Huyu Hapa Ndiye Unayepaswa Kumkabidhi Maisha Yako

Hii inamuhusu tu yule ambaye anataka kupiga hatua kubwa kwenye maisha yake kama wewe siye ruksa kuishia hapa.

Ni kweli huna pesa za kufanya biashara kwa sasa, lakini je, ukiendelea kukaa hivyo na kusubiri pesa zitakuja?

Ni kweli umeumizwa katika mahusiano yako yaliyopita lakini je ukiendelea kulia maisha yatabadilika?

Ni kweli umefeli katika elimu yako, lakini je ukiendelea kuwaza kufeli kwako maisha yatabadilika?

Ni kweli wazazi wako wameshindwa kukusaidia lakini je, ukiendelea kuwalaumu na kuwanung’unikia maisha yako yatakuwa bora?

Uko hapo ulipo sasa kwa sababu ndivyo ulivyojitengeneza.

Na kama unataka kuwa tofauti na ulivyo sasa, lazima ujitengeneze upya.

Matajiri wanaamini wao ndiyo wamejitengeneza wenyewe na hivyo wanawajibika na maisha yao.

Lakini masikini wanaamini maisha waliyonayo yametengenezwa na wengine na hakuna wanachoweza kufanya kuyabadili.

Masikini hujiona ni watu wa kuonewa na kuna njia tatu wanazotumia kuonesha hilo.

Njia ya kwanza ni kulaumu, masikini hulaumu kila kitu kwamba ndiyo kimewafikisha walipo.

Hulaumu uchumi, serikali, mazingira, wazazi, wenza na chochote kile wanachoona ndiyo sababu ya umaskini wao.

Njia ya pili ni kuhalalisha, masikini kwa kuwa hawana fedha, utawasikia wakisema fedha siyo muhimu sana.

Na hilo linawafanya wazidi kuwa maskini, kwa sababu unapoona kitu siyo muhimu, kinakukimbia.

Njia ya tatu, ni kulalamika, masikini wana kila sababu na malalamiko kwa nini wao ni maskini.

Huwalalamikia wengine na hali mbalimbali kuwa chanzo cha wao kubaki kwenye umasikini.

Kwa kulalamika, wanajivunia wajibu wa maisha yao na kuwapa wale wanaowalalamikia, hivyo kuzidi kubaki kwenye umasikini.

Ili kuwa tajiri, amini kwamba wewe ndiye unayatengeneza maisha yako na hivyo chukua wajibu wa kuyatengeneza vyema.

Epuka kabisa kulaumu, kuhalalilisha au kulalamikia wengine.

Wewe ndiye unayepaswa kuwajibika na maisha yako, hakuna mwingine anayeweza kufanya hivyo badala yako.

Kama unataka kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako nakushauri usome eBOOK Mpya Inayoitwa TABIA ZA KITAJIRI,

Ambayo Itakufundisha Tabia Za Kuishi Kila Siku Ili Kupata Utajiri, Mafanikio Na Furaha.

Ina maana baada ya kumaliza kusoma eBOOK hii utakuwa umejifunza;

Mambo makubwa matano kuhusu utajiri, Mafanikio Na Furaha.

Kwanza utajifunza kuhusu sayansi ya utajiri na kujua kanuni za kufanyia kazi ili uweze kufika kwenye utajiri mkubwa.

Hii ni sayansi inayofanya kazi kwa yeyote anayefuata kanuni sahihi.

Hapa utajifunza kanuni hizo na ukizifuata utajiri ni lazima kwako.

Pili unakwenda kujifunza tabia kumi muhimu za kuishi kwenye kila siku ya maisha yako ili kufika kwenye utajiri.

Hizi ni tabia zilizofanyiwa tafiti na kugundulika matajiri wengi wanaziishi kila siku.

Tabia hizo kumi hazihitaji ufanye mabadiliko makubwa kwenye maisha yako, bali ni kubadili tu mtindo wa kuyaendesha maisha yako kila siku.

Kwa kuwa na mtindo mpya wa kuendesha maisha yako, unajenga utajiri mkubwa kwako bila kujali unaanzia wapi.

Tatu unakwenda kujifunza imani 17 muhimu za kujijengea ili uweze kufikia utajiri mkubwa.

 Imani na mitazamo tuliyonayo ina athari kubwa kwetu kifedha, ulipo sasa ni matokeo ya imani ulizonazo, ambazo umebeba kutoka kwenye jamii iliyojaa masikini wengi.

Hapa unakwenda kujifunza imani 17 mpya kutoka kwa matajiri na kwa kuziishi, utayabadili maisha yako na kufikia utajiri mkubwa.

Hapa utajifunza jinsi imani zinavyoathiri hisia, ambazo zinaathiri fikra, kisha maamuzi, matendo na matokeo unayopata.

Nne unakwenda kujifunza tabia 50 za kwenda kujijengea kwenye maisha yako ambazo zitakufikisha kwenye utajiri mkubwa na maisha ya mafanikio na furaha.

Hapa unapata mkusanyiko na msisitizo wa yote muhimu unayopaswa kufanyia kazi ili kufika kwenye utajiri na furaha.

Na hata baada ya kufika kwenye hatua hizo, tabia hizo 50 zinakuwa kinga kwako usianguke.

Tano ni hatua nane za kufika kwenye utajiri mkubwa.

Kitabu hiki siyo tu nadharia ya utajiri, bali pia unaondoka na hatua za kwenda kuchukua ili ufike kwenye utajiri.

Hapa utajifunza hatua nane za kutoka kwenye umasikini mpaka kwenye utajiri mkubwa, hatua ambazo ukizichukua kama unavyojifunza, nakuhakikishia hutaweza kubaki hapo ulipo sasa.

Uzuri hatua hizo hazihitaji usubiri, unaanza nazo mara moja, hapo hapo ulipo na unaanza kujenga utajiri.

Karibu sana usome eBOOK mpya inayoitwa TABIA ZA KITAJIRI, ujifunze kwa kina na kuyaelewa maarifa haya muhimu sana kwako, kisha uchukue hatua ili maisha yako yaweze kubadilika, ufike kwenye utajiri, mafanikio na furaha.

JINSI YA KUPATA KITABU.

eBOOK mpya inayoitwa TABIA ZA KITAJIRI inapatikana kwenye app ya SOMA VITABU ambayo inapatikana kwenye mfumo wa ANDROID (PLAY STORE).

Kupata app hiyo fungua kiungo hiki; http://bit.ly/somavitabuapp au nenda moja kwa moja kwenye play store kisha tafuta SOMA VITABU.

Ukishaweka app kwenye kifaa chako (simu au tablet) utakiona kitabu na kufuata mchakato wa kukinunua moja kwa moja kwenye app.

Kupata maelezo zaidi ya jinsi ya kutumia app, kununua na kusoma vitabu, fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/somavitabuapp

ZAWADI YA KITABU.

Rafiki yangu mpendwa,

Kwa kuwa umekuwa unafuatilia mafunzo ninayotoa kwa muda mrefu, nakwenda kukupa eBOOK hii ya TABIA ZA KITAJIRI KAMA ZAWADI.

Hivyo kwa siku hizi chache utakipata kitabu hiki kwa tsh elfu moja pekee (1,000/=).

Kitabu hiki kina thamani ya mamilioni kwako, ila wewe unakipata sawa na bure kabisa, kwa tsh elfu moja tu.

Lengo langu ni wewe usiwe na sababu yoyote ya kukikosa, kwa sababu nataka sana uyabadili na kuyaboresha maisha yako na maarifa yaliyo kwenye kitabu hiki ndiyo unayahitaji sana.

Chukua hatua sasa rafiki yangu, zawadi hii ni ya muda mfupi, bei ya kitabu itakuwa kubwa zaidi baadaye hivyo usikubali kukosa.

Utajiri ni haki na wajibu wako, kama wapo wengine walioweza kufikia utajiri, na wewe pia unaweza kuufikia. Unachohitaji ni kuijua kanuni sahihi na kuifuata.

Kitabu hiki cha TABIA ZA KITAJIRI kina kanuni hizo, wajibu wako ni kuzijua na kuzifuata na utajiri kwako unakuwa swala la muda tu.

Jipatie kitabu chako sasa kwa bei ya zawadi, fungua; http://bit.ly/somavitabuapp

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post

Mpaka Sasa Hujafanikiwa Kuongeza Kipato Chako Kwa Sababu Ya Kukosa Maarifa Jifunze Mbinu Sahihi Zitakazokusaidia Kuongeza Kipato Chako Leo.Mpaka Sasa Hujafanikiwa Kuongeza Kipato Chako Kwa Sababu Ya Kukosa Maarifa Jifunze Mbinu Sahihi Zitakazokusaidia Kuongeza Kipato Chako Leo.

Hapo Zamani, Mtaalamu  – Benjamin_Franklin, Alinukuliwa Akisema, “Sote tumezaliwa wajinga, tunahitaji bidii kidogo ili kuwa na maarifa, au bidii kubwa sana ili kuendelea kubaki wapumbavu. Baadhi huchagua njia ya pili.”