ANGALAU SASA! Unaweza Kujifunza Jinsi Ya Kuuepuka Usumbufu Unaokuzuia Kufanikiwa Bila Kupoteza Muda…!

ANGALAU SASA! Unaweza Kujifunza Jinsi Ya Kuepuka Usumbufu Unaokuzuia Kufanikiwa Bila Kupoteza Muda…!

Kama umekuwa unashindwa kuweka umakini kwenye yale unayofanya , basi naku sii usifanye kosa la kutokusoma makala hii mpaka mwisho.

Umakini wako ndiyo utajiri wako, kama utaweza kuweka umakini wako wote kwenye kile unachofanya, kwa hakika utaweza kuongeza kipato chako maradufu.

Mtaalam Mmoja Aliwahi Kusema Hivii. Siku zijazo, kutakuwa na makundi makuu mawili ya watu duniani.

Kundi la kwanza litakuwa la wale ambao wanaruhusu umakini wao kudhibitiwa na watu wengine, ambao wanaruhusu kila aina ya usumbufu kuwaingia. Kundi hili litakuwa na watu wengi sana, na mara zote watakuwa wamevurugwa na wasiweze kufanya makubwa kwenye maisha yao.

Kundi la pili litakuwa la wale ambao wanadhibiti umakini wao na kutoruhusu usumbufu wa aina yoyote ile kuwavuruga. Kundi hili litakuwa na watu wachache sana, na hawa ndiyo watakaoweza kufanya makubwa na kufanikiwa sana.”

Swali kwako, je kwa hali inavyokwenda sasa kwenye maisha yako, unajiona ukielekea kwenye kundi lipi kati ya hayo mawili?

Na je ungependa kuwa kwenye kundi lipi? Kama ungependa kuwa kwenye kundi la kwanza huna cha kufanya, endelea kufuata mkumbo na kila aina ya kelele.

Lakini kama ungependa kuwa kwenye kundi la pili, basi yale yote ambayo umejifunza kwenye kitabu cha juma hili yafanyie kazi.

Jua usumbufu wako wa ndani na wa nje na tenga muda wa kufanya yale muhimu na kuepukana na usumbufu.

Maarifa tayari unayo, kama hutachukua hatua huna wa kumlaumu, utakuwa umechagua wewe mwenyewe.

LEO, Unaweza Kuuepuka Usumbufu Unaokuzuia Kufanikiwa Kwa Kusoma Kitabu Kinachoitwa EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI, Kwa Sababu Utajifunza Jinsi Ya Kutenga Muda Wa Kufanya Yale Muhimu Na Kujizuia Kufanya Yale Ambayo Siyo Sahihi.

Kwenye kitabu cha “EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI” utajifunza mpango kamili wa kuondoa usumbufu kwenye maisha yako, ufanyie kazi ili uweze kuwa na umakini makubwa na kuongeza kipato chako pia.

Ndani ya kitabu cha “EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI “utajifunza mambo saba(7) makubwa ambayo yatakufanya uwe huru na yatakayo yataharakisha safari yako ya mafanikio.

Moja utajifunza jinsi ubongo wako unavyofanya kazi na namna teknolojia mpya zinavyotumia ubongo huo kukufanya kuwa mtumwa.

Teknolojia mpya zimetengenezwa kwa namna ambayo zitajenga uteja/uraibu kwenye ubongo wako.

Kwa kujua njia hiyo utaweza kuepuka kuingia kwenye utumwa wa teknolojia hizo.

Mbili utajifunza kuhusu zama tunazoishi sasa, zama za maarifa na taarifa lakini ambazo zimegeuka kuwa zama za usumbufu.

Utajifunza zama hizi za usumbufu zimetengeneza makundi makubwa mawili, wachache wanaonufaika sana, kama Mark Zuckerberg ambaye ni mmiliki wa Facebook na wengi ambao ni kama watumwa wa wachache hao wanaonufaika.

Tatu utajifunza jinsi ya kujua kama tayari umeshanasa na kuwa mtumwa wa teknolojia hizo mpya.

 Unaposoma hapa unaweza kusema wewe hujawa mtumwa, unatumia kwa kupanga mwenyewe, lakini nikuambie kitu kimoja, kwa sehemu kubwa sana umeshakuwa na utaziona dalili kwa kusoma kitabu hiki.

Nne utajifunza jinsi ya kuondoka kwenye utumwa wa kidijitali ambao umeshaingia.

Baada ya kuona jinsi ambavyo umenasa kwenye utumwa huo, utajifunza njia za kujinasua.

Hapa utajifunza jinsi ya kuizidi ujanja simu janja yako.

Tano utajifunza falsafa mpya ya kuendesha maisha yako kwa uhuru katika zama hizi za usumbufu.

Pamoja na kujifunza kuhusu zama hizo na jinsi ya kuondokana na utumwa wake, usumbufu wake hautaisha, teknolojia mpya zinaendelea kugunduliwa kila siku na zikiwa na ushawishi mkubwa.

Hivyo unahitaji kuwa na falsafa unayoitumia kuchagua huduma za kidijitali utakazochagua kutumia kwa manufaa yako.

Sita utajifunza jinsi ya kutumia akili yako kuvunja uraibu wowote ambao umeshajijengea.

Kama tulivyoona, huduma za kidijitali zinatumia jinsi ubongo unavyofanya kazi kukuingiza kwenye utumwa.

Hivyo wewe unapaswa kuutumia ubongo wako vizuri kuondoka kwenye utumwa huo.

Saba utajifunza sababu kumi kwa nini unapaswa kuondoka kwenye mitandao yote ya kijamii sasa hivi.

 Hizi ni sababu ambazo zimechambua jinsi matumizi ya mitandao ya kijamii yalivyo na athari kwenye akili yako, utulivu wako, mahusiano yako, uchumi wako na hata imani yako.

 Kwa kuzijua sababu hizi kumi, utajionea mwenyewe jinsi ulivyorudi nyuma tangu umeanza kutumia mitandao hiyo na hivyo kuachana nayo ili kuepuka madhara yake.

Mwisho kabisa utajifunza njia za kutumia kufanya maamuzi iwapo utumie huduma ya kidijitali.

Utajifunza jinsi ya kutumia vigezo vitatu vya AFYA, UTAJIRI na HEKIMA katika kuchagua na kutumia teknolojia mpya, ambazo zitakuwa na manufaa kwako badala ya kukufanya mtumwa.

Tuko kwenye vita, adui mkuu anajua yuko vitani ila wanaolengwa hawajui.

Hivyo unapaswa kuwa na maandalizi mazuri ya kupambana na vita hii ili uweze kutoka salama na siyo kuwa mfungwa.

Pata na usome kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI ili upate mbinu za kupambana kwenye vita hii na kutoka ukiwa mshindi.

Kitabu hiki kimechapwa kwa nakala ngumu (hardcopy).

Wekeza LEO  tsh elfu 20 (20,000/=) TU!, ambazo zitakulipa zaidi huko mbeleni.

 Ili kukipata Sasa Hivi Tuma Ujumbe ” EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI” Kwenda Namba 0752 977 170 na utaletewa au kutumiwa kitabu popote ulipo Tanzania na Afrika Mashariki.

MUHIMU; Kama utanunua na kusoma kitabu hiki na ukaona hakina manufaa yoyote kwako, unaruhusiwa kukirudisha na ukarejeshewa fedha zako.

 Hivyo chukua hatua sasa, huna cha kupoteza lakini una mengi ya kupata, yatakayokuweka huru kwenye zama tunazoishi sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post