ANGALIA; Tofauti Yako na Matajiri Kwenye Fikra Za Kitajiri…

ANGALIA;Tofauti Yako Na Matajiri  Kwenye Fikra Za Kitajiri…

Rafiki Yangu Mpambanaji,

Watu waliofanikiwa ni watu chanya, wenye hamasa, nguvu na furaha kwenye maisha yao.

 Ni watu ambao wanajisikia kuwa na nguvu, udhibiti na kujiamini.

Na hili halitokei kwa bahati mbaya, bali ni matokeo ya FIKRA ZA KITAJIRI.

 Watu hawa wanapojiongelesha au kufikiri, wanatumia maneno chanya, ya kuwainua na kuwapa moyo.

Wanajipongeza kwa hatua mbalimbali walizopiga badala ya kujikosoa kila wakati.

 Wanatumia kauli chanya kila siku kutengeneza fikra na mtazamo chanya kwenye maisha yao.

Hawakati tamaa pale wanapokutana na changamoto, bali wanajua kila changamoto inakuja na fursa ndani yake.

Watu waliofanikiwa wanadhibiti fikra na hisia zao.

Fikra hasi zinapoingia kwenye akili zao zinaondolewa haraka kwa fikra chanya.

Wanajua kwamba fikra hasi ikiachwa kwa muda mfupi inakaribisha fikra hasi nyingine na ndani ya muda mfupi wanakuwa wameshabadilika na kuwa hasi.

Hivyo hawabembelezi kabisa fikra yoyote hasi inayowaingia, inang’olewa hapo hapo kabla haijaota mizizi.

Watu hawa wanalisha akili zao mawazo mazuri na chanya na wanaruhusu haya yajenge mizizi kwenye akili zao na kuzaa matunda ya matendo chanya yanayoleta mafanikio.

Watu waliofanikiwa kila siku wanafikiri fikra za kitajiri.

Wanatumia kauli chanya na kujienga taswira chanya za kile wanachotaka na kule wanakotaka kufika.

 Watu hawa wanadhibiti sana kila taarifa wanayoruhusu kuingia kwenye akili zao, hasa kutoka kwa wengine na kwenye vyombo vya habari.

Wanachagua kupata taarifa na maarifa chanya na kuepuka kupata taarifa na maarifa hasi. Wanadhibiti ni habari zipi wanafuatilia na mitandao ipi wanayotembelea.

Wanajua habari nyingi ni hasi na mitandao mingi imejazwa taarifa hasi.

 Watu hawa wanachukua juhudi za makusudi kuzuia maarifa na taarifa hasi zilizojaa kila eneo kuingia kwenye akili zao.

Wanatumia muda wao kusoma na kufuatilia taarifa na maarifa chanya yanayowainua na kuwapa hamasa ya kuchukua hatua zaidi.

Pia watu waliofanikiwa ni watu wa shukrani kwa kila wanachokutana nacho kwenye maisha.

Kila siku wanatoa shukrani kwa maisha waliyonayo, wanafanya hivi kabla ya kulala au pale wanapoamka.

Watu hawa huwa wanakuwa na orodha ya vitu wanavyoshukuru kwa kuwa navyo kwenye maisha.

 Kwa kuwa watu wa shukrani, wanafikiria zaidi kile walichonacho na siyo walichokosa.

Kwa kuwa watu wa shukrani, hawapati kabisa muda wa kulalamika, na hilo linawaondoa kabisa kwenye hali hasi.

Kwa upande wa pili, watu ambao hawajafanikiwa ni watu wa kujikosoa muda wote.

Muda wote wanakuwa na fikra hasi na za kubomoa.

Wanaruhusu fikra mbaya na hasi kuingia kwenye akili zao na kuweka mizizi kitu ambacho kinatengeneza tabia hasi na mbaya ambazo zinawazuia kufanikiwa.

Kwa kuwa na fikra hasi, wanakosa hamasa na msukumo wa kuchukua hatua zaidi ili kufanikiwa.

Mara nyingi huwa wanajikuta kwenye hali ya kukata tamaa na hata kupata sonona ambayo inawazuia kuchukua hatua zaidi.

Watu wasiofanikiwa ni wafuatiliaji wazuri wa taarifa na maarifa hasi.

Wanaruhusu kila aina ya habari iingie kwenye akili zao,

…wanafuatilia kila taarifa ya habari, kusoma magazeti yaliyopambwa kwa vichwa vya habari hasi na muda wao mwingi wanautumia kwenye mitandao iliyojaa habari hasi.

Kwa kufuatilia kwao habari hasi, kila wakati wanajikuta kwenye hali ya kukata tamaa,

…na kujiona hawana nguvu wala uwezo wa kufanya chochote na maisha yao.

Bila ya kutengeneza tabia ya kuwa na fikra za kitajiri, na kuilazimisha akili yako kila siku kutawaliwa na fikra hizi za kitajiri,

…kupiga hatua kutakuwa kugumu sana kwenye maisha yako.

Kwa sababu akili zetu zina nguvu sana, na nguvu hiyo isipotumiwa vizuri inakuwa kikwazo kikubwa kwako.

Utajisikiaje kama mwaka ujao tarehe kama ya leo huna madeni,huwazi kesho utakula nini,

…una pesa zakutosha za kuendesha maisha yako zaidi ya miezi 6,pesa zinakufanyia kazi, unapata kila unachotaka kwa wakati, usiku unalala kwa amani kama mtoto mchanga,

…unayafurahia maisha pamoja na familia yako?…

Kama unataka iwe hivyo,

Karibu usome kitabu kipya kinachoitwa TABIA ZA KITAJIRI, ili utoke kwenye umasikini wa kutupwa.

Kama unacho nakusii sana, urudie kukisoma na uanze kufanyia kazi yale yote uliyojifunza.

JINSI YA KUPATA KITABU CHAKO;

  1. Tuma Meseji Yenye Neno “UTAJIRI” .
  2. Kwenye WhatsAPP Namba 0752977170.
  3. Kuweka Oda Yako.
  4. Kisha Utatuma Majina Yako, na Mkoa Uliopo.
  5. Kama upo Ndani Ya Mkoa Wa Dar es salaam, utaletewa kitabu chako popote ulipo.
  6. Kama upo mkoani utatumiwa kitabu chako kwa magari ya mizigo.
  7. Na kama utasoma kitabu chako na ukaona hakijakusaidia, nipigie kisha tutakurudishia pesa zako zote pamoja nyongeza ya gharama ya usumbufu tuliokuletea.
  8. KWASABABU Ya Maombi Wa WATEJA WETU WENGI leo utakipata kitabu chenye thamani Ya Dola 50, unakipata kwa TSHS 14,999 Tu!
  9. Unasubiri nini?…
  10. Sema TABIA ZA KITAJIRI.

Kila Lakheri,

Shabiki Yako Ninayekuamini,

AmryRamadhani|CopywriterOfSomaVitabuTanzani|

Karibu, USOME www.somavitabu.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post