukumu gumu ambalo kila mtu anapitia kwenye maisha.

Haijalishi kama upo kwenye ajira, biashara au mama wa nyumbani, kuna nyakati unajikuta kwenye wakati mgumu kutokana na wale unaokabiliana nao.

Tafiti zinaonesha kwamba asilimia 15 ya mafanikio ya mtu yanatokana na ujuzi alionao, huku asilimia 85 ikitokana na mahusiano yake na ushawishi kwa wengine.

Kwenye kila tasnia, watu wanaolipwa zaidi ni wale wanaoweza kuendana na watu wengine vizuri, wanaoweza kuongoza na kuibua hamasa kwa wengine.

Ndio maana hakukosea aliyesema Mahusiano ni kazi…

Hakuna kitu chenye thamani kwenye maisha ambacho hakihitaji kazi katika kukijenga na kukilinda.

Huwa tunafikiria kazi na biashara tunazofanya ndiyo zinahitaji kuweka kazi na juhudi, huku vitu vingine tukitegemea vitokee vyenyewe, bila sisi kuweka kazi.

Hapo ndipo wengi wanapokwama, kwa kutokuweka kazi kwenye maeneo mengine ya maisha yao, yanaanguka na hivyo kupelekea kuanguka kwenye yale wanayoweka kazi pia.

Moja ya maeneo ambayo huwa tunayasahau sana ni mahusiano, huwa tunaamini tukifanya kazi au biashara zetu na kuingiza kipato cha kutosha, basi mahusiano yetu yatakuwa bora.

Lakini huo siyo ukweli, mahusiano huwa hayawi bora yenyewe, bali mahusiano yanakuwa bora kama yanajengwa.

Na hapa ni mahusiano yote, kuanzia ya ndoa au mapenzi, familia, urafiki na mengineyo, kazi inahitajika katika kujenga mahusiano ambayo ni bora na imara.

Kila mahusiano yanahitaji muda, muda wa kuwa na wale ambao una mahusiano nao ni hitaji muhimu katika kujenga na kuimarisha mahusiano.

Kadiri watu wanavyokosa muda wa kuwa pamoja, ndivyo mahusiano yanavyodhoofu.

Kila mahusiano yana migogoro na hali ya kupishana au kutokuelewana, inahitaji kazi kutatua migogoro hiyo, kuelewana na kwenda pamoja.

Wengi wamekuwa wanakimbia mahusiano kwa sababu ya migogoro, wakiamini wanaweza kuwa na mahusiano mengine yasiyo na migogoro, kitu ambacho huwa hakitokei.

Mahusiano huwa yanatupima, yanatufundisha na pia kutupa fursa mbalimbali za kupiga hatua kwenye maisha.

Tunachopaswa kufanya ni kuweka kazi ya kutosha ili kujenga na kuimarisha mahusiano muhimu kwetu.

Kwa kuliona hili ndio maana nmekuandalia zawadi ya bure kabisa.

Itakayokusaidia kuimarisha mahusiano yako mara dufu……

Je Upo Tayari Kupokea Zawadi Yako LEO Siku Ya Wapendanao?….

Kama Upo Tayari Andika Neno “NIPO”.

Kwenda WHATSAPP NAMBA 0752977170 Ili Kupokea Zawadi Yako Ndani Ya Masaa 24tu!.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,

Bwana Rama, Copywriter Wa SOMA VITABU TANZANIA.

www.somavitabu.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post