Ongeza Thamani Yako Ulipwe Zaidi Kwa Kufanya Jambo Hili Kila Siku.

Wahenga waliwahi kusema “ELIMU HAINA MWISHO”.

Wapo sahihi kabisa kwa sababu,

Ili upate mafanikio makubwa, lazima uchague kuwa mwanafunzi maisha yako yote.

Ujifunze kuhusu maisha na mafanikio kwa ujumla.

Ujifunze kuhusu fedha na uwekezaji.

Ujifunze kuhusu biashara na uchumi.

Ujifunze kwa kina kuhusu kile unachofanya.

Kwa kuwa maarifa yanaongezeka kila siku, huwezi kufika mahali na kusema umeshajua kila kitu, hivyo kujifunza ni endelevu mpaka siku unaondoka hapa duniani.

Kauli ya kujitamkia kila siku” Nitajifunza kila siku bila kukoma ili niweze kukua zaidi  kimafanikio na kiutajiri.”

Matajiri huwa wanajifunza kila siku na kuendelea kukua.

Hakuna wakati wanajiona wameshajua kila kitu, wanajua kuna mengi hawajui na hivyo kuwa wanyenyekevu na kujifunza.

Masikini huwa hawajifunzi kila siku, wakishahitimu masomo wanaamini tayari wanajua kila kitu.

Kwa njia hiyo hawakui kwa sababu kuna mengi hawajui ambayo yanakuwa kikwazo kwao.

Matokeo unayoyapata sasa yanatokana na kile unachojua sasa.

Kama unataka kupata matokeo ya tofauti, lazima ujifunze vitu vya tofauti.

Kwa kuwa masikini hawajifunzi vitu vya tofauti , wanaendelea kupata matokeo yale yale.

Kwa kuwa matajiri wanajifunza vitu vya tofauti, wanapata matokeo ya tofauti.

Kama bado hujafika pale unapotaka kufika, jua kuna kitu bado hujajifunza.

Kama hutajifunza kitu hicho hutaweza kufika unakotaka kufika.

Kitu muhimu unachopaswa kujua ni kwamba hakuna mtu aliyezaliwa akiwa anajua chochote.

Wote tulizaliwa tukiwa tunajua kulia na kunyonya tu.

Mengine yote tumefundishwa au kujifunza hapa duniani.

Hivyo unapoona wenzako wana vitu ambavyo wewe huna, jua hawakuzaliwa navyo, bali walijifunza.

Hivyo hata wewe unaweza kujifunza na ukawa na vitu hivyo.

Kama wengine wanaweza kuwa matajiri na wewe pia unaweza kuwa tajiri, unachopaswa ni kujifunza kile wanachojua ambacho wewe hujui , chukua hatua wanazochukua ambazo wewe huchukui na utayapata matokeo kama yao.

Matajiri wanajua kwamba wanapaswa kwanza kuwa na mtazamo wa kitajiri, kasha kuchukua hatua za kitajiri na hatimaye wapate utajiri.

Masikini wanategemea wapate kwanza utajiri, ndiyo wachukue hatua za kitajiri na hapo wawe matajiri.

Unaweza kuona hapo kwa nini matajiri wanajifunza sana na kuwa matajiri, huku masikini wakiwa hawajifunzi na hivyo hawawi matajiri.

Matajiri pia wamebobea sana kwenye kile wanachofanya, wanakijua kwa viwango vya juu kuliko wengine wote.

Lakini masikini hawajabobea kwenye wanachofanya , huwa wanafanya tu kwa mazoea.

Kama unataka kuongeza thamani yako leo jifunze hapa   (http://bit.ly/somavitabuapp).

Utajifunza njia na hatua za kuchukua ili uongeze thamani zaidi.

Utajiri ni mchezo,

Mchezo ambao una kanuni zake na sheria zake,

Na ili uweze kushinda mchezo huu,

 Lazima uzijue kanuni na uzishike sheria.

Haiwezekani kabisa kwa mtu ambaye hajui kanuni za mpira wa miguu,

Hana mazoezi akaenda uwanjani na kushinda.

Wengi wamekuwa wanaingia kwenye mchezo wa utajiri kama vile ni kitu cha kubahatisha,

Hawajui kanuni wala sheria,

Hawana maandalizi na kinachotokea ni kushindwa vibaya sana.

Karibu sana usome EBOOK mpya inayoitwa TABIA ZA KITAJIRI,

Ujifunze kwa kina na kuyaelewa maarifa haya muhimu sana kwako,

 Kisha uchukue hatua ili maisha yako yaweze kubadilika, ufike kwenye utajiri, mafanikio na furaha.

JINSI YA KUTUMIA EBOOK YAKO.

EBOOK mpya inayoitwa TABIA ZA KITAJIRI inapatikana kwenye app ya SOMA VITABU ambayo inapatikana kwenye mfumo wa ANDROID (PLAY STORE).

Kupata app hiyo fungua kiungo hiki; http://bit.ly/somavitabuapp au nenda moja kwa moja kwenye playstore kisha tafuta SOMA VITABU.

Ukishaweka app kwenye kifaa chako (simu au tablet) utakiona kitabu na kufuata mchakato wa kukinunua moja kwa moja kwenye app.

Kupata maelezo zaidi ya jinsi ya kutumia app, kununua na kusoma vitabu, fungua hapa; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/somavitabuapp .

Au Piga Simu Namba 0752977170, Kwa Msaada Zaidi.

ZAWADI YA EBOOK.

Rafiki yangu mpendwa,

Kwa kuwa umekuwa unafuatilia mafunzo ninayotoa kwa muda mrefu,

Nakwenda kukupa EBOOK hii ya TABIA ZA KITAJIRI KAMA ZAWADI.

Hivyo kwa siku hizi chache utaipata EBOOK hii kwa TSH elfu moja(1)  pekee (1,000/=).

EBOOK hii ina thamani ya mamilioni kwako, ila wewe unaenda kuipata sawa na bure kabisa, kwa TSH elfu moja tu.

Lengo langu ni wewe usiwe na sababu yoyote ya kuikosa,

 Kwa sababu nataka sana uyabadili na kuyaboresha maisha yako na maarifa yaliyo kwenye kitabu hiki ndiyo unayahitaji sana.

Chukua hatua sasa rafiki yangu,

Zawadi hii ni ya muda mfupi,

Bei ya EBOOK hii itakuwa kubwa zaidi baadaye hivyo usikubali kukosa.

Utajiri ni haki na wajibu wako, kama wapo wengine walioweza kufikia utajiri, na wewe pia unaweza kuufikia.

Unachohitaji ni kuijua kanuni sahihi na kuifuata.

EBOOK hii ya TABIA ZA KITAJIRI ina kanuni hizo, wajibu wako ni kuzijua na kuzifuata na utajiri kwako unakuwa swala la muda tu.

Jipatie kitabu chako sasa kwa bei ya zawadi, fungua; http://bit.ly/somavitabuapp

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post