MPYA: Hatua 3 Na Rahisi Za Kuanzisha Biashara Bila Mtaji…!
Kati ya maswali niliyowahi kukutana nayo sana. Watu wengi wakiniuliza wanasema nitaanzaje biashara? Nawezaje kuanza biashara yangu.
Leo nilitaka nikuambie kuna hatua tatu rahisi sana za kuanzisha biashara yako.
Hatua Ya Kwanza: Tunasema gundua eneo lako linalogusa moyo wako, kitu unachokipenda kukifanya ni eneo gani la maisha unapenda zaidi kufanya kwa sababu mafanikio yote huwa yanakuja baada ya kugundua ni kitu gani Fulani maalumu unachotaka kukifanya.
Hatua Ya Pili: Tunasema Pata WAZO, katika hilo eneo , wewe unaweza kusema eneo lako unalolipenda ni kilimo, eneo lako unalolipenda ni kuuza nguo au eneo lako unalolipenda ni kucheza mpira.
Hapo sasa unapata wazo, tafuta wazo na mawazo yanapatikana katika njia mbalimbali wazo la biashara unaweza kulipata kwa ajili ya uhitaji,
Unaweza kuangalia ni kitu gani kinahitajika katika mazingira husika unapata wazo kwa sababu kumbuka siku zote wazo la biashara maana yake ni kwamba ni kitu ambacho watu wanachokithamini na wako tayari kukilipia pesa ili wakipate lakini namna nyingine ya kupata wazo ni unaweza ukaangalia wengine wanafanya nini mahali pengine wanafanya nini na wewe ukalileta lile wazo katika mazingira yako na ukaliweka lifanane na mazingira yako na likafanya kazi tu, kama kawaida.
Kwahiyo unaweza ukapata wazo katika eneo lako ukishagundua eneo lako unalolipenda.
Hatua Ya Pili, Tafuta wazo na je, hatua ya tatu tunafanyaje?
Hatua Ya Tatu: Ni rahisi sana, hatua ya tatu tunasema “ Anza Na Ulichonacho”.
Moja ya changamoto moja kubwa sana watu wengi wanakuwa nayo.
Wanataka kuanza na mtaji mkubwa, wanataka kuanza na ofisi kubwa .
Hapana kanuni ya mafanikio inasema katika biashara anza na ulichonacho pale ulipo na vile ulivyo swali siyo sina kitu Fulani hapana swali ni kwamba una nini?
Swali langu katika point ya tatu inasema una nini mkononi mwako?.
Kile ulichonacho ndicho kinaweza kutumika kama MTAJI nambari moja na kuna aina mbalimbali za mitaji ambazo utajifunza ndani ya kitabu kinachoitwa ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA.
Leo itoshe kusema unakitu ambacho ukiamua kukitumia kitakufikisha mbali sana.
Inaweza ikawa ni maarifa au ujuzi anza na hatua hizi tatu au inawezekana ni kitu Fulani kidogo tu, lakini anza na kidogo ulichonacho katika hatua hizi tatu zinaweza kukusaidia kuanzisha biashara yako kwa haraka sana na ukafanikiwa.
LEO HII! Mtu Yeyote Anaweza Kuanzisha Na Ukafanikiwa Kwenye Biashara Ya Aina Yoyote Unayotaka Kufanya au Unayofanya, Kwa Kusoma Kitabu Kinachoitwa ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA, Kwa Sababu Baada Ya Kumaliza Kusoma Kitabu Hiki Utakuwa Na Uwezo Wa Kujua Aina 5 Za Mitaji Ambazo Utaweza Kuzitumia Vizuri Ili Kuleta Mabadiliko Makubwa Kwenye Biashara Yako.
Kukipata Kitabu Cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA, Tuma Ujumbe Unaosomeka “ BIASHARA”.
Kwenda Namba 0752977170, Utaletewa au Utatumiwa Kitabu Chako Popote Ulipo Ndani Ya AFRIKA MASHARIKI.