Mitandao Ya Kijamii na Fursa Zinavyokupita Kushoto…
Rafiki Yangu,
Sekunde 5 Zijazo Unaenda Kusoma Kitu Ambacho Kitaufungua Ubongo Wako na Hivyo Utapata Muda Wa Kuitumia Fursa Hii Adhimu Kila Siku.
Ukweli ni kwamba Mitandao Ya kijamii inakunyima Fursa Ya Muda Wa Kuwa Pekee Yako.
…kwa sababu ya urahisi wa kukufikia.
Ukichukua mfano, kabla ya ujio wa simu janja, watu hawakuwa na mawasiliano ya muda wote wa siku.
Hivyo kama upo kwenye kazi na huna cha kufanya, ulilazimika kukaa peke yako na mawazo yako.
Au kama uko na watu wengine, ulilazimika kujihusisha na mazungumzo na watu hao, kwa sababu hukuwa na kitu kingine cha kufanya.
Kwa kifupi, kabla ya ujio wa simu janja na mitandao ya kijamii, maisha yako ya kawaida yalikuwa yanakulazimisha uwe na muda wako peke yako.
Na hapo ulipata nafasi ya kuyatafakari maisha yako na hata kuja na mawazo mazuri na suluhisho la changamoto mbalimbali.
Lakini baada ya kuja kwa simu janja na mitandao ya kijamii, mambo yamebadilika.
1. Urahisi wa kubeba simu hizi umefanya tuweze kuwa nazo kwa masaa 24 ya siku na siku 7 za wiki.
Hatuwezi hata kwenda kitandani na kuacha simu zetu, ni kama zimegandishwa kwenye mikono yetu.
Siku hizi hata mgeni akifika nyumbani, kitu cha kwanza ni kuchaji simu yake, ili isiishe chaji akapitwa na dunia.
2. Kuwa na simu hizi muda wote zinaondoa kabisa ile nafasi ya mtu kuwa peke yako na mawazo yako.
Ukiwa kwenye kazi na huna cha kufanya nini kinaendelea?
Unajiambia wacha niingie facebook au instagram mara moja, na unakuja kustuka nusu saa baadaye unazidi kushuka tu kuangalia maisha ya wengine yanaendeleaje.
3. Simu janja na mitandao ya kijamii inatunyima kabisa ile hali ya uchoshi, na hivyo mtu anapochoka kidogo kwenye kitu chochote anachofanya, badala ya kukaa na kufikiri, anakimbilia kwenye mitandao ya kijamii.
4. Mitandao hii inatupa njia rahisi ya kutoroka matatizo au changamoto zetu.
Mtu anakabiliwa na changamoto fulani kwenye maisha yake, badala ya kuitatua yeye anakimbilia kwenye kitandao ya kijamii kulalamika kuhusu changamoto hiyo.
5. Mitandao hii inatulaghai kwamba unaweza kuchungulia mara moja na kutoka, lakini hakuna anayeweza kufanya hivyo.
Kila unapochungulia unaletewa vitu vya kuvutia zaidi na kujikuta umetumia muda mwingi kuliko ulivyopanga.
Kwa njia hizi, simu janja na mitandao ya kijamii imetunyima kabisa nafasi ya kukaa peke yetu na mawazo yetu.
Imekuwa usumbufu mkubwa kwetu ambao umetuganda na hatupati kabisa muda wa upweke ambao ni muhimu kwa ukuaji wetu kama binadamu.
Swali ni Je, Utawezaje Kuidhibiti Hii Mitandao Ya Kijamii na Kuweza Kuitumia Kwa Manufaa Yako?….
Jibu la swali hili lipo ndani ya kitabu cha EPUKA UTUMWA KIDIJITALI,
Kama tayari unacho Fungua ukurasa wa 134 wa kitabu chako.
Kama bado hujapata kitabu chao tuwasiliane sasa hivi kwa kupiga simu namba 0752977170.
Na kwa sababu nakupenda nimekulipia Tshs 5,000 NZIMA,
Kwahiyo leo utakipata kwa bei ya ofa ya Tshs 14,999 Tu Badala Ya Tshs 20,000.
Piga simu namba 0752977170.
Uletewe kitabu chako.
Kila Lakheri,
Nakupenda.
Kutoka Kwa Shabiki Yako Namba 1,
AmryRamadhani|CopywriterOfSomaVitabuTanzania|