KITABU KIPYA; MJASIRIAMALI MJANJA.

KITABU KIPYA; MJASIRIAMALI MJANJA.

Kitakufundisha Jinsi Ya Kuanzia Popote Ulipo Na Kupata Kila Unachotaka Kwenye Maisha Yako.

Rafiki Yangu Mkubwa,

Vp Hali Yako?

Mda mchache ujao utasoma kitu kipya ambacho kitakupa tumaini la kuendelea mbele hata kama unahisi uchovu wa akili na mwili.

Ilivyo ni kwamba…

 Wajasiriamali ni watu wanaoleta miujiza mikubwa hapa duniani.

 Ni watu wanaoanza na wazo la kitu ambacho hakipo, kisha kulileta wazo hilo kwenye uhalisia na kuwa na manufaa makubwa kwa wengine.

Ni kupitia ujasiriamali ndiyo tumeweza kupata uvumbuzi ambao umeyafanya maisha yetu kuwa bora kabisa hapa duniani.

Ukiangalia kila kinachokuzunguka sasa hapo ulipo, hakikuwepo miaka mingi iliyopita.

Kilianza na wazo kwa mtu, kisha akalifanyia kazi wazo hilo.

Chukua mfano wa simu ya mkononi, ambayo kila mtu anaitumia sasa.

 mwaka 1900 simu hizi hazikuwepo kabisa, lakini miaka 100 baadaye, yaani mwaka 200, simu hizi zikawepo kwa wingi na kwa sasa ni kama sehemu ya maisha ya kila mtu.

 Simu hizi zilianza kama wazo kwa mtu, akalifanyia kazi na hatimaye kuja na kitu ambacho kimekuwa na manufaa kwa wengi.

Ujasiriamali pia ndiyo njia ya uhakika ya mtu kupata chochote anachotaka kwenye maisha yake.

 Kuanzia kupata utajiri mkubwa, uhuru kamili wa kifedha na muda na hata kuwa na ushawishi mkubwa kwa wengine, yote hayo yanawezekana kupitia ujasiriamali.

Ukiangalia orodha ya matajiri wakubwa duniani, wengi ni wajasiriamali.

Ukiangalia makampuni yenye nguvu na ushawishi mkubwa duniani, yote ni ya kijasiriamali, tena ambayo yalianza kidogo na kukua kwa muda mrefu.

Lengo kuu la kitabu hiki ni kukushauri wewe ambaye unafikiria kuingia kwenye ujasiriamali au ambaye tayari upo kwenye ujasiriamali uweze kuufanya kwa mafanikio makubwa.

Uweze kuamini kwenye ndoto kubwa ulizonazo hata kama wengine hawaziamini.

Lakini la muhimu zaidi, uweze kujenga biashara sahihi itakayowezesha wazo lako kubwa kutimia.

 Kwa sababu wajasiriamali wengi wamekuwa wana mawazo makubwa na mazuri, lakini wanashindwa kuyatekeleza kwa kushindwa kujenga biashara sahihi.

Kwenye kitabu hiki, maneno ujasiriamali na biashara yametumika kwa kuchanganya lakini kwa vyovyote unavyosoma, kuwa na uelewa huu.

 Ujasiriamali ni kile ambacho mtu ANAKUWA na biashara ni kile ambacho mtu ANAFANYA.

 Kwa maneno mengine, biashara ndiyo njia ya kutekeleza ujasiriamali.

Tukirudi kwenye mfano wa simu tulioanza nao hapo juu, kuwa na wazo la watu kuweza kuwasiliana wakiwa mbali kwa kifaa ambacho mtu anatembea nacho kila mahali ni ujasiriamali.

 Kuzalisha, kusambaza na kuuza simu hizo kunahitaji biashara inayojiendesha kwenye msingi sahihi.

Hivyo tofauti kubwa ya kitabu hiki na vitabu vingine vya ujasiriamali ni hakikuonyeshi tu upande wa wazo,

…bali pia kinakuonyesha upande wa kulileta wazo hilo kwenye ujasiriamali.

Mafunzo mengi ya ujasiriamali huwa yanawapa watu ujuzi wa kuwa wabunifu na kuzalisha vitu.

 Watu hao wanazalisha vitu kweli, lakini wanakwama kwa kushindwa kufikia soko na kuuza vile walivyozalisha.

Kitabu hiki kinakuonyesha jinsi ya kujenga biashara ambayo itatimiza wazo lako la ujasiriamali.

Utajifunza jinsi ya kulifikia soko na kuwashawishi watu kununua.

Kilicho muhimu kabisa ambacho pia utajifunza kupitia kitabu hiki ni kuweza kuambatanisha maisha na ujasiriamali.

Watu wengi wamekuwa wanakwama kwenye biashara na ujasiriamali kwa sababu wanakuwa wametenganisha na maisha yao.

Kwenye kitabu hiki utajifunza jinsi ya kuvileta hivyo pamoja, yaani maisha na ujasiriamali.

Kupitia kulijua kusudi laki na kuliishi, unakuwa na maisha kamilifu na yenye mafanikio makubwa.

Karibu sana usome kitabu hiki cha MJASIRIAMALI MJANJA,

…ambacho kitakuwezesha wewe kuwa mjasiriamali mjanja na kuweza kupata kila unachotaka kwenye maisha yako.

Tayari una uwezo mkubwa sana ndani yako,

Kilicho baki ni wewe kusoma kitabu hiki ili uweze kuutumia kufanya makubwa zaidi.

Na habari njema ni kwamba badala ya Tshs 30,000 leo unakipata kwa Tshs 19,999Tu!

Tuwasiliane kwa namba 0752977170.

Kupata kitabu hiki cha MJASIRIAMALI MJANJA.

KUMBUKA; 19 Wa Kwanza Wanaunganishwa Kwenye Group Maalum.

Na kina pages 252.

Karibu Sana,

Shabiki Yako #1,

Bwana AmiriRamadhani|CopywriterOfSomaVitabuTanzania|

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post