Nani Mwingine Anataka Kuwa Na Ushawishi Zaidi?
Rafiki Yangu Mkubwa,
Kama na wewe unataka kuwa na ushawishi zaidi basi makala hii inakuhusu.
Kwa sababu inaenda kukufunulia MAENEO MATATU (3) Muhimu Ya Kuzingatia Ili Uweze Kuwa na Ushawishi Zaidi.
Ina maana baada ya kumaliza kusoma makala hii fupi na kufanyia kazi yale yote utakayojifunza hapa basi utaweza kumshawishi yeyote yule,
…na hivyo hutatumia nguvu nyingi tena kushawishi.
Kama ambavyo tumeshajifunza,
…kila mtu sasa ni muuzaji,
…kila mmoja wetu kuna kitu ambacho anauza kwa wengine.
Inaweza kuwa bidhaa au huduma au hata ushawishi fulani unaotaka kuwa nao kwa wengine, yote hiyo ni kuuza.
Japokuwa kila mmoja wetu yupo kwenye mauzo, watu wamekuwa hawakai chini na kujifunza njia bora za kuuza kile wanachouza.
Badala yake wamekuwa wanafanya kwa mazoea.
Ile dhana kwamba kama una kitu basi wenye uhitaji watakuja.
Njia hiyo ilifanya kazi zamani ambapo hakukuwa na usumbufu mkubwa.
Lakini kwa zama hizi haifanyi kazi, kwanza ushindani ni mkubwa na pili watu wamevurugwa.
Hivyo ili watu wajue kwamba upo na waje kununua kile unachouza, unapaswa kuwa na mbinu bora za ushawishi.
Hapa tunakwenda kujifunza maeneo matatu ya kuzingatia ili kutengeneza ushawishi mkubwa kwa wengine na kuweza kuuza zaidi.
Mbinu za zamani za mauzo zilikuwa ni kuwalazimisha watu kununua, kuwasukuma mpaka kuhakikisha wamenunua.
Mbinu hizo zilifanya kazi kwa sababu watu hawakuwa na machaguo mengi na hawakuwa na taarifa za kutosha.
Lakini zama tunazoishi sasa, huwezi kumlazimisha mtu kununua, kwa sababu kwanza ana machaguo mengi na pili ana taarifa nyingi.
Kabla mtu hajaja kwako kununua unachouza, jua kabisa ameshakusanya taarifa za kutosha mtandaoni na kwingineko.
Kama utategemea mbinu ya kulazimisha, mteja mwenye taarifa nyingi kuliko hata wewe na mwenye uwezo wa kuchagua anunue wapi, kamwe hatonunua kwako.
Unapaswa kubadili mbinu zako za mauzo, na badala ya kutumia kulazimisha, unapaswa kutumia urafiki kuwashawishi wateja kununua.
Wateja wanashawishika kununua pale wanapoamini wewe ni rafiki yao, kwamba upo upande wao,
…kwamba unawataka wanunue unachouza kwa sababu unaamini kinakwenda kuyafanya maisha yao kuwa bora zaidi.
Hapa unakwenda kujifunza maeneo matatu ya kuzingatia ili kuweza kuwa na ushawishi na kuuza sana. Maeneo hayo ni kama ifuatavyo;
Eneo La Kwanza; Wajue Vizuri Wateja Wako.
Kitu cha kwanza muhimu kuzingatia ili uwe na ushawishi na kuuza zaidi ni kuwajua vizuri wateja wako.
Katika kuwajua vizuri wateja wako, fikra, mtazamo na hatua unazochukua, zote zinalenga kuyafanya maisha yao kuwa bora zaidi,
… kwa sababu unajua ni nini hasa wanachotaka wanapokuja kununua kwako.
Katika kuwajua vizuri wateja wako na kujenga ushawishi mkubwa,
Na haya hapa ni mambo ma 3 ya kufanyia kazi.
- Ongeza nguvu zako kwa kuzipunguza.
Anza mahusiano yako na mteja kwa kuwa upande wa chini na mteja kuwa upande wa juu.
Hii inakupa wewe nafasi ya kumwelewa vizuri mteja wako na hapo kuweza kumshawishi vizuri.
Lakini ukianza kwa kuona wewe upo juu na mteja yupo chini, hutajifunza kuhusu yeye na utashindwa kumshawishi.
- Tumia akili na moyo wako.
Ukitaka kuwashawishi wateja wako, usiongee na akili zao pekee, ongea na mioyo yao pia.
Gusa hisia zao, kwa sababu watu hufanya maamuzi ya kununua kwa hisia na kisha kuhalalisha kwa fikra.
Usiwape fikra pekee, wape na hisia pia.
- Iga matendo ya mteja wako, lakini kwa uangalifu.
Watu huwa wanashawishika kuchukua hatua pale wanapoamini kwamba mtu anayewashawishi kuchukua hatua yuko upande wao.
Na njia bora ya kuwafanya watu waamini hivyo ni kuiga matendo yao.
Unapokuwa na mteja, jaribu kuiga kile anachofanya, kama mteja amekunja mikono na wewe kunja mikono.
Kama anaongea kwa sauti ya chini na wewe ongea kwa sauti ya chini.
Kama anajigusa usoni na wewe fanya hivyo.
Kuwa makini sana unavyofanya hivyo, kwa kuhakikisha mteja haoni kwamba unamuiga, yaani aone ni kama watu mnaoendana tu, na hilo litamshawishi kuchukua hatua.
Zingatia mambo hayo matatu yanayokufanya umwelewe zaidi mteja wako na yeye atashawishika na kununua kwako.
Na Eneo La 2 na La 3 Utalikuta Ukurasa 151 wa Kitabu Hiki Kipya,
Kinachoitwa MJASIRIAMALI MJANJA.
Na uzuri leo unakipata kwa OFA Ya Tshs 19,999 Tu! Badala Ya Tshs 30,000.
Tuwasiliane Kwa Namba Hii 0752977170,
Kupata Kitabu Hiki Kipya.
Wahi Mapema Kabla OFA hii Haijakupita.
KUMBUKA; Mwisho Wa OFA Hii Ni Mwezi Huu Tarehe 30|9|2022.
Nakupenda.
Shabiki Yako Namba 1,
Bwana AmiriRamadhani|CopywriterOfSomaVitabuTanzania||MjasiriamaliMjanja|