98% Utatoa Maana Gani Ya Kile Kitakachokutokea LEO Hii.?…

98% Utatoa Maana Gani Ya Kile Kitakachokutokea Leo Hii?…

Rafiki Yangu,

Maana Yako Itajulisha Utashinda au Utashindwa.

Utafanikiwa au Utashindwa.

Na ndani ya makala hii utajifunza somo la maisha ambalo hutosahau…

Mwaka 2005 kulikuwa na Mapacha mawili na Baba yao mlevi huko Manyoni – Singida, waitwao Shafih na Saleh.

Kumbuka Ndugu hawa wawili (2) ni Mapacha wasiofanana na Baba Yao hakuwa tu mlevi bali alikuwa mlevi mwenye hasira na mkali kupita maelezo yani mkali sana.

Baba huyu alikuwa mfano mbaya wakuigwa kwa watoto wake.

Mapacha hawa wawili (2) walishuhudia mambo yote mabaya ambayo baba yao aliyokuwa akiyafanya, kwa kuona kwa macho yao na kusikia kwa masikio yao.

 Walimtazama baba yao katika utoto wao wote, miaka yao ya ujana… na hadi pale walipohama  nyumbani na kwenda kujitegemea.

Kwa bahati mbaya baba yao hakuwahi kubadilika.

Unywaji wa pombe kupita kiasi haukukoma… uchungu ukaongezeka… hasira juu ya ulimwengu iliongezeka na kulaumu matatizo yake yote duniani hayakukoma.

Miaka 15 baadaye  … Mapacha sasa ni watu wazima… watu wazima wenye umri wa miaka 30.

Kutokana na ukorofi, baba yao alishtakiwa kwa kosa la kufanya uhalifu wa kutumia nguvu.

Na si mara ya kwanza anafanya kosa hilo…

Saleh ambaye ni mmoja wa wale mapacha naye amefungwa kwa kosa la kuvunja sheria za nchi..

Mama wa Mapacha anaenda kumtembelea mwanae (Saleh)  gerezani … na anamuuliza mwanae …

“Uliishiaje hivi?”

Saleh akiwa amekasirishwa na swali aliloulizwa na mama yake, anajibu kwa hasira:

“Baba yangu alikuwa mlevi … nilikuwa na chaguo gani!!!?”

Alimlaumu baba yake kwa jinsi maisha yake yalivyokuwa.

Baada ya yote, alikuwa mfano wa tabia kama hiyo.

Baada ya kumuona mwanae Saleh na kuridhika.

Anaelekea kumtembelea pacha mwingine ambaye ni Shaffih…

 Maisha ya pacha huyu yalibadilika kidogo.

Hajawahi kutumia kilevi cha aina yoyote katika maisha yake, ana ndoa yenye furaha, na watoto 2 wazuri na anaishi maisha yenye furaha sana, yenye mafanikio.

Mama anamuuliza Shaffih: “Uliishiaje hivi?”

Shaffih Anajibu: “Baba yangu alikuwa mlevi aliye na hasira sana … nilikuwa na chaguo gani?”

“Sikutaka maisha hayo kwangu… ‘Hilo halitatokea kwangu kamwe!’ Haijalishi nini – nitaishi kinyume na tabia za baba alizoziishi maisha yake yote hapa duniani”

SOMO;

Haijalishi ni nini kinakututokea-

Muhimu tu ni MAANA gani unatoa kwa kile kinachokutokea –

98% Maana utakayoitoa itajulisha ushinde au ushindwe. Ufanikiwe au ufeli.

Jifunze kuona wema wa wengine na wema katika hali ZOTE…

Na hivyo itakusaidia kutorudia makosa ambayo uliyafanya hapo nyuma na yaliyofanywa na wengine.

Ukiweza kulifanya hili kila siku, hakika utaweza kuboresha maisha yako na utakuwa mtu wa thamani sana.

Na Habari Njema Ni Kwamba Leo Unaweza Kuboresha Maisha Yako na Kuongeza Thamani Yako,

Kwa Kusoma Vitabu Vifuatavyo;

1.  KITABU; ELIMU YA MSINGI YA FEDHA.

2.  KITABU; ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA.

3.  KITABU; UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA.

4.  KITABU; EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI.

5.  KITABU; MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO.

6.  KITABU; TABIA ZA KITAJIRI.

7.  KITABU; KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO.

KWA SABABU Ya Maombi Ya Wengi LEO Ukichagua Vitabu Vitatu (3) Kati Ya 7 Hapo Juu.

Utavipata Kwa OFA YA TSHS 49,999TU! Badala Ya Tshs 60,000.

Tuwasiliane Kwa Namba 0752977170.

Namba Ni 0752977170.

KUMBUKA; OFA Hii Ni Kwa Wale Watakaochukua Kuanzia Vitabu Vitatu (3) Na Sio Chini Ya Hapo,

OFA HII; Ni Ya LEO TU!

Kila Lakheri,

Nakupenda.

Kutoka Kwa AmryRamadhani|CopywriterOfSomaVitabuTanzania|

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post