99.97 Anza Kabla Hujawa Tayari.

99.97 Anza Kabla Hujawa Tayari.

Rafiki Yangu Mkubwa,

Utapata Nguvu Kubwa Sana Ya Akili Baada Ya Kuanza.

Na leo unaenda kujifunza kutoka kwa MWANZILISHI WA MGAHAWA,

Na ukifanikiwa kusoma makala hii fupi mpaka mwisho basi utapata amani ya moyo wako.

Pata picha MWANZILISHI WA MGAHAWA, alianza kabla hajawa tayari na sasahivi anavyo vile ambavyo alikuwa hana kabla hajaanza.

Anzia hapa kwanza,

Kitu kimoja ambacho kimekuwa kinawakwamisha wengi wasiingie kwenye biashara ni kutokuwa tayari.

Labda wazo ambalo mtu analo linakuwa halijakamilika,

… mtaji alionao hautoshi,

… hajapata kila alichotaka ili kuanza biashara na mengine mengi.

Kwa kuwa mtu anakuwa hajawa tayari,

… anajiambia ni sahihi kwake kuendelea kusubiri,

Na anaendelea kujifariji ni sahihi kwake kutokuanza kwa sababu bado hajapata kila ambacho anataka kuwa nacho ili aanze.

Japo kwa fikra za kawaida hilo linaweza kuonekana kuwa sawa,

…kwa upande wa mafanikio siyo sawa.

Hakuna wakati wowote ule ambao utakuwa tayari kwa kila kitu ndiyo uanze.

Kila wakati kuna kitu utakuwa unakosa,

…kuna kitu ambacho kitakuwa hakijakamilika.

Hivyo njia pekee ya kuanza biashara na kufanikiwa, ni kuanza kabla hujawa tayari.

Leo Jifunze Kutoka Kwa Mwanzilishi Wa Mgahawa.

Fred DeLuca ambaye ni mwanzilishi wa migahawa inayouza vyakula vya haraka (Subway) anatushirikisha,

…jinsi alivyoingia kwenye biashara kabla hajawa tayari,

…akakutana na changamoto nyingi lakini kwa kupambana nazo akaweza kufanikiwa.

Fred anatuambia kilichomsukuma kuingia kwenye biashara ilikuwa ni kupata ada ya kujisomesha chuo.

Kwa sababu wazazi wake hawakuwa na uwezo wa kumlipia ada,

…alikuwa akijishughulisha mwenyewe
kwenye vibarua mbalimbali.

Lakini kipato alichokuwa anaingiza kupitia vibarua, kisingetosha kuweza kumlipia ada ya chuo.

Hivyo alienda kwa rafiki wa baba yake, aitwaye Pete,

…ambaye alikuwa na uwezo kidogo maana alikuwa mwajiriwa,

…akamuomba ushauri anawezaje kupata ada ya chuo.

Fred anasema wakati anaomba ushauri huo, kwenye mawazo yake alitegemea rafiki huyo angemkopesha fedha ili aje kulipa baadaye.

Lakini alichomwambia ni kwa nini usianzishe biashara?

Fred alimuuliza kwa mshangao, biashara gani?

Ndipo Pete akamwambia kwamba amesoma kwenye gazeti kuna mtu anafanya biashara ya migahawa na ana migahawa 32 licha ya kuwa alianza kwa hatua ndogo sana.

Fred alifikiria hajawahi kufanya biashara yoyote,

… na hata huyo Pete anayemshauri aingie kwenye biashara hajawahi kufanya biashara bali tu amesoma kuhusu mtu aliyefanikiwa kwenye biashara.

Alianza kumweleza Pete kwamba hilo halitawezekana kwa sababu hana uzoefu wala mtaji.

Pete akamjibu nipo tayari kuwa mshirika wako, na nitakupa mtaji wa kuanza.

Kwa nafasi hiyo ya kupata mtaji,

Fred aliona hana cha kupoteza, hivyo alikubali kuingia kwenye biashara,

…huku akiwa hajui chochote kuhusu biashara hiyo.

Baada ya kukubaliana kuingia kwenye biashara pamoja,

Pete alimwambia Fred ni lazima wajiwekee lengo, na kupitia hamasa aliyoipata baada ya kusoma mtu mwingine aliyefanikiwa,

…waliweka lengo la kuwa na migahawa 32 ndani ya miaka kumi,

Lengo ambalo hawakujua hata watalifikiaje, lakini walijiwekea lengo hilo.

Walianza kutafuta eneo la kufanyia biashara yao, na kwa sababu mtaji walioanza nao ulikuwa kidogo,

…hawakuweza kumudu maeneo mazuri.

Hivyo walipata eneo ambalo halikuwa sehemu nzuri ambayo watu wanapita.

Baada ya kupata eneo, walianza kufanya utafiti kwa kwenda kula kwenye migahawa mingine inayotengeneza vyakula vya haraka.

Walienda kama wateja lakini walitumia kila fursa kuchunguza jinsi ambavyo migahawa hiyo inaendeshwa, jinsi vyakula vinavyoandaliwa na mengine mengi.

Baada ya utafiti huo mfupi, mwaka 1965 walifungua mgahawa wao wa kwanza, kwa mtaji mdogo wa dola elfu moja pekee.

Siku ya kwanza ya ufunguzi ilikuwa nzuri sana, watu walikuwa wengi kiasi cha kushindwa kuwahudumia.

Walipata matumaini kwamba biashara hiyo ni nzuri na watafanikiwa sana.

Lakini hawakuwa sahihi, kadiri siku zilivyokwenda ndivyo wateja walivyopungua na kipato kuwa kidogo.

Biashara ilianza kujiendesha kwa hasara.

Kwa bahati nzuri sana, Pete na Fred walikuwa na utaratibu wa kuwa na kikao cha kibiashara kila siku ya jumatatu usiku.

Siku hiyo walipita namba muhimu walizokuwa wanafuatilia kwenye biashara yao,

…hasa mauzo, idadi ya wateja na faida.

Walipoona kila wiki wateja na mauzo vinapungua,

…waliona kuna umuhimu wa kuchukua hatua za haraka.

Walijifunza vitu vingi sana ambavyo hawakuwa wanavijua awali.

Walifanya makosa mengi kwa kutokujua,

…lakini kwa sababu walikuwa wameshaingia kwenye biashara, hawakuwa na budi bali kukabiliana na kila wanachokutana nacho.

Baada ya kuona mgahawa mmoja walionao hajiendeshi vizuri, walipata wazo la kufungua mgahawa mwingine.

Hili lilikuwa wazo la ajabu ambalo kama wangesema wanaenda kuomba mkopo benki,

…hakuna benki ambayo ingeweza kuwakubalia.

Yaani mgahawa wa kwanza unaendeshwa kwa hasara,

…halafu wanataka kufungua mgahawa mwingine?

Kwa falsafa ya Fred ya anza kabla hujawa tayari, walianzisha mgahawa mwingine,

…na hapo mauzo yalianza kupanda.

Wakaanzisha mwingine wa tatu na
mauzo yakazidi kupanda zaidi.

Miaka nane baadaye tangu waingie kwenye biashara, walikuwa wamefanikiwa kufungua migahawa 16
pekee.

Lengo lao ilikuwa ni kufungua migahawa 32 ndani ya miaka kumi.

Kwa miaka 2 iliyobaki aliona hawezi kufungua migahawa mingine 16.

Hivyo walifikiri kwa kina na kuja na wazo la kutoa kibali kwa watu wengine kuendesha mgahawa kwa mfumo wao (franchise).

Japokuwa hawakuwa wanajua chochote kuhusu aina hiyo ya uendeshaji wa biashara, waliona ndiyo sahihi kwao kufikia lengo.

Walikutana na changamoto nyingi mwanzo, lakini maamuzi hayo yaliwasaidia sana.

Kwani miaka 11 tangu waingia kwenye biashara walikuwa wamefungua migahawa 32, miaka 2 baadaye migahawa 100 na miaka mitano baada ya migahawa hiyo 100 walikuwa wamefungua migahawa 200.

Fred anatushirikisha mengi sana kuhusu safari yake ya kuingia kwenye biashara kabla hajawa tayari,

kuweka malengo makubwa na kujisukuma kuyafikia na kuweza kuukuza sana mgahawa wa Subway.

Kwa sasa mgahawa huu umesambaa dunia nzima na hata hapa Tanzania migahawa hii ipo.

Fred anakiri kwamba kama angesubiri mpaka awe tayari, asingeweza kuingia kwenye biashara hii ya mgahawa.

Anasema baada ya kuingia alikutana na vitu vingi ambavyo hakuvijua kuhusu biashara ya mgahawa,

…lakini kwa kuwa alishaingia hakuwa na namna bali kukabiliana navyo.

SOMO KUBWA;

Hivi ndivyo tunavyopaswa kuwa kama tunataka kuingia kwenye biashara na kufanikiwa.

Kama bado hujaingia kwenye biashara, basi anza kabla hujawa tayari.

Chagua sehemu yoyote unayoweza kuanzia,

…anza kidogo na anza na tatizo ambalo tayari watu wanalo na wapatie suluhisho la tatizo hilo. Utakutana na changamoto nyingi,

… lakini usikubali kukwama, kabiliana nazo na songa mbele.

Kama tayari upo kwenye biashara, jiwekee malengo makubwa zaidi ya yale unayofanyia kazi kwa sasa.

Malengo ambayo watu wengine wataona ni makubwa na hayawezekani, kisha jisukume kuyafikia.

Usisubiri mpaka uwe tayari, badala yake anza sasa, jiwekee lengo kubwa na anza kulifanyia kazi mpaka ulifikie.

Hakuna wakati ambao utakuwa tayari kwa kila unachotaka kiwe tayari.

Hivyo acha kujichelewesha na anza sasahivi,

… mengine utaendelea kuyafanyia kazi kadiri unavyokwenda.

Rafiki Yangu,

Kwa Mfano leo ukisoma kitabu hiki kipya kinachoitwa MJASIRIAMALI MJANJA,

…kinakufunulia mbinu na hatua za kufuata ili uweze kufikia malengo yako kabla hata hujawa tayari.

Kukipata Kitabu Hiki Kwa OFA Ya Tshs 19,999Tu Badala Ya Tshs 30,000.

Tuwasiliane kwa namba 0752977170.

KUMBUKA; Mwisho Wa Ofa Hii Ni Tarehe 30|9|2022, na zimebaki siku mbili ofa kuisha.

Karibu Sana,

Wako,

Rafiki Yako Anayekujali Sana,

Bwana AmiryRamadhani|CopywriterOfSomaVitabuTanzania|

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post