Mafanikio sio mchezo wa kubahatisha.
Ni mchezo wa kuzifuata kanuni na kuziishi kila siku.
Hakuna kingine kinachowatofautisha wanaotajirika na wanaobaki masikini kama tabia.
Hivyo kwa kuzijua tabia za kitajiri na kuziishi kwenye maisha yako ya kila siku, unakuwa kwenye nafasi nzuri ya kufikia utajiri pia.
Huenda kwa kusoma hapa na kusikia mambo ya utajiri umejisikia vibaya, na kama ndivyo basi hiki kitabu ni chako, kwani kinaenda kuvunja kikwazo kikubwa kinachokuzuia kuwa tajiri.
Mambo mengi sana yamekuwa yanasemwa kuhusu utajiri na matajiri, lakini mengi kati ya mambo hayo siyo sahihi.
Mengi yanayosemwa kuhusu utajiri na matajiri, hasa kwa upande hasi siyo sahihi na yamewafanya wengi kuendelea kubaki kwenye umasikini.
Ukweli ni kwamba utajiri ni mzuri, pale mtu unapoweza kuwa na fedha unazohitaji kwa ajili ya mahitaji ya maisha yako, maisha yanakuwa bora sana kwako.
Na pale unapokosa fedha, maisha yanakuwa siyo bora, kuanzia kwako binafsi na hata kwenye mahusiano yako.
Hivyo yeyote anayesema utajiri siyo muhimu, anajidanganya tu na kujipa moyo.
Fedha na utajiri ni vitu muhimu sana kwenye maisha yetu ya kila siku.
Ukweli wa kuumiza ni kwamba katika kila jamii, yaani ukianza na dunia nzima, ukaja kwenye nchi, ukaenda kwenye mkoa, wilaya na hata mtaa, utajiri umegawanyika kwenye namba ambazo ni sawa kwenye kila eneo.
Namba hizo ni 99/1, 95/5 na 90/10.
Namba ya kwanza ni 99 kwa 1, ikimaanisha asilimia moja ya watu ndiyo wenye utajiri mkubwa mno duniani, kushinda asilimia 99 kwa ujumla.
Hii ina maana katika watu 100, mmoja ana utajiri mkubwa kushinda jumla ya utajiri wa wale wengine tisini na tisa.
Namba ya pili ni 95 kwa 5, ikimaanisha asilimia 5 ya watu kwenye eneo ndiyo wanaokuwa na utajiri na uhuru wa kifedha, huku asilimia 95 wakiwa na maisha ya kawaida au ya chini kabisa.
Wale waliopo kwenye asilimia 5 hata kama siyo matajiri kama asilimia 1, lakini maisha yao yana uhuru mkubwa.
Hawa hutawaona kwenye orodha ya matajiri wakubwa, lakini wameshafikia uhuru wa kifedha na wanaishi maisha bora sana kwao.
Namba ya tatu ni 90 kwa 10, ambapo asilimia 10 ya watu wanakuwa na utajiri au maisha ya juu, huku asilimia 90 ya watu wakiwa na maisha magumu sana.
Hii ina maana katika watu 100, watu 90 wapo kwenye hali ngumu sana kifedha, hawana uhakika kesho au mwezi ujao wanaendeshaje maisha yao.
Hawa ni watu ambao kila wakati wanaishi kwa wasiwasi kwa sababu hawana msingi wowote kifedha.
Namba sahihi kwa wewe kuwa ni kwenye 95/5, unapaswa kuwa kwenye asilimia 5 ya juu kwenye jamii yako na hata dunia kwa ujumla kwa kuwa na uhuru wa kifedha, kuwa na fedha ambazo unaweza kuendesha maisha yako kwa namna unavyotaka wewe.
Hii ni namba sahihi kwako kuwa kwa sababu huhitaji kushindana na yeyote na wala huhitaji kuwa na bahati kuifikia.
Kwa kujijengea tabia nzuri, kuweka juhudi kubwa na kutokukata tamaa, utaweza kufika kwenye asilimia 5 ya juu na maisha yako yakawa bora sana.
Utajiri ni mchezo, mchezo ambao una kanuni zake na sheria zake, na ili uweze kushinda mchezo huu, lazima uzijue kanuni na uzishike sheria.
Haiwezekani kabisa kwa mtu ambaye hajui kanuni za mpira wa miguu, hana mazoezi akaenda uwanjani na kushinda.
Wengi wamekuwa wanaingia kwenye mchezo wa utajiri kama vile ni kitu cha kubahatisha, hawajui kanuni wala sheria, hawana maandalizi na kinachotokea ni kushindwa vibaya sana.
Kwenye kitabu hiki cha TABIA ZA KITAJIRI, unakwenda kujifunza mambo makubwa matano kuhusu utajiri.
Kwanza utajifunza kuhusu sayansi ya utajiri na kujua kanuni za kufanyia kazi ili uweze kufika kwenye utajiri mkubwa.
Hii ni sayansi inayofanya kazi kwa yeyote anayefuata kanuni sahihi.
Hapa utajifunza kanuni hizo na ukizifuata utajiri ni lazima kwako.
Pili unakwenda kujifunza tabia kumi muhimu za kuishi kwenye kila siku ya maisha yako ili kufika kwenye utajiri.
Hizi ni tabia zilizofanyiwa tafiti na kugundulika matajiri wengi wanaziishi kila siku.
Tabia hizo kumi hazihitaji ufanye mabadiliko makubwa kwenye maisha yako, bali ni kubadili tu mtindo wa kuyaendesha maisha yako kila siku.
Kwa kuwa na mtindo mpya wa kuendesha maisha yako, unajenga utajiri mkubwa kwako bila kujali unaanzia wapi.
Tatu unakwenda kujifunza imani 17 muhimu za kujijengea ili uweze kufikia utajiri mkubwa. Imani na mitazamo tuliyonayo ina athari kubwa kwetu kifedha, ulipo sasa ni matokeo ya imani ulizonazo, ambazo umebeba kutoka kwenye jamii iliyojaa masikini wengi.
Hapa unakwenda kujifunza imani 17 mpya kutoka kwa matajiri na kwa kuziishi, utayabadili maisha yako na kufikia utajiri mkubwa.
Hapa utajifunza jinsi imani zinavyoathiri hisia, ambazo zinaathiri fikra, kisha maamuzi, matendo na matokeo unayopata.
Nne unakwenda kujifunza tabia 50 za kwenda kujijengea kwenye maisha yako ambazo zitakufikisha kwenye utajiri mkubwa na maisha ya mafanikio na furaha. Hapa unapata mkusanyiko na msisitizo wa yote muhimu unayopaswa kufanyia kazi ili kufika kwenye utajiri na furaha.
Na hata baada ya kufika kwenye hatua hizo, tabia hizo 50 zinakuwa kinga kwako usianguke.
Tano ni hatua nane za kufika kwenye utajiri mkubwa. Kitabu hiki siyo tu nadharia ya utajiri, bali pia unaondoka na hatua za kwenda kuchukua ili ufike kwenye utajiri.
Hapa utajifunza hatua nane za kutoka kwenye umasikini mpaka kwenye utajiri mkubwa, hatua ambazo ukizichukua kama unavyojifunza, nakuhakikishia hutaweza kubaki hapo ulipo sasa.
Uzuri hatua hizo hazihitaji usubiri, unaanza nazo mara moja, hapo hapo ulipo na unaanza kujenga utajiri.
ZAWADI YA EBOOK.
Rafiki yangu mpendwa,
Kwa kuwa umekuwa unafuatilia mafunzo ninayotoa kwa muda mrefu,
Nakwenda kukupa EBOOK hii ya TABIA ZA KITAJIRI KAMA ZAWADI.
Bei halisi ya EBOOK hii ni TSH 10,000/=.
Hivyo kwa siku ya LEO utaipata EBOOK hii kwa TSH elfu moja(1) pekee (1,000/=).
OKOA TSH 9,000 NZIMA LEO.
Lengo langu ni wewe usiwe na sababu yoyote ya kuikosa,
Kwa sababu nataka sana uyabadili na kuyaboresha maisha yako na maarifa yaliyo kwenye kitabu hiki ndiyo unayahitaji sana.
Chukua hatua sasa rafiki yangu,
Zawadi hii ni ya muda mfupi,
Bei ya EBOOK hii itakuwa kubwa zaidi baadaye hivyo usikubali kukosa.
Utajiri ni haki na wajibu wako, kama wapo wengine walioweza kufikia utajiri, na wewe pia unaweza kuufikia.
Unachohitaji ni kuijua kanuni sahihi na kuifuata.
EBOOK hii ya TABIA ZA KITAJIRI ina kanuni hizo, wajibu wako ni kuzijua na kuzifuata na utajiri kwako unakuwa swala la muda tu.
Jipatie EBOOK Yako sasa kwa bei ya zawadi, fungua; http://bit.ly/somavitabuapp.
Kwa msaada zaidi wasiliana na namba 0752977170.
Good book
Karibu, umeshapata nakala? Kama bado tuwasiliane 0678977007