Njia 10 Za Uhakika Kupata Mpenyo Ambazo Zitakusaidia Sana Kufanikiwa Kwenye Kazi au Biashara Unayofanya.
Rafiki Yangu Mkubwa,
Vp Hali Yako?
Mda sio mrefu utaenda kujifunza njia 10 za kupata mpenyo ambazo zitakusaidia sana kufanikiwa kwenye kazi au biashara yoyote unayoifanya.
Na ukiwa makini na kuzitumia Njia tatu (3) za mwisho zinaenda kuyabadilisha maisha yako mazima.
Mpenyo ni wazo jipya la kufanya kitu ambalo linaleta matokeo bora kuliko ambavyo ilikuwa ikifanywa awali.
Watu wote ambao wamefanikiwa sana kuna kipindi walikuwa chini kabisa, kisha wakapata mpenyo na kuutumia vizuri.
Hapa tunakwenda kujifunza njia 10 za kupata mpenyo ambazo zitaweza kukusaidia sana wewe kufanikiwa kwenye kazi au biashara unayofanya.
Jifunze hapa kisha uchukue hatua na hutabaki pale ulipo sasa.
1. Kuna Fursa Zimejificha Kila Mahali.
Watu wengi hufikiri kwamba fursa ni kitu adimu sana ambacho kinapatikana kwa bahati na kwa watu wachache.
Lakini hili siyo kweli, fursa zipo kila mahali, na hapo ulipo sasa, kwa kazi au biashara unayofanya, zipo fursa nyingi kwako kupiga hatua zaidi.
Ili kuziona na kuweza kuzitumia fursa hizi lazima uwe na mtazamo wa kuzitafuta fursa kwenye kila unachofanya na ukishazipata kuchukua hatua mara moja bila ya kuchelewa.
Wanaofanikiwa ni wale ambao wanakuwa wa kwanza kwenye fursa yoyote ile.
2. Tafuta Njia Mpya Ya Kuingiza Kipato Kila Miezi Mitatu.
Kwa kile unachofanya, kila wakati tafuta njia mpya ya kuingiza kipato kila miezi mitatu.
Watu wengi wamekuwa wanaendesha maisha yao kwa mazoea kwa kufanya kile ambacho wamekuwa wanafanya siku zote.
Hawakuzi kipato chao siyo kwa sababu fursa hazipo, ila kwa sababu hawazitafuti na kuzifanyia kazi.
Wewe jisukume kila miezi mitatu uje na njia mpya ya kuingiza kipato. Kumbuka, atafutaye hupata, asiyetafuta hapati.
3. Jitofautishe Na Wengine.
Njia ya uhakika ya kupata mpenyo wa kibiashara au hata kwenye kazi ni kujitofautisha kabisa na wengine.
Hakikisha kwamba kuna kitu ambacho watu wanakipata kwako, ambacho hawawezi kukipata sehemu nyingine yoyote ile.
Kile unachofanya kiwe cha kipekee na chenye manufaa makubwa kwa wale wanaokutegemea na hapo utaweza kuwavutia wengi zaidi.
4. Kazana Kuwanufaisha Wengine Kabla Hujajifikiria Wewe.
Kinachowazuia watu wengi kufanikiwa ni ubinafsi uliopitiliza. Watu wamekuwa wanajifikiria wao wenyewe zaidi kuliko wanavyowafikiria watu wengine.
Hivyo kwa kile mtu anachofanya, anajiuliza nanufaikaje kwanza mimi. Wewe usijiulize hivyo, bali uliza wengine wananufaikaje kupitia kile unachofanya.
Ukiweka mbele maslahi ya wengine, utaweza kupata mpenyo wa kufanikiwa sana kwenye kile unachofanya.
5. Tengeneza Na Kuza Mtandao Wako.
Ni kupitia mtandao wako ndipo unapojifunza na kupata mawazo ya tofauti, ambayo ukiyatumia utaweza kufanikiwa sana kwenye kile unachofanya.
Unahitaji kuwa na mtandao mzuri wa wale ambao mnafanya kitu kimoja na kupitia mtandao huo utajifunza njia bora kabisa za kufanya unachofanya.
Pia unahitaji kuwa na mtandao wa nje ya kile unachofanya, na hapo utaweza kujifunza vitu vinavyofanyika kwingine na jinsi ya kuvitumia kwenye kile unachofanya.
6. Ondoa Kabisa Hatari Kwa Mteja.
Moja ya vitu vinavyowafanya wateja kusita kuchukua hatua ni kukosa uhakika wa kile wanachoshawishiwa kununua.
Wateja wanakuwa na hofu kwamba wanaweza kupoteza fedha, kama watanunua kitu ambacho hakiwafai.
Njia bora kwako kutumia ili kuwapa wateja uhakika ni kuondoa kabisa hatari kwao.
Hapa unawapa uhakika kwamba iwapo walichonunua hakitawafaa, basi wataweza kupata kitu kingine au wakarejeshewa fedha walizolipa, bila ya usumbufu wowote.
Kwa kuondoa hatari kwa mteja, unatengeneza mpenyo wa biashara yako kukua zaidi.
7. Kuwa Na Njia Mbadala Za Kupata Mawazo Bora.
Wazo moja bora linaweza kuwa na matokeo makubwa sana kwenye biashara yako.
Lakini wafanyabiashara wengi wamekuwa hawapati mawazo bora kwa sababu wanajiwekea ukomo wa wapi pa kupata mawazo yao.
Unapaswa kuwa na njia nyingi na mbadala za kupata mawazo bora ya kuiwezesha biashara yako kukua zaidi.
Kwa kifupi, kila wakati na kwa kila unachofanya, jiulize ni kipi unajifunza unachoweza kutumia kwenye biashara yako.
Mfano umeenda kwenye mgahawa kupata chakula, ukapata huduma nzuri au mbovu, ondoka hapo na somo la vitu gani vya kuzingatia au kuepuka kwenye biashara yako.
Kila unachokutana nacho au kupitia kwenye biashara yako, hakikisha unaondoka na hatua za kwenda kuchukua kwenye biashara yako.
Rafiki Yangu,
Habari njema ni kwamba njia 3 za mwisho ambazo zinaenda kuyabadilisha maisha yako mazima utazikuta kwenye SURA YA 5 Ya Kitabu Hiki Kipya Kinachoitwa MJASIRIAMALI MJANJA.
Na bahati uliyonayo leo hii badala ya kuwekeza Elfu 30 unakipata kwa Tshs 19,999Tu!
Kwa msaada zaidi.
Tuwasiliane kwa namba hii 0752977170.
Karibu Sana.
Bwana AmiriRamadhani|CopywriterOfSomaVitabuTanzania||Mjasiriamali|