Ni kauli aliyotoa Mr DAVID wakati anahojiwa na BBC.
Pale David alipoamua kupumzika kutumia mitandao ya kijamii,
Hakuamini kama angeweza kukaa nje ya mitandao ya kijamii kwa zaidi ya mwaka.
Lakini kwa muda wa wiki hizo 65 kati ya mwaka 2016 na 2017,
Alifanikisha lengo lake la kutokutumia facebook ,instagram na twitter (mitandao ya kijamii).
Anasema,
Wiki ya kwanza ilikuwa ngumu.
Wiki ya pili ilikuwa nzuri,
Baada ya siku 14 (wiki mbili) kuwa nje ya mitandao ya kijamii anashangazwa na anaanza kuona mabadiliko hasa hasa kwenye matumizi yake ya muda,
Akagundua ndani ya siku moja anapata masaa mengi ya kupumzika tofauti na hapo kabla.
Anahisi vizuri na anaanza kutumia uwepo wa akili kwenye kila anachofanya.
David kipindi anaishi San Francisco,
Alikuwa huru lakini alikosa ufanisi kwenye kazi zake.
Kwa sababu muda mwingi alikuwa anashinda kwenye mitandao ya kijamii,
Kilikuwa ni kitu cha kwanza kufanya baada ya kutoka kazini na kuangalia wenzake wame posti nini,
Kiukweli hali ilikuwa mbaya zaidi wastani kwa siku alikuwa anatumia masaa matatu (3) kuzurura kwenye mitandao ya kijamii.
Mwanzoni mwa mwaka 2018 alihama San Francisco na kuhamia New York.
Lengo na madhumuni kuhamia New York, ilikuwa kutafuta changamoto mpya kwenye fani ya mitindo.
Baada ya muda wa wiki 65 kupita alirudi kutumia mitandao ya kijamii,
Kipindi hiki alitumia kwa ajili ya kujifunza zaidi kuhusu fani ya mitindo na sio nje na hapo.
Kwa hiyo taarifa alizokuwa anazipata ni zile zinazohusu fani ya MITINDO tu.
Anakiri kwamba kilichomsaidia zaidi ni KUTUMIA UWEPO WA AKILI na FALSAFA BORA YA MATUMIZI YA MITANDAO YA KIJAMII, kila mara anapotaka kuingia kwenye mitandao ya kijamii.
Hizi mbinu mbili alizotumia Mr DAVID unakwenda kujifunza kwa kina ndani ya kitabu kinachoitwa EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI.
Tunajifunza kwamba,
Ili tuweze kuvunja uraibu wowote, tunapaswa kutumia akili zetu vizuri, kama zilivyotuwezesha kujenga tabia, hivyo pia zitatuwezesha kuvunja tabia na uraibu.
Kama unataka kuvunja tabia za kimaskini ambazo zinakupotezea muda na zina kurudisha nyuma na huzipendi, huna budi kutumia uwepo wa akili (mindful) , mbinu hii itakusaidia sana kuvunja tabia nyingi mbaya.
Hii ni mbinu ambayo imenisaidia mimi na maelfu ya watu utajifunza kwa kina kwenye sura ya sita (6) ndani ya kitabu kipya kinachoitwa EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI, kama unacho kitabu chako nenda moja kwa moja kwenye sura ya (6) ukurasa wa 125.
Kama bado hujapata nakala yako wasiliana na namba 0752977170 utaletewa au utatumiwa popote ulipo ndani ya AFRIKA MASHARIKI.
Kupitia kitabu hiki utajifunza mambo saba(7) makubwa ambayo yatakufanya uwe huru na kuondokana na usumbufu unao kuingiza kwenye utumwa.
Moja utajifunza jinsi ubongo wako unavyofanya kazi na namna teknolojia mpya zinavyotumia ubongo huo kukufanya kuwa mtumwa.
Teknolojia mpya zimetengenezwa kwa namna ambayo zitajenga uteja/uraibu kwenye ubongo wako.
Kwa kujua njia hiyo utaweza kuepuka kuingia kwenye utumwa wa teknolojia hizo.
Mbili utajifunza kuhusu zama tunazoishi sasa, zama za maarifa na taarifa lakini ambazo zimegeuka kuwa zama za usumbufu. Utajifunza zama hizi za usumbufu zimetengeneza makundi makubwa mawili, wachache wanaonufaika sana, kama Mark Zuckerberg ambaye ni mmiliki wa Facebook na wengi ambao ni kama watumwa wa wachache hao wanaonufaika.
Tatu utajifunza jinsi ya kujua kama tayari umeshanasa na kuwa mtumwa wa teknolojia hizo mpya.
Unaposoma hapa unaweza kusema wewe hujawa mtumwa, unatumia kwa kupanga mwenyewe, lakini nikuambie kitu kimoja, kwa sehemu kubwa sana umeshakuwa na utaziona dalili kwa kusoma kitabu hiki.
Nne utajifunza jinsi ya kuondoka kwenye utumwa wa kidijitali ambao umeshaingia.
Baada ya kuona jinsi ambavyo umenasa kwenye utumwa huo, utajifunza njia za kujinasua.
Hapa utajifunza jinsi ya kuizidi ujanja simu janja yako.
Tano utajifunza falsafa mpya ya kuendesha maisha yako kwa uhuru katika zama hizi za usumbufu.
Pamoja na kujifunza kuhusu zama hizo na jinsi ya kuondokana na utumwa wake, usumbufu wake hautaisha, teknolojia mpya zinaendelea kugunduliwa kila siku na zikiwa na ushawishi mkubwa.
Hivyo unahitaji kuwa na falsafa unayoitumia kuchagua huduma za kidijitali utakazochagua kutumia kwa manufaa yako.
Sita utajifunza jinsi ya kutumia akili yako kuvunja uraibu wowote ambao umeshajijengea. Kama tulivyoona, huduma za kidijitali zinatumia jinsi ubongo unavyofanya kazi kukuingiza kwenye utumwa.
Hivyo wewe unapaswa kuutumia ubongo wako vizuri kuondoka kwenye utumwa huo.
Saba utajifunza sababu kumi kwa nini unapaswa kuondoka kwenye mitandao yote ya kijamii sasa hivi. Hizi ni sababu ambazo zimechambua jinsi matumizi ya mitandao ya kijamii yalivyo na athari kwenye akili yako, utulivu wako, mahusiano yako, uchumi wako na hata imani yako. Kwa kuzijua sababu hizi kumi, utajionea mwenyewe jinsi ulivyorudi nyuma tangu umeanza kutumia mitandao hiyo na hivyo kuachana nayo ili kuepuka madhara yake.
Mwisho kabisa utajifunza njia za kutumia kufanya maamuzi iwapo utumie huduma ya kidijitali.
Utajifunza jinsi ya kutumia vigezo vitatu vya AFYA, UTAJIRI na HEKIMA katika kuchagua na kutumia teknolojia mpya, ambazo zitakuwa na manufaa kwako badala ya kukufanya mtumwa.
Tuko kwenye vita, adui mkuu anajua yuko vitani ila wanaolengwa hawajui.
Hivyo unapaswa kuwa na maandalizi mazuri ya kupambana na vita hii ili uweze kutoka salama na siyo kuwa mfungwa.
Pata na usome kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI ili upate mbinu za kupambana kwenye vita hii na kutoka ukiwa mshindi. Kitabu hiki kimechapwa kwa nakala ngumu (hardcopy).
Kitabu kinauzwa TSH elfu 20 (20,000/=) na ili kukipata wasiliana na 0752 977 170 na utaletewa au kutumiwa kitabu popote ulipo Tanzania na Afrika Mashariki.
Kwa sababu ya maombi ya watu wengi Leo tunatoa OFA kwa watu ishirini (20) ukinunua LEO kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI, utapata fursa ya kujiunga na chaneli ya SOMA VITABU TANZANIA.
Nb LEO Tarehe 1/5/2021, NDIO MWISHO WA OFA HII.