Njia 1 Pekee Ya Wewe Kupata Unachokitaka Bila Kupoteza Muda…

Rafiki yangu,

Leo hii unakwenda kupata unachotaka kwenye maisha yako…

Kama umeshajaribu kila njia kufikia malengo yako bila mafanikio hayo sio makosa yako bali makosa yapo katika kutokujua…

Hata kama umeshajaribu kila njia ili uweze kufikia malengo yako bila mafanikio basi usiwe na wasiwasi  ondoa hofu na relax kitu pekee unachotakiwa kufanya ili kupata unachotaka ni kusoma makala hii mpaka mwisho.

Kupoteza muda bila mafanikio inakera sana…

Uhitaji Elimu kubwa sana, ili kuelewa hili bali unahitaji umakini kidogo tu!…

Swali ni Je Matendo Yako Yanaendane Na Maneno Yako?…

Jibu unalo, haya twende pamoja…

Tumekuwa hatupati tunachotaka na wakati huo huo tunakuwa haturidhiki na maisha tuliyonayo.

Na hii siyo kwa sababu wengine wanapata wanachotaka au wana maisha bora sana kuliko sisi,

…bali kwa sababu tunajua tunajikwamisha wenyewe.

Tumekuwa tunajikwamisha sisi wenyewe pale ambapo maneno yetu hayaendani na matendo yetu.

Tunasema na kuweka mipango mikubwa, tunakuwa na malengo makubwa sana, na pia tunatamani kufika hatua za juu zaidi.

Lakini hatua tunazochukua zinakuwa ni hatua za kawaida sana, hatua ambazo tumekuwa tunachukua maisha yetu yote.

Kwa hatua hizo tunazochukua, tunapata matokeo yale yale ambayo tumezoea kuyapata, na hapa ndipo tunapoona labda sisi hatuna bahati.

Ukweli uko wazi rafiki, huwezi kufika unakotaka kama matendo yako hayaendani na maneno yako.

Kama unafikiria makubwa na kufanya kidogo, huwezi kamwe kupata makubwa.

Utaishi kupata matokeo yanayoendana na hatua unazochukua, bila ya kujali unafikiri makubwa kiasi gani, hata kama unaamini inawezekana kiasi gani.

Utapata unachofanyia kazi, na siyo unachofikiri au kutamani.

Kila siku jikumbushe hili, kila unapoyaandika malengo yako, jiulize je kwa hatua unazochukua utayafikia malengo hayo?

Kila hatua unayochukua jiulize ina mchango kiasi gani kukufikisha kwenye malengo yako makubwa.

Kama umeingia facebook au instagram mara 5 kwa siku, jiulize je kuingia kwako instagramu mara hizo 5 kwa siku kuna mchango gani kwako kufikia mafanikio makubwa?

Kama umebishana na watu kwa saa nzima, au umeangalia habari kwa saa nzima, jiulize je saa hiyo nzima umeiwekeza sawasawa ili kufika kule unakotaka?

Ukianza kufikiri hivi rafiki, utajirekebisha maeneo mengi sana, utajikamata ukiwa unafanya mambo yasiyo muhimu kwako na mara zote utakuwa na vipaumbele unavyofanyia kazi.

 Utaacha kufanya vitu kwa mazoea na kuiga wengine na utaanza kufanya vitu kwa umuhimu na kipaumbele.

Matendo yako yaendane na maneno yako, ndiyo njia pekee ya wewe kupata unachotaka.

Rafiki Yangu,

Kama unataka kupata chochote unachotaka kwenye maisha yako.

Kama unataka kuachana na maisha ya kawaida. 
Kama unataka kuacha kwenda kwa mazoea.
Na kama unataka kuacha alama hapa duniani,

Nakushauri  usome  kitabu kinachoitwa MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO ambacho ni nguzo muhimu sana kwa mafanikio yako.
Kitabu hiki kina maarifa muhimu sana unayohitaji ili uweze kufanikiwa kwenye maisha yako.
Piga simu kwenda namba 0752977170  sasahivi kupata kitabu chako cha MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO.

MUHIMU; Watu 17 wa kwanza watapata kitabu hiki kwa OFA ya Tshs 19,999 Tu (Badala ya Tshs 50,000 na tayari nafasi 7 zimeshachukuliwa).

Kutoka Kwa Rafiki Yako Anayekujali Sana,

Bwana Rama|CopywriterOfSomaVitabuTanzania|

Karibu. www.somavitabu.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post