Je Utajiri Unatokana na Nini?…

Je Utajiri Unatokana Na Nini?…

Rafiki Yangu Mpambanaji, leo ni siku ambayo unakwenda kujua na kuelewa utajiri unatokana na nini,

…endapo tu utasoma makala hii mpaka mwisho.

Ukweli ni kwamba utajiri unatengenezwa na vitu viwili (2) vikubwa;

 1; NAMNA YA KUFIKIRI.

Kiungo cha kwanza muhimu cha sayansi ya utajiri ni NAMNA YA KUFIKIRI.

Kuna namna ya kufikiri ambayo matajiri wanaijua na wanaitumia wakati masikini hawaijui na wala hawaitumii.

 Matajiri wanafikiri chanya kuhusu fedha na utajiri,

…wanafikiri kuhusu uwezekano na wanajua kuna utele wa chochote wanachotaka kwenye maisha yao.

Wanajua hakuna kinachokosekana wala hawahitaji  kuwanyang’anya wengine ili kupata wanachotaka.

Wanajua dunia ina rasilimali za kutosha na haziwezi kuisha kamwe,

…kwa sababu dunia inaendelea kuzalisha rasilimali hizo muhimu.

 Kwa njia hii ya kufikiri, matajiri wanakuwa watu wa shukrani na ushirikiano na wengine.

Kwa upande wa pili, masikini wana namna ya kufikiri ambayo inawaweka kwenye umasikini maisha yao yote.

Kwanza wanaamini utajiri siyo kitu kizuri, wanajiambia umasikini ndiyo bora.

Pia wanaamini kwenye uhaba, kwamba dunia ina uchache na wachache pekee ndiyo wanaoweza kunufaika na rasilimali chache zilizopo.

 Kwa kuwa na mtazamo huu, masikini hufikiri ili wao wapate lazima wengine wakose,

…hivyo muda wote wanakuwa kwenye hali ya ushindani na hawatoi ushirikiano kwa wengine.

Unapaswa kujenga namna bora ya kufikiri ili kutoka kwenye umasikini na kwenda kwenye utajiri mkubwa.

2; NAMNA YA KUTENDA.

Kiungo cha pili cha sayansi ya utajiri ni namna ya kutenda.

Wale wanaotajirika wana namna ya kufanya mambo yao ambayo inawaletea matokeo makubwa na mazuri sana.

Wakishapanga kitu cha kufanya, wanachukua hatua mara moja,

… hawaahirishi kitu na hawaruhusu usumbufu wowote uwatoe kwenye kile wanachofanya.

Watu hawa wana vipaumbele ambavyo wanavisimamia na kufanyia kazi.

Na chochote wanachofanya, wanakifanya kwa ubora wa hali ya juu sana.

Wanatoa thamani kubwa sana kwa wengine kupitia kile anachofanya.

Na hili ndiyo linalovutia utajiri na mafanikio makubwa kwao.

Kwa upande wa pili,

…masikini wana namna yao ya kutenda ambayo inawafanya waendelee kuwa masikini kwa maisha yao yote.

 Kwanza kabisa hawajui wanataka nini, hivyo muda wote wako ‘bize’ lakini hakuna matokeo wanayopata.

Pili ni wazuri kwenye kuahirisha mambo, wanapanga wenyewe vitu vya kufanya lakini unapofika wakati wa kufanya wanajiambia watafanya kesho.

Wamezungukwa na kila aina ya usumbufu na hawataki kupitwa na chochote,

…hili linawachosha kabla hata hawajafanya kazi.

Na hata pale wanapofanya kazi, wanaifanya kwa ukawaida sana, kama vile hawataki,

…hawatoi thamani kubwa na hivyo hawawezi kuvutia utajiri na mafanikio makubwa kwao.

Ni namna ya kufikiri na namna ya kutenda ndiyo vitu pekee vinavyowatofautisha wanaofikia utajiri na wanaobaki kwenye umasikini.

Habari njema, ni kwamba unaweza kutoka kwenye UMASIKINI  kwa kusoma kitabu kipya cha TABIA ZA KITAJIRI,

…utaweza kujenga msingi mzuri sana wa namna ya kufikiri na kutenda kila siku ili uweze kupiga hatua na kufikia utajiri mkubwa na kuishi maisha yenye furaha na amani.

KARIBU, kupata kitabu chako cha TABIA ZA KITAJIRI.

Sasahivi, tuma meseji yenye neno “UTAJIRI” kwenye WHATSAPP Namba 0752977170.

…kisha nitakupa utaratibu wa kupata kitabu chako.

Bado ni Tshs 14,999Tu! Badala Ya Tshs 20,000,

OKOA Tshs 5,000 NZIMA.

Ni LEO….

Unasubiri Nini?

Tuwasiliane 0752977170.

Shabiki Yako Ninayekupenda,

AmryRamadhani|CopywriterOfSomaVitabuTanzania|

Karibu, usome www.somavitabu.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post