Mitazamo Mi 5 Ambayo Itakufanya Uendelee Kuwa Na Maisha Magumu Licha Ya Kupambana Sana…


Mitazamo Mitano (5) Ambayo Inakufanya Uendelee Kuwa Na Maisha Magumu Sana…

Rafiki Yangu Mpambanaji,

Hata kama sasa una maisha magumu sana, umeshajaribu kila njia kujikwamua kiuchumi na umefeli…basi hiki unachoenda kukiona ndani ya sekunde 11 zijazo kitabadilisha kila kitu katika maisha yako.

Je ni upi mtazamo sahihi wa kukuwezesha kuongeza kipato chako?

Ni kipi ambacho ukikifanyia kazi kweli, kitakuhakikishia kuwa na kipato kikubwa wakati wowote?

Na jibu ni kwamba,

Kipo kitu ambacho ukikisimamia hicho, kikawa ndiyo mwongozo wako kwenye kazi zako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla, utashangaa namna ambavyo kipato chako kinaongezeka bila hata ya kusumbuka sana.

Mtaalam Jim Rhon ambaye alinukuu hili vizuri sana, akisema;

You don’t get paid for the hour. You get paid for the value you bring to the hour.

Akimaanisha kwamba, hulipwi kwa saa unayofanya kazi, bali unalipwa kwa thamani unayotengeneza kwenye saa unayofanya kazi.

Na mimi naweza kusema kwa kujiamini kabisa ya kwamba ukiweza kuishi kauli hii moja tu kila siku, utajiweka vizuri sana kwa upande wa kipato.

 Kauli hiyo ni kwamba, unalipwa kwa thamani unayozalisha, thamani unayoitoa kwa wengine.

 Jiambie kauli hii kila unapoamka asubuhi, jiambie kauli hii kila unapoanza kazi au biashara yako, jiambie kauli hii kila unapofikiria kuhusu fedha.

 Jiambie kwa sauti; nalipwa kulingana na thamani ninayozalisha, je nizalishe thamani gani sasa ili nilipwe zaidi?

Ukiweza kuiishi kauli hii kila siku, ukaweza kuifanyia kazi, iwe umeajiriwa, umejiajiri au unafanya biashara, una uhakika wa kuongeza kipato chako, kadiri utakavyo.

Kwa sababu kitu pekee unachohitaji kufanya, ni kuzalisha thamani zaidi kwa wengine.

Na kwa dunia hii ambayo kila mtu ana kitu cha kulalamika kwenye kila kitu, zipo fursa nyingi sana za wewe kuongeza kipato chako kwa kutoa thamani zaidi.

Angalia sasa,

Kama bado unaiishi hii mitazamo utachelewa sana kufanikiwa…

1; Kama bado una amini unalipwa kulingana na elimu uliyonayo.

Mtazamo ambao umewaingiza wengi sana kwenye matatizo ya kifedha ni kuamini kwamba malipo yao kwenye ajira zao na hata biashara ambazo wanafanya, yanategemea elimu waliyonayo. Kwa mtazamo huu, watu wamekuwa wanakazana kusoma na kuongeza elimu, lakini mwisho wa siku wanajikuta kwenye matatizo zaidi kifedha.

Tena kwa elimu za kutegemea mikopo au ufadhili, yeyote anayeongeza elimu kwa lengo tu la kuongeza kipato, anatengeneza matatizo makubwa sana kwenye maisha yake, hasa kifedha.

Sisemi elimu siyo muhimu, ila ninachosema unapotumia elimu kama njia ya kuongeza kipato na kuondokana na changamoto zako za kifedha, umeshapoteza njia.

2; Kama bado una amini unalipwa kulingana na muda unaofanya kazi.

Moja ya vitu ambavyo mfumo rasmi wa ajira umewajengea watu kuhusu ufanyaji wa kazi ni kwamba, muda ndiyo kipimo muhimu. Hivyo kama utafanya kazi masaa mengi zaidi, basi kipato chako kitakuwa kikubwa zaidi. Na hili lina ukweli, lakini kwa kiasi kidogo sana, kwa sababu, kuna masaa 24 pekee kwa siku. Hivyo hata kama utafanya kazi usiku na mchana, bado huwezi kutengeneza muda zaidi. Hivyo kwa vyovyote vile, bado utakuwa na ukomo wa kipato, kwa sababu ya ukomo wa muda.

Kadhalika hapa sisemi kwamba usifanye kazi kwa muda mrefu, lakini dhana kwamba muda pekee utakutoa kwenye changamoto za kifedha ni jambo la ajabu, na kujitengenezea matatizo zaidi.

3; Kama bado una amini unalipwa kulingana na uzoefu wako.

Kwamba utaanza kazi na mshahara kidogo, halafu kadiri unavyoendelea kukaa kwenye kazi hiyo, mshahara wako unaendelea kupanda.

 Hivyo kama utafanya kazi miaka 20 au 30 basi mshahara wako utapanda sana.

 Hapa kuna ukweli kiasi, lakini uongo ni mkubwa zaidi.

Je ni kweli kwamba kipato kinaongezeka sawasawa kulingana na miaka ambayo mtu amefanya kazi?

Au kipato kinaongezeka kufidia mfumuko wa bei ambao huwa unatokea kila mwaka?

Kutegemea uzoefu pekee kama kigezo cha kuongezeka kwa kipato ni dhana potofu.

Kwa sababu licha ya uzoefu wa muda mrefu, bado sehemu ya kipato inayoongezeka ni ndogo sana, huku ukizingatia kadiri muda unavyokwenda gharama za maisha ya mtu zinazidi kuwa kubwa zaidi.

 Kama alianza kazi akiwa mwenyewe, kadiri anavyokwenda anakuwa na familia sasa.

Changamoto nyingine kubwa kuhusu uzoefu ni kwamba, wengi hawana uzoefu wanaosema wanao.

Wengi wanaokuambia nina uzoefu wa miaka kumi, wanachomaanisha ni kwamba, wana uzoefu wa mwaka mmoja, uliojirudia mara kumi. Kwa sababu wanakuwa wanafanya mambo kwa mazoea na hakuna wanachobadili.

4; Kama bado una amini unalipwa kulingana na unavyoonekana unafanya kazi.

Maajabu huwa hayaishi duniani, na binadamu sisi ni viumbe wazuri sana kwenye maigizo.

Watu wengi sana wamekuwa wanaigiza kazi ili kuonekana ni wachapa kazi wakiamini hilo litaongeza kipato chao.

Hapa ndipo unapokuta watu wakiahidi vitu ambavyo hawawezi kutekeleza, wakikazana kufanya mambo yanayoonekana kwa nje, lakini kwa ndani hayana maana yoyote.

Kwenye baadhi ya maeneo hili linafanya kazi kiasi, hasa kwenye siasa na taasisi za umma, lakini lina ukomo mkubwa sana wa kipato.

 Kwa sababu unakuwa unategemea zaidi neema ya mtu mwingine kukuona unakazana ndiyo akuongezee malipo. Mpango ambao siyo mzuri kabisa.

5; Kama bado una amini unalipwa kwa sababu unastahili.         

Yaani kila ninapokuwa nawasikiliza watu wakilalamika kuhusu malipo madogo wanayopokea, huwa nashangaa kwa nini watu hawaoni zama zimeshabadilika sana.

 Zile zama za vyama vya wafanyakazi kuendesha migomo kushinikiza waajiri kuongeza malipo, kwa sababu watu wanastahili  kulipwa zaidi zimeshapita.

Hakuna tena anayeweza kudai kulipwa zaidi kwa sababu anastahili kulipwa, kwa sababu hakuna tena hata ambao wanaajiri.

Hivyo kufikiria kwamba una haki ya kulipwa kwa sababu unastahili, unajidanganya.

Kwa wingi wa watu wanaohitaji kazi, na uchache wa nafasi za kazi, hustahili chochote kutoka kwa anayekuajiri au kukulipa.

Bali yeye ndiye anayestahili kitu kutoka kwako.

Kwenye dhana hizo tano, nina imani umeona wapi umekuwa unakwama, wapi ambapo umewekeza nguvu kubwa lakini matokeo huyaoni.

Na Habari Njema Ni Kwamba Leo Unaweza Kuongeza Thamani Yako,

Kwa Kusoma Vitabu Vifuatavyo;

  1. KITABU; ELIMU YA MSINGI YA FEDHA.
  2. KITABU; ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA.
  3. KITABU; UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA.
  4. KITABU; EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI.
  5. KITABU; MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO.
  6. KITABU; TABIA ZA KITAJIRI.
  7. KITABU; KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO.

KWA SABABU Ya Maombi Ya Wengi LEO Vitabu Vitatu (3) Hapo Juu.

Utavipata Kwa OFA YA TSHS 44,999TU! Badala Ya Tshs 60,000.

Tuwasiliane Kwa Namba 0752977170.

Namba Ni 0752977170.

KUMBUKA; OFA Hii Ni Kwa Wale Watakaochukua Kuanzia Vitabu Vitatu (3) Na Sio Chini Ya Hapo,

OFA HII; Ni Ya LEO TU!

Kila Lakheri,

Nakupenda.

Kutoka Kwa AmryRamadhani|CopywriterOfSomaVitabuTanzania|

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post