Swali; Je Kama Leo Ingekuwa Siku Yako Ya Mwisho Hapa Duniani, Ungeitumiaje?…

SWALI; Je Kama Leo ingekuwa Siku Yako Ya Mwisho Hapa Duniani, Ungeitumiaje?

Rafiki Yangu Mpambanaji,

Kama kwa uhakika kabisa ni kwamba siku ya leo inapoisha tu, ndiyo mwisho wa maisha yako, je ungeiendeshaje siku yako?

Je ungekubali kupoteza muda wako kuzurura kwenye mitandao ya kijamii na kufuatilia habari za udaku?

Je ungekubali kugombana na watu, kuwa na hasira na chuki kwa sababu ya mambo ambayo watu wengine wanayafanya?

Je ungeahirisha kufanya mambo muhimu kama kuwasiliana na watu wa karibu na kukamilisha kazi muhimu kabisa inayoacha alama yako hapa duniani?

Rafiki, majibu yako ni ya wazi kabisa, kama siku yako ni ya mwisho, hutakuwa tayari kupoteza hata sekunde moja kwa mambo hayo.

Lakini cha kushangaza, hayo ndiyo mambo umekuwa unayaruhusu yapoteze muda wako wa kila siku.

Umekuwa unahangaika na mambo mengi yasiyokuwa na tija kabisa, huku yale yenye tija ukiyaahirisha.

Swali hilo linapaswa kukuamsha kutoka kwenye mazoea yako na kukupa msukumo wa kutumia kila siku yako kwa ukamilifu wake.

 Swali hilo halipaswi kukukatisha tamaa na uone hakuna maana ya kuhangaika na chochote, au ndiyo uone ni bora tu uipoteze siku yako ya mwisho.

 Bali swali hilo linapaswa likupe msukumo wa kufanya kitu kinachokwenda kuacha alama kubwa hapa duniani.

Wote tunajua jinsi ambavyo kifo ni fumbo kubwa kwetu duniani. Hakuna anayejua ni lini atakufa, lakini kila mtu atakufa.

Kuna watu jana walikuwa na mipango mizuri sana ya leo, lakini hawajaiona. Na kuna watu leo wana mipango mizuri sana ya kesho, lakini hawataiona hiyo kesho.

Hivyo kila mmoja wetu ana siku ambayo ni ya mwisho kwake, siku ambayo atakuwa na mipango mizuri ya kesho yake, lakini hiyo kesho hataiona.

 Hakuna anayejua siku hiyo ni ipi, na hapo ndipo unapokuja umuhimu wa kuichukulia kila siku kama siku ya mwisho.

Kwa kila siku unayoipata hapa duniani, ichukulie ndiyo siku yako ya mwisho hapa duniani.

Chukulia ndiyo nafasi ya mwisho uliyoipata ya kufanya mambo yako muhimu.

 Kwa kuchukulia siku hivyo, utaweka umakini kwenye mambo ambayo ni muhimu zaidi na yale yasiyo muhimu hayatapata nafasi.

Hutaahirisha jambo lolote muhimu kwa ajili ya kesho, kwa sababu unajua hiyo kesho haipo. Utaweka vizuri vipaumbele vyako na kuvizingatia katika kuiendesha siku yako.

 Hutaruhusu chuki, hasira au wivu vikutawale, kwa sababu unajua una siku moja pekee.

 Hata watu wanapokukosea, huwezi kuwa na kinyongo nao, zaidi utawaonea huruma, kwa sababu unachukulia hawatakuona tena kwenye maisha yao.

Unaweza kujiambia huku ni kujidanganya, vipi kama nikipata siku nyingine ya kesho?

 Na jibu ni siyo kujidanganya, bali ni kuishi kwa uhalisia ambao umekuwa unaukwepa. Unapopata siku nyingine ya kesho, hiyo ni zawadi na yenyewe pia iishi kama siku ya mwisho kwenye maisha yako.

Kwa kifupi, kuanzia leo, iishi kila siku yako kama ndiyo siku ya mwisho ya maisha yako.

 Na pale unapopata siku nyingine, ichukulie kama zawadi na yenyewe iishi kama siku yako ya mwisho hapa duniani.

Mtazamo huu wa kuziishi siku zako utakuwa na nguvu kubwa sana kwako kuhakikisha unaziishi siku zako zote kwa mafanikio makubwa, ukizingatia yale yaliyo muhimu na kuachana na yasiyokuwa muhimu.

Mwanafalsafa Seneca alikuwa mmoja wa waliofundisha dhana hii kwa msisitizo sana.

Akisema kila siku funga vitabu vya siku hiyo, kamilisha kila muhimu linalopaswa kukamilishwa, kwa sababu ndiyo siku pekee ambayo una uhakika nayo.

Unaweza kupanga mengi kwa siku zijazo, lakini huna uhakika wala udhibiti wa siku hizo zijazo.

Hivyo nguvu zako weka kwenye siku iliyo mbele yako, ambayo ndiyo siku una udhibiti nayo.

Hivyo ndiyo unavyopaswa kuiendea kila siku yako, kwa kuichukulia kama siku yako ya mwisho hapa duniani na hivyo kuzingatia yale yaliyo muhimu tu.

Kutumia vizuri kila sekunde kwa sababu unajua ukishaipoteza huwezi kuipata tena.

Hili halimaanishi usiwe na malengo na mipango ya muda mrefu, kuwa nayo utakavyo, lakini udhibiti wako wote uweke kwenye siku iliyo mbele yako leo,

… kwa sababu ndiyo siku pekee ambayo una uhakika nayo, kama utapata nyingine shukuru na itumie vizuri.

Kuna kauli kwamba mipango siyo matumizi.

 Na kauli nyingine ikisisitiza kwamba mwanadamu hupanga na Mungu hucheka.

 Hizo ni kauli ambazo zinatuonyesha pamoja na kuwa na mipango mikubwa na mizuri, hatuna udhibiti nayo, kwa sababu hatujui nini kitatokea kesho.

Pamoja na kukosa udhibiti kwenye siku zijazo, tusiache kuweka malengo na mipango.

 Lakini tukishaweka malengo hayo na mipango yake, tusihangaike sana na mambo yajayo, badala yake tuhangaike na yale yaliyopo sasa.

 Tusiangalie sana kesho tutafanya nini, bali tuangalie leo tunafanya nini.

Kuna siku itakuwa siku yako ya mwisho, siku ambayo huijui na hivyo unaweza usiwe na maandalizi nayo.

Badala ya kuendelea na maisha ya mazoea, maisha ambayo unayapoteza kwa kujidanganya kuna kesho, anza sasa kuiishi kila siku yako kama ndiyo siku ya mwisho.

Utumie muda wako vizuri ili uweze kufanya makubwa.

Umejionea wazi kwamba mafanikio hayatokei kama ajali au bahati, bali ni mkusanyiko wa siku nyingi ambazo mtu ameziishi kwa mafanikio.

Ni wajibu wako kwenda kuidhibiti kila siku yako, tangu unapoianza asubuhi na mapema mpaka unapoimaliza.

Huhitaji kuangalia siku nyingi zijazo, unachohitaji ni kuiangalia siku yako moja na kuiishi hiyo kwa ukamilifu wake, halafu unarudia hilo kwenye siku nyingine.

Na Kitabu Kipya cha KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO, kitakufundisha kanuni rahisi ya KUIDHIBITI SIKU YAKO, TANGU UNAPOIANZA ASUBUHI NA MAPEMA MPAKA UNAPOIMALIZA.

Na hivyo itakusaidia kuokoa muda wako mwingi unaopoteza kila siku.

Kupata kitabu chako cha KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO Kwa bei ya OFA Ya TSHS 14,999Tu!

Tuma meseji yenye maneno “ SIKU YA MAFANIKIO” Kwenye WHATSAPP NAMBA 0752977170.

Kisha utapata utaratibu wa kuletewa au kutumiwa kitabu chako.

KUMBUKA; OFA Hii Inaisha Tarehe 7|6|2022.

Kila Lakheri,

Kutoka Kwa SHABIKI YAKO NAMBA 1,

AmryRamadhani|CopywriterOfSomaVitabuTanzania|

Karibu. www.t.me/somavitabutanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post