Thamani Ya Maisha Yako Imefichwa Kwenye Kitu Hiki Nasio Hiko…

*Thamani Ya Maisha Yako imefichwa Kwenye Kitu Hiki Nasio Hiko* …

Rafiki Yangu Mpendwa,

Je Mpaka Sasa Umeshaijua Thamani Ya Maisha Yako?

Na habari njema ni kwamba ukiweza leo hii kuijua kwani utaweza kujithamini, kujiheshimu, kujipenda na kubwa kuliko utaongeza hali ya kujiamini,

… na hivyo utaweza kufanya mambo makubwa kuwahi kutokea.

Na leo nikurudishe nyuma kidogo tarehe 15|3|1997 nchini Brazili kulikuwa na kijana machachari sana aliyejulikana kwa jina la DO’SANTOS kipindi hiko alikuwa ana miaka 17Tu! .

Na alikuwa anaishi na Baba Yake ambaye alisifika sana kwa kuwa na HEKIMA sana.
Na mbaya Zaidi kilichokuwa kinampa HUZUNI muda wote ni yeye kutokuijua thamani yake imejificha wapi.

Na alijaribu kuitafuta kwa kila namna kwa kuomba ushauri kwa kila mtu LAKINI aliishia kujisikia vibaya Zaidi na mwishowe alidharaulika sana.

Hivyo baada ya kusumbuka kwa muda mrefu ndipo akaamua kumuuliza BABA YAKE.

DO’SANTOS Alisikika Akisema Baba Ni Ipi Thamani Yangu?

Na kwasababu baba yake alikuwa na hekima sana.

Kabla ya kumjibu alimtengenezea mwanaye mazingira ili aweze kuuona ukweli mwenyewe kwa kumwambia kesho kuna sehemu nitakutuma.

DO’SANTOS akaitikia kinyonge sawa BABA,
Na siku iliyofuata Asubuhi Baba alimuita DOS’ANTOS Na Kumtuma SOKONI,

…lakini cha kushangaza Alimpa JIWE KUBWA LILILOCHONGOKA,

Akamwambie akifika SOKONI alinyooshe juu bila ya kusema chochote,

Na atakayemuuliza ANYOOSHE JUU VIDOLE VITATU (3) VYA KUSHOTO,

…bila ya kusema chochote.

Ghafla akatokea Mdada Mmoja Mrembo Mweupe, Akilishangaa Lile JiWE KUBWA LA KUVUTIA,

Akisema WOW! AMAZING.

DO’SANTOS akatabasamu yule mdada akauliza UNA LIUZA DOLA NGAPI?

DO’SANTOS akaendelea kunyoosha juu vidole vitatu (3) bila ya kusema chochote,

Basi yule mdada akauliza kwa sauti kubwa DOLA 30,000 ?

Siamini macho yangu na siwezi kuiacha hii fursa inipite,

DOSANTOS akatabasamu na kukimbia nakurudi nyumbani na kwenda kumueleza BABA YAKE kile kilichojiri,

BABA YAKE akatabasamu kisha akamwambia VIZURI SANA,

Na siku Ya Pili Asubuhi Baba alimwita DO’SANTOS Na Kumtuma MAKUMBUSHO.

Na Alimpatia Lile Lile JIWE KUBWA LILILOCHONGOKA,

Akamwambie akifika MAKUMBUSHO Alinyooshe Juu Bila Ya Kusema Chochote,

Na atakayemuuliza ANYOOSHE JUU VIDOLE VITATU (3) VYA KUSHOTO,

….bila kusema chochote.

Ghafla akatokea Kijana Mmoja Wa Makamo Pale Mapokezi  ,

Akilishangaa Lile JiWE KUBWA LA KUVUTIA, kwa muda,

…kisha akamuuliza DOSANTOS UNA LIUZA DOLA NGAPI?

DO’SANTOS akaendelea kunyoosha juu vidole vitatu (3) bila ya kusema chochote,

Basi yule Kaka akauliza kwa sauti kubwa DOLA 300,000 ?

Siamini macho yangu na siwezi kuiacha hii fursa inipite,

Nilijua Utaniambia Dolla 30,000,000 (Dola Millioni Thelathini)

DOSANTOS akatabasamu na kukimbia nakurudi nyumbani na kwenda kumueleza BABA YAKE kile kilichojiri,

BABA YAKE akatabasamu kisha akamwambia VIZURI SANA.

Kama ilivyo kawaida siku ya kwanza, siku ya pili na leo ni siku ya tatu,

Asubuhi Baba akamwita DO’SANTOS Na Akamtuma Kwenye UKUMBI WA MAONYESHO,
…lakini cha kushangaza Alimpa LILE LILE JIWE KUBWA LILILOCHONGOKA,

Akamwambie akiingia kwenye  UKUMBI WA MAONYESHO alinyooshe juu bila ya kusema chochote,

Na atakayemuuliza ANYOOSHE JUU VIDOLE VITATU (3) VYA KUSHOTO,

…bila kusema chochote.

Ghafla mzee wa makamo akamfuata DO’SANTOS pale aliposimama,

Akisema WOW! AMAZING  I Have Never Seen Before (Akiwa na Maana Kwamba Anashangaa Na Hajawahi Kuona JIWE kama HiLo Hapo Kabla)

DO’SANTOS akatabasamu yule mzee akauliza UNA LIUZA DOLA NGAPI?

DO’SANTOS akaendelea kunyoosha juu vidole vitatu (3) bila ya kuongea chochote,

Basi yule mzee akashangaa kwa kuuliza kwa sauti kubwa DOLA 3,000,000 ?

Siamini macho yangu na hauwezi kuwa seriazi,
Nilijua Utaniambia Dolla 300,000,000 (Dola Millioni Mia Tatu)

DO’SANTOS akatabasamu na kukimbia nakurudi nyumbani na kwenda kumueleza BABA YAKE kile kilichojiri,

BABA YAKE akatabasamu kisha akamwambia VIZURI SANA,

Kisha ndio akamwambia DOSANTOS Mwanangu UMEELEWA THAMANI YA MAISHA YAKO?

DO’SANTOS Akajibu NDIYO,

Baba akaendelea kumwambia THAMANI YA MAISHA YAKO INAPIMWA NA JINSI UNAVYOJIWEKA,

Unaweza Kuamua Kuwa Wa Dolla 30,000 au Kuwa Wa Dola 30,000,000,

Kwasababu Kuna baadhi ya watu watakupenda tu vile ulivyo,

Lakini kuna baadhi ya watu watakutumia tu kama bidhaa kwenye maisha yao na wasiione thamani yako.
Mpaka Pale Utakapoamua Kuionyesha Thamani Yako,

Na Njia Rahisi Zaidi Ya Kuongeza Thamani Yako,
Ni Kubadili Jinsi Unavyofikiri Na Jinsi Unavyotenda.

Hivyo, Thamani Yako Imejificha Kwenye Jinsi Unavyofikiri Na Unavyotenda,

Hapo Ndipo Pakuanzia,

Nikiwa namaana kwamba ukianza kubadili namna unavyojiona utaongeza thamani yako,

Na pia ukiweza kubadili namna unavyofanya kazi zako utaongeza ufanisi wako na thamani yako itapanda mara dufu.

Kwahiyo ukweli ni kwamba thamani yako imejificha kwenye fikra zako na matendo yako.

Na Imegundulika Kwamba Msomaji Wa Vitabu Vizuri Na Akafanyia Kazi Yale Yote Anayojifunza Kila Siku Ana  99.9% Kuongeza Kipato Chake Mara Dufu Baada Ya Kuionyesha Thamani Yake,

…kuliko yule ambaye hasomi kabisa vitabu ,

Na Kama Mpaka Sasa Hujui Vitabu Vizuri Utavipata Wapi,

Basi Bonyeza Hapa    *https://wa.link/ngxgc4*       Sasahivi,

Kisha Nitakushauri Vya Kuanza Navyo.

Kila Lakheri, Tukutane Kileleni,

Na Hii Meseji Imetoka Kwa Rafiki Yako Anayekujali Na Kukukubali Sana,

*Bwana Amir Ramadhani*
|CopywriterOfSomaVitabuTanzania||Sales Consultant|

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post