Je, Ungependa Kupata Utulivu Wa Akili?
Wahenga waliwahi kusema“ Usipoziba Ufa Utajenga Ukuta”…
Hakuna anayeweza kubisha kwamba kumekuwa na ukuaji mkubwa sana wa teknolojia kwenye zama tunazoishi sasa.
Kuna maendeleo makubwa ambayo yametokea tangu kuanza kwa karne ya 21 ambayo hakuna aliyetegemea yangetokea kwa kasi kubwa hivyo.
Nani alidhani angeweza kuwasiliana na mtu aliye bara la mbali kwa kuonana uso kwa uso bila hata ya kutumia gharama kubwa?
Nani alifikiri vitabu vyote duniani vingeweza kuweka mtandaoni na ikawa rahisi mtu kuvipata na kuvisoma?
Nani alifikiri kungekuja simu za mkononi (simu janja) ambazo unaweza kuzitumia kufanya kila kitu kama unavyotumia kompyuta, kuanzia kuwasiliana, kutunza kumbukumbu, kupiga picha, kurekodi sauti na video, kuuza na kununua na hata kujifunza?
Haya ni maendeleo makubwa, ambayo mtu aliyefariki kwenye karne ya 20, akifufuliwa leo atashangaa mno kwa maendeleo haya na angetegemea kuona maisha ya watu yakiwa bora kutokana na maendeleo haya makubwa.
Lakini hapo ndipo atakaposhangazwa zaidi, kwani licha ya maendeleo makubwa ya teknolojia atakayokuwa ameyaona, atagundua maisha ya watu yako hovyo kuliko kipindi ambacho teknolojia hizo hazikuwepo.
Atashangaa kuona watu wakiwa wamechoka, wana msongo na hawana muda kabisa.
Atashangaa kuona watu wakitumia muda wao mwingi kwenye simu zao, kwa mambo ambayo hayana manufaa kwao.
Atashangaa jinsi watu wanaonena wivu kwa mambo ambayo wanayaweka kwenye mitandao ya kijamii.
Ujumbe atakaokuwa ameupata ni mmoja, kwamba teknolojia hizi mpya ambazo zina nguvu ya kufanya maisha ya wengi kuwa bora, zimegeuka kuwa gereza lililowafungia wengi na hawana tena uhuru wa kuyaishi maisha yao.
Ni dhahiri kwamba teknolojia mpya, hasa simu janja na mitandao ya kijamii, vimekuwa tatizo kubwa kwa wengi. Kila mtu analalamika jinsi vitu hivyo vinavyochukua muda mwingi, kuleta uchovu na hata msongo.
Wanaotengeneza na kuendesha teknolojia hizo hawajali kuhusu hilo, kwani kadiri unavyozitumia kwa muda mrefu, ndivyo wao wanavyopata faida. Hivyo wamejipanga kuhakikisha watumiaji wanaendelea kuwa wafungwa kwenye teknolojia hizo.
Na kwa kuwa teknolojia hizi ni mpya, hakuna mwenye uzoefu wa jinsi ya kukabiliana nazo, hivyo watu wanaingia kwenye teknolojia hizo mpya kwa kuhadaiwa watanufaika sana, lakini kinachotokea ni wanageuzwa kuwa wafungwa.
Leo nina habari njema kwako, habari hizo ni kupatikana kwa mwongozo wa kuzitumia teknolojia hizi mpya vizuri na ukombozi wa ufungwa ambao teknolojia hizo zimetengeneza kwako.
Nimekuandalia kitabu kinachoitwa EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI, kitabu kinachokuonesha jinsi teknolojia mpya zinavyokufanya mtumwa na njia za kuondoka kwenye utumwa huo.
Kupitia kitabu hiki utajifunza mambo saba makubwa ambayo yatakufanya uwe huru na utumie teknolojia hizi kwa manufaa makubwa kwako.
Moja utajifunza jinsi ubongo wako unavyofanya kazi na namna teknolojia mpya zinavyotumia ubongo huo kukufanya kuwa mtumwa. Teknolojia mpya zimetengenezwa kwa namna ambayo zitajenga uteja/uraibu kwenye ubongo wako. Kwa kujua njia hiyo utaweza kuepuka kuingia kwenye utumwa wa teknolojia hizo.
Mbili utajifunza kuhusu zama tunazoishi sasa, zama za maarifa na taarifa lakini ambazo zimegeuka kuwa zama za usumbufu. Utajifunza zama hizi za usumbufu zimetengeneza makundi makubwa mawili, wachache wanaonufaika sana, kama Mark Zuckerberg ambaye ni mmiliki wa Facebook na wengi ambao ni kama watumwa wa wachache hao wanaonufaika.
Tatu utajifunza jinsi ya kujua kama tayari umeshanasa na kuwa mtumwa wa teknolojia hizo mpya. Unaposoma hapa unaweza kusema wewe hujawa mtumwa, unatumia kwa kupanga mwenyewe, lakini nikuambie kitu kimoja, kwa sehemu kubwa sana umeshakuwa na utaziona dalili kwa kusoma kitabu hiki.
Nne utajifunza jinsi ya kuondoka kwenye utumwa wa kidijitali ambao umeshaingia. Baada ya kuona jinsi ambavyo umenasa kwenye utumwa huo, utajifunza njia za kujinasua. Hapa utajifunza jinsi ya kuizidi ujanja simu janja yako.
Tano utajifunza falsafa mpya ya kuendesha maisha yako kwa uhuru katika zama hizi za usumbufu. Pamoja na kujifunza kuhusu zama hizo na jinsi ya kuondokana na utumwa wake, usumbufu wake hautaisha, teknolojia mpya zinaendelea kugunduliwa kila siku na zikiwa na ushawishi mkubwa. Hivyo unahitaji kuwa na falsafa unayoitumia kuchagua huduma za kidijitali utakazochagua kutumia kwa manufaa yako.
Sita utajifunza jinsi ya kutumia akili yako kuvunja uraibu wowote ambao umeshajijengea. Kama tulivyoona, huduma za kidijitali zinatumia jinsi ubongo unavyofanya kazi kukuingiza kwenye utumwa. Hivyo wewe unapaswa kuutumia ubongo wako vizuri kuondoka kwenye utumwa huo.
Saba utajifunza sababu kumi kwa nini unapaswa kuondoka kwenye mitandao yote ya kijamii sasa hivi. Hizi ni sababu ambazo zimechambua jinsi matumizi ya mitandao ya kijamii yalivyo na athari kwenye akili yako, utulivu wako, mahusiano yako, uchumi wako na hata imani yako. Kwa kuzijua sababu hizi kumi, utajionea mwenyewe jinsi ulivyorudi nyuma tangu umeanza kutumia mitandao hiyo na hivyo kuachana nayo ili kuepuka madhara yake.
Mwisho kabisa utajifunza njia za kutumia kufanya maamuzi iwapo utumie huduma ya kidijitali. Utajifunza jinsi ya kutumia vigezo vitatu vya AFYA, UTAJIRI na HEKIMA katika kuchagua na kutumia teknolojia mpya, ambazo zitakuwa na manufaa kwako badala ya kukufanya mtumwa.
Tuko kwenye vita, adui mkuu anajua yuko vitani ila wanaolengwa hawajui. Hivyo unapaswa kuwa na maandalizi mazuri ya kupambana na vita hii ili uweze kutoka salama na siyo kuwa mfungwa.
Pata na usome kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI ili upate mbinu za kupambana kwenye vita hii na kutoka ukiwa mshindi. Kitabu hiki kimechapwa kwa nakala ngumu (hardcopy).
LEO utawekeza TSH 14,999 TU! Badala Ya TSH 20,000 (OKOA TSH 5,000 NZIMA).
Tumetoa OFA hii ya muda mfupi kwa sababu ya maombi ya clients wetu wengi, ili kukipata piga simu namba 0752 977 170 na utaletewa au kutumiwa kitabu chako popote ulipo Tanzania na Afrika Mashariki.
Nb. OFA Hii Inaisha Siku Ya IJUMAA Ya Tarehe 25/6/2021, saa nne kamili usiku.
MUHIMU; Kama utanunua na kusoma kitabu hiki na ukaona hakina manufaa yoyote kwako, unaruhusiwa kukirudisha na ukarejeshewa fedha zako. Hivyo chukua hatua sasa, huna cha kupoteza lakini una mengi ya kupata, yatakayokuweka huru kwenye zama tunazoishi sasa.