Jinsi Ya Kuboresha Furaha Na Mahusiano Yako

Rafiki yangu mpendwa,

Hivi unajua kwamba una wajibu na furaha yako kwa 90%?

Vipi kama leo nitakuambia wewe ndiye mkurugenzi wa maisha yako?

Huku ukiendelea kutafakari  tujikumbushe kutoka kwenye hadithi ya kijana aliyemsaidia kipepeo kutoka kwenye buu lake.

Siku moja, kijana mmoja alimpata kipepeo

Ambaye alikuwa anajitahidi kutoka kwenye buu lake.

Akakaa chini na kuanza kumuangalia kwa makini kuona kile kitakachotokea

Baada ya muda kidogo alimuona kipepeo akipambana kutoa kichwa kwa taabu sana.

Ndipo kijana akaamua kumsaidia kipepeo kutoka kwenye buu lake.

Akachukua mkasi na akakata buu lililobakia kidogo.

Kisha kipepeo akatoka kwa urahisi

Ingawa alikuwa na mwili uliozubaa na mabawa madogo yaliyokauka.

 Kijana huyo ingawa hakuwa na kiti , akaketi chini na kusubiri kumuona kipepeo akizinduka na kuanza kuruka

Hata hivyo, hilo halikutokea kabisa.

Kipepeo alitumia maisha yake yote kushindwa kuruka

Akawa anatambaa na mwisho kufa.

Licha ya moyo mwema wa kijana huyo

Hakuelewa kilichotokea mategemeo yake yalikuwa ni kumsaidia aweze kuruka lakini mwisho ilishindikana.

Kumbe hakujua kwa kumsaidia kipepeo kutoka ndiko kulimfanya ashindwe kuruka, kwa kuwa ndivyo sheria ya asili ilivyo.

Sheria ya asili inaeleza kuwa kumnyima kipepeo fursa ya kupambana kutoka kwenye buu lake kutamfanya ashindwe kuruka, kwani mapambano ndiyo yanamsaidia kukua na kuimarisha mabawa yake.

Hadithi hii ya kijana aliyemsaidia kipepeo kutoka kwenye buu lake, inatufundisha kwamba baadhi ya watu wanashindwa kwenye maisha kwa kukosa fursa ya kupambana.

Fursa ya kupambana inatusaidia kuimarika zaidi, jijengee ufahamu kuwa nafasi ya kupambana ni fursa nzuri katika maisha yako na chukua hatua bila kusubiri wengine wakuhurumie na kukusaidia.

Furaha ni wajibu wako hakuna mtu mwingine atakayekupa furaha kuanzia leo jitamkie kwamba una wajibu wa furaha yako.

Ukiwa na utulivu wa akili na mwili utaweza kuwa na furaha na kuboresha MAHUSIANO yako na wale wote unao husiana nao.

Wakati mwingine sisi sote tunahitaji kupumzika kutokana na magumu tunayopitia.

Baada ya siku ndefu kwenye kazi unahitaji kupumzika na kusoma kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI.

Wateja ambao wamesoma kitabu hiki, wanajua namna ya kupata muda wa utulivu mwisho wa siku na wote wanafanya vizuri kwenye hili.

Mapumziko yanakusaidia kupambana mwenyewe na changamoto za kesho unakuwa ni mwenye FURAHA zaidi huku ukiwa umepumzika vizuri.

Kamata nakala yako leo na tenga muda wa kukaa pekee yako.

Wasiliana na  namba 0752977170, kupata nakala yako utaletewa au utatumiwa popote ulipo ndani ya AFRIKA MASHARIKI.

Kupitia kitabu hiki utajifunza mambo saba (7) makubwa ambayo yatakufanya uwe huru na  kuondokana na usumbufu unao kuingiza kwenye utumwa.

Moja utajifunza jinsi ubongo wako unavyofanya kazi na namna teknolojia mpya zinavyotumia ubongo huo kukufanya kuwa mtumwa.

Teknolojia mpya zimetengenezwa kwa namna ambayo zitajenga uteja /uraibu kwenye ubongo wako.

 Kwa kujua njia hiyo utaweza kuepuka kuingia kwenye utumwa wa teknolojia hizo.

Mbili utajifunza kuhusu zama tunazoishi sasa, zama za maarifa na taarifa lakini ambazo zimegeuka kuwa zama za usumbufu.

Utajifunza zama hizi za usumbufu zimetengeneza makundi makubwa mawili, wachache wanaonufaika sana, kama Mark Zuckerberg ambaye ni mmiliki wa Facebook na wengi ambao ni kama watumwa wa wachache hao wanaonufaika.

Ndani ya sura hii utajifunza jinsi ya kufikia viwango vya juu vya ufanisi.

Tatu utajifunza jinsi ya kujua kama tayari umeshanasa na kuwa mtumwa wa teknolojia hizo mpya.

 Unaposoma hapa unaweza kusema wewe hujawa mtumwa, unatumia kwa kupanga mwenyewe, lakini nikuambie kitu kimoja, kwa sehemu kubwa sana umeshakuwa na utaziona dalili kwa kusoma kitabu hiki.

Nne utajifunza jinsi ya kuondoka kwenye utumwa wa kidijitali ambao umeshaingia.

 Baada ya kuona jinsi ambavyo umenasa kwenye utumwa huo, utajifunza njia za kujinasua.

Hapa utajifunza jinsi ya kuizidi ujanja simu janja yako.

Tano utajifunza falsafa mpya ya kuendesha maisha yako kwa uhuru katika zama hizi za usumbufu.

Pamoja na kujifunza kuhusu zama hizo na jinsi ya kuondokana na utumwa wake, usumbufu wake hautaisha, teknolojia mpya zinaendelea kugunduliwa kila siku na zikiwa na ushawishi mkubwa.

Hivyo unahitaji kuwa na falsafa unayoitumia kuchagua huduma za kidijitali utakazochagua kutumia kwa manufaa yako.

Sita utajifunza jinsi ya kutumia akili yako kuvunja uraibu wowote ambao umeshajijengea. Kama tulivyoona, huduma za kidijitali zinatumia jinsi ubongo unavyofanya kazi kukuingiza kwenye utumwa.

 Hivyo wewe unapaswa kuutumia ubongo wako vizuri kuondoka kwenye utumwa huo.

Saba utajifunza sababu kumi kwa nini unapaswa kuondoka kwenye mitandao yote ya kijamii sasa hivi. Hizi ni sababu ambazo zimechambua jinsi matumizi ya mitandao ya kijamii yalivyo na athari kwenye akili yako, utulivu wako, mahusiano yako, uchumi wako na hata imani yako. Kwa kuzijua sababu hizi kumi, utajionea mwenyewe jinsi ulivyorudi nyuma tangu umeanza kutumia mitandao hiyo na hivyo kuachana nayo ili kuepuka madhara yake.

Mwisho kabisa utajifunza njia za kutumia kufanya maamuzi iwapo utumie huduma ya kidijitali.

Utajifunza jinsi ya kutumia vigezo vitatu vya AFYA, UTAJIRI na HEKIMA katika kuchagua na kutumia teknolojia mpya, ambazo zitakuwa na manufaa kwako badala ya kukufanya mtumwa.

Tuko kwenye vita, adui mkuu anajua yuko vitani ila wanaolengwa hawajui.

Hivyo unapaswa kuwa na maandalizi mazuri ya kupambana na vita hii ili uweze kutoka salama na siyo kuwa mfungwa.

Pata na usome kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI ili upate mbinu za kupambana kwenye vita hii na kutoka ukiwa mshindi. Kitabu hiki kimechapwa kwa nakala ngumu (hardcopy).

Kitabu kinauzwa TSH elfu 20 (20,000/=) na ili kukipata wasiliana na 0752 977 170 na utaletewa au kutumiwa kitabu popote ulipo Tanzania na Afrika Mashariki.

MUHIMU; Kama utanunua na kusoma kitabu hiki na ukaona hakina manufaa yoyote kwako, unaruhusiwa kukirudisha na ukarejeshewa fedha zako.

Hivyo chukua hatua sasa, huna cha kupoteza lakini una mengi ya kupata, yatakayokuweka huru kwenye zama tunazoishi sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post