Unajua Kwanini Wanakosa Furaha?

Unajua Kwa Nini Wanakosa Furaha?

Ili uweze kufanikiwa kwenye malengo ambayo unayo ni lazima uwe mtu mwenye furaha.

Na wapo watu wengi sana ambao wamekosa furaha kwenye maisha yao na inawezekana hii imesababishwa na changamoto mtu anazozipitia mambo anayopitia, inawezekana ni changamoto za kifedha, changamoto za kimahusiano au ni changamoto za kiuongozi.

Lakini kuna jambo ambalo limenyanganya furaha ya watu wengi sana.

Lakini kitu kimoja ambacho watu wengi sana ambacho hawakifahamu furaha huwa haianzii nje furaha huwa inaanzia ndani yako.

 Na kuna vitu ambavyo watu waliofanikiwa siku zote kuwa na furaha kwenye maisha yao, wamezingatia na wamevifanya siku zote.

Kuna mambo ukiyafahamu utakuwa na furaha kila siku bila kujali nini kinaendelea, bila kujali hauna nini na ndio mambo leo ninataka uyazingatie na kujifunza, ili uweze kuyatumia kama sehemu ya kujenga furaha yako inawezekana kabisa kuwa na furaha kila siku kwenye maisha yako.

Jambo a ambalo mwanasaikolojia leonard ambalo alilisema 1954, ili uwe na furaha usijilinganishe na watu wengine , yeye alitumia concept nzuri sana, upward comparison na downward comparison, kwamba kuna kujilinganisha kwa juu yako au kujilinganisha chini yako, kwa watu wengine wenye mitazamo chanya inawasaidia kama kutamani lakini wengi sana inakuwa kama inawakatisha tamaa, wanajiona kama wamechelewa wanasema kwa kweli najiona kama nimechelewa.

Maana kama Yule kafanikiwa kiwango kile kwa nini mimi sijafanikiwa kwenye hichi.

 Lakini wale wanaojilinganisha na wachini yao tunasema wao wanajiona kama wamefanikiwa sana, wakijilinganisha na wale watu ambao wapo chini yao.

Mwanasaikolojia leonard, anasema ukifanya ulinganifu wako na watu wengine itakupa shida sana kufanikiwa kwako, kwa sababu ukweli ni kwamba (“somebody ten chapter it can be your one chapter”).

Kwamba sura ya kumi ya mtu mwingine unayemwangalia kwako inawezekana ikawa ni sura ya kwanza kwenye kitabu chako, kwa maneno mengine unapojilinganisha unakuwa hujui kinachoendelea kwenye maisha ya mtu mwingine watu wengi kwa ajili ya kujilinganisha wamejikuta wamejikuta wameingia kwenye maisha yenye gharama kubwa sana, wamejikuta wanatumia vitu katika viwango vikubwa kuliko walivyokuwa wanatakiwa.  

Mtu anajilazimisha kufanya mambo yaliyo juu sana ya uwezo wao, kutokana tu na kujilinganisha.

Unachotakiwa kujua ni kwamba watu wengi hawakuonyeshi kitu kilichopo wanakuonyesha kitu wanachotaka wewe ukione.

Rudia ili uelewe vizuri, watu hawaonyeshi kitu kilichopo kwao wanakuonyesha kitu wanachotaka wewe ukione.

Kitakacho tokea ni nini? Wewe utakuwa unajilinganisha na kitu ambacho wanataka wewe ukione lakini hujui uhalisia wa mambo yaliyojificha, lakini ushawahi kukutana na hali au ukasikia kitu cha mtu ukasema aisee nilikuwa sijui kama jamaa ndivyo alivyo kumbe alikuwa anaigiza kumbe maisha yake hayakuwa hivyo, kwa hiyo usijilinganishe na watu wengine, watu wengi ambao wanajilinganisha nao, unawakuta wana struggle kwenye maisha yao, kuna mambo wanaendelea kustruggle kuyapata.

kwa hiyo focus kwenye kitu unachokifanya, focus kwenye maono yako, angali kitu unachopaswa kukifanya , angalia jinsi maisha yako wanavyopaswa kwenda, acha kujilinganisha utajikuta kwenye matatizo makubwa  sana kwenye maisha yako.

Nilishawahi kukutana na mtu mmoja, akawa ananiambia alikuwa na anajilinganisha sana, alikuwa anawatamani sana watu Fulani, lakini siyo kitu kibaya wapo watu ambao wanaishi vizuri lakini mwisho wa siku tunasema lazima urudi kwako wewe mwenyewe kwa sababu yeye mwenyewe anakuja kusema alichokuja kugundua baadae akawa anasema kwa kweli ningekuwa nawajua nisinge watamani wapo ki hivyo.

Kuna watu umekuwa unawatamani wanaendesha magari mazur, unatamani kujifunza vitu vizuri kutoka kwao lakini isifike sehemu ukawa unajiona wewe siyo kitu, hauna maana kwa sababu ya kujilinganisha sana na wengine kwa hiyo cha kwanza acha kujilinganisha badilisha kutoka kwenye kujilinganisha kwenda katika kujifunza, kujifunza alifanya nini akapata alichokipata, alifanya nini au alijifunza nini, au alipita njia gani ili na mimi niweze kupita.

Lakini mtu ambaye anajilinganisha ni Yule anayesema na mimi nataka kuwa kama Fulani bila kujifunza yaliyo nyuma yake.

Unaweza kuwa na furaha kila siku kwa kusoma kitabu kinachoitwa UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA, Kwa sababu kitakufundisha hatua kwa hatua jinsi ya kujijengea tabia zinazoleta furaha.

Kwa sababu ya maombi ya clients wetu,LEO Utakipata kwa bei ya OFA, piga simu namba 0752977170, kupata kitabu chako utaletewa au utatumiwa popote ulipo ndani ya AFRIKA MASHARIKI.

Nb. OFA hii inaisha tarehe 26/6/2021, siku ya JUMAMOSI saa tatu na nusu usiku.

Tuendelee Kujifunza Hapa (www.amkamtanzania.com/vitabu).

2 thoughts on “Unajua Kwanini Wanakosa Furaha?”

  1. Ahsante kwa mafundisho mazuli hakika binafsi nazidi kuji jenga na kuji inua kupitia wewe pia kama ita faa naomba tufundishe na Masomo ya sakolojia Mf: mtu kuji tambua yuko kundi gani?? nini madhaifu yake na imani ita kuwa njia nyepesi ya kuzi kabiri changamoto zetu na kuishi na watu bila mifalakano

Leave a Reply to somavitabu Cancel reply

Your email address will not be published.

Related Post