GUNDUA; Njia Rahisi Ya Kugeuza Kikwazo Chochote Kuwa Fursa Kwako…

Rafiki Yangu,

Hata kama unakutana na kila aina ya kikwazo kwenye maisha yako, habari njema ni kwamba leo unakwenda kugundua njia rahisi ya kugeuza kikwazo chochote kuwa fursa kwako.

Unaweza ukawa unajiuliza nitawezaje kugundua njia hiyo?…

Uzuri ni kwamba ukisoma makala hii mpaka mwisho, utaweza kupata jibu la swali lako hapo juu.

Pamoja na kuwa na malengo na mipango mizuri. Pamoja na kuwa tayari kuweka juhudi kubwa ili kufikia malengo yako. Safari haitakuwa rahisi, njia haitakuwa nyoofu,utakutana na kila aina ya vikwazo na changamoto. Kama kweli unataka kufikia malengo yako, basi hupaswi kuruhusu kikwazo au changamoto yoyote ikuzuie. Badala Yake unapaswa kugeuza kila kikwazo kuwa ndiyo njia.

Kama unataka kuanzisha au kukuza biasharayako  ila kikwazo ni mtaji, usiruhusu hilo likuzuie, badala yake geuza kukosa mtaji kuwa ndiyo njia ya wewe kuanzisha au kukuza biashara yako. Kama unataka kuandika kitabu lakini kikwazo ni huna muda, tumia ukosefu huo wa muda kama njia ya kuwa mwandishi. Hakuna kikwazo chochote ambacho hakiwezi kuwa njia unayoweza kutumia kufikia malengo yako.

Unachohitaji ni kubadili mtazamo wako. Unapokutana na kikwazo chochote badala ya kujiuliza unakikimbiaje, jiulize kinawezaje kuwa njia kwako kufika unakotaka. Swali hilo rahisi lina nguvu ya kubadili kila kitu kwenye safari yako ya mafanikio. Kila unapokutana na kikwazo kwenye njia yako ya kuelekea kwenye mafanikio, jiulize unawezaje kukitumia kama njia ya wewe  kufikia mafanikio yako. Azimia kwamba hakuna kitakachoweza kukuzuia kufanikiwa na kila kinachokuja kwako kinakuwa njia.

Yageuze maisha yako kuwa moto ambao unawaka kwa ukubwa na chochote kinachoingia kwenye moto huo kinawaka pia. Maisha yako yawe moto wa mafanikio unaowaka bila kuzima na chochote kinachokuja kama kikwazo kinakuwa nishati ya kuchochea moto huo zaidi.

 Hayo yote hapo juu yanawezekana endapo tu!

Utaweza kujitamkia kila siku maneno haya” Sikubali Kikwazo au changamoto yoyote inizue kufikia malengo yangu. Nageuza Kila Kikwazo Kuwa Njia Ya Mimi Kuyafikia Malengo Yangu”

Rafiki Yangu,

Kama unataka kuachana na maisha ya kawaida. 
Kama unataka kuacha kwenda kwa mazoea.
Na kama unataka kuacha alama hapa duniani,
Jipatie leo na usome kitabu cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO.
Kwa Kupiga simu kwenda namba ; 0752977170.

Kutoka Rafiki Yako Anayekujali Sana,

Bwana Rama|Copywriter Of SomaVitabuTanzania|

Karibu. www.somavitabu.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post