Siku moja Baba alirudi nyumbani akiwa amechelewa kutoka kazini.
Alikuwa amechoka huku akiwa amekasirika.
Alipofika nyumbani alimkuta mwanae wa miaka mitano akimsubiri mlangoni.
Mtoto alipomuona baba yake , alimwambia “ Baba ninaweza kukuuliza swali?”
Baba akajibu, “ndio, unaweza ni nini shida?
Mtoto akamuuliza, “baba, unaingiza kiasi gani cha pesa kwa li saa?”
Baba akamjibu kwa hasira, “ Haikuhusu. Kwanini unaniuliza hilo swali ?
Mtoto akasema , “ Ninataka kujua. Tafadhali niambie, unaingiza kiasi gani kwa li saa?”
Baba akajibu kwa hasira, “kwani ni lazima.
Ninaingiza elfu (5) kwa li saa.”
Akiwa ameinamisha kichwa chini mtoto akajibu, “Oh! Baba , unaweza kunikopesha elfu mbili mia tano.?”
Baba alikasirika, “akamwambia kama sababu ya kuuliza maswali yote hayo ni kwa ajili ya kwenda kununua midoli au upumbavu mwingine nenda haraka chumbani ukalale”.
Kusikia hivyo, mtoto akaondoka kinyonge kwenda kwenye chumba chake na kujifungia.
Dakika chache baadae hasira zilipoisha baba alianza kufikiria yale mazungumzo na kijana wake , alifikiria, “Labda kuna kitu mwanae anataka kununua na hiyo pesa kwa sababu haombagi pesa mara kwa mara.”
Baba alienda kwenye chumba cha mwanae na kufungua mlango.
Akamsogelea kijana wake na kumuuliza” Mtoto wangu umelala?”.
Mtoto akajibu, “ Hapana Baba, nipo macho.”
Baba akamwambia mwanae hii hapa pesa ulioniomba.”
Baada ya mtoto kupewa pesa alitabasamu . Akamshukuru baba yake.
Mtoto akaelekea kwenye kapu na kuchukua pesa zake alizozihifadhi.
Baba baada ya kuona mwanae alikuwa na hela , akaanza kukasirika.
Mtoto akaanza kuhesabu pesa zake.
Baba akafoka, “ Kwanini umeomba hela hakati ulikuwa unazo?”
Mtoto akajibu,” Kwa sababu sikuwa nazo hapo kabla lakini sasa hivi ni nazo.”
Mtoto akamkabidhi zile pesa zote baba yake na kumwambia, “ Baba nina elfu (5) . Sasa hivi. Ninaweza kulinunua li saa la muda wako.?
Tafadhali wahi kurudi nyumbani kesho. Ningependa kula chakula cha usiku na wewe.”
Baba alibaki ameduwaa. Alimbeba mwanae na kumuomba msamaha.
Tunajifunza tufanye kazi kwa bidii lakini tukumbuke kutumia muda wetu na wale tunaowapenda.
Lazima kuwe na mipaka kati ya kazi na familia.
Muda na pesa ni vitu viwili unavyoweza kutumia kupima vipaumbele vya mtu na hata kuweza kutabiri kwa uhakika mtu huyo ataishia wapi.
Tukianza kwenye vipaumbele, hata kama mtu hajakuambia chochote, ukiangalia jinsi anavyotumia muda na pesa zake, utajua wazi vipaumbele vyake ni nini.
Mtu anaposema kwamba hana muda wa kufanya kitu fulani, maana yake kitu hicho siyo kipaumbele kwake.
Kwa sababu kila mtu ana masaa 24 kwenye siku yake, na katika masaa hayo kuna vitu anafanya, ili afanye kitu fulani, inabidi aache baadhi ya vile anavyofanya sasa.
Na hapo ndipo kipaumbele kinapohusika, mtu hataacha kilicho muhimu kwake ili kufanya kisichokuwa muhimu.
Hivyo kama unajiambia huna muda wa kufanya vitu fulani, labda kujifunza, kusoma na mengine, jiambie tu ukweli, jiambie kwamba vitu hivyo siyo vipaumbele kwako, acha kujificha kwenye muda na kuwa mkweli kwako mwenyewe.
Kadhalika kwenye pesa, mtu anaposema hawezi kumudu kitu fulani, maana yake ni kwamba kitu hicho siyo kipaumbele kwake.
Tunajua kitu kinapokuwa kipaumbele hasa, mtu atafanya kila namna aweze kukimudu. Hivyo kama huna pesa za vitu fulani, jua wazi hujavipa kipaumbele, hujavifanya kuwa vitu ambavyo uko tayari kufanya chochote ili kuvipata.
Kwa upande wa kutabiri, kama mtu atafanikiwa au la, wewe angalia tu jinsi anavyotumia muda na fedha zake.
Mtu ambaye ana masaa 24 kwenye siku yake ambayo ameyajaza mambo mengi ya kufanya, lakini anakosa muda wa kujifunza, hawezi kufikia mafanikio makubwa.
Mtu ambaye kila kipato anachopata anatumia chote na anaenda mbele zaidi na kukopa kwa ajili ya matumizi, atabaki kwenye umasikini kwa kipindi chote atakachoishi kwa namna hiyo.
Usijisumbue kutabiri wengine wataishia wapi kwenye maisha yao, badala yake jitabirie wewe mwenyewe.
Jifanyie tathmini ya matumizi ya muda na fedha zako na jiulize kama ukienda hivyo utafika kule unakotaka kufika. Kama jibu ni hapana, anza kuchukua hatua sahihi sasa.
Kila siku fanya tathmini ya matumizi ya vitu hivi viwili, unapoimaliza siku yako angalia ulivyotumia muda wako na fedha zako kwa siku nzima, kisha jiulize kama ukienda hivyo kila siku utafika wapi.
Tathmini za aina hii zitakuonesha mapema wapi unakosea na utaweza kuchukua hatua sahihi ili usipotee.
Karibu upate vitabu mbalimbali kwa kufungua www.amkamtanzania.com/vitabu na www.t.me/somavitabutanzania.
Rafiki yako mpendwa,
Sir Rama |Copywriter| |Sales Officer Of Soma Vitabu Tanzania|