Nakumbuka ilikuwa ni siku ya jumapili ya mwezi wa 12 mwaka 2020 majira ya saa 9 na nusu alasiri nikiwa kitandani nimejipumzisha…
Gafla Ukaingia Ujumbe Mrefu Kwenye Email Yangu uliokuwa unasomeka Hivi…
Habari za Leo Kocha, Dr. Makirita Amani.
Awali ya yote napenda kukushukuru kwa kazi yako bora ya kuandika kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA na vitabu vyako vingine.
Asante Sana Kocha Kazi Yako Imebadili Maisha
Yangu….
Majina yangu naitwa Mwalimu. Tumaini Ninaishi halmashauri ya mji kahama, Shinyanga. Ni mwajiriwa wa serikali katika Halmashauri ya wilaya MBOGWE-GEITA, Idara ya Elimu Msingi. Pia ni mfanyabiashara wa duka la mahitaji ya nyumbani na Biashara ya kutengeneza na kuuza chaki.
Hakuishia Hapo Tu, Akaendelea Kutoa Ushuhuda…
Maisha Yangu Kabla Ya Kusoma Kitabu Cha Biashara Ndani Ya ajira…
Mwaka 2015 nilihitimu masomo yangu ya ualimu. Nikiwa kwenye furaha sana kwamba ningeenda kupata ajira ambayo ingeyafanya maisha yangu kwenda vizuri.
Maana kwa muda wote toka utotoni hadi kufikia kuhitimu masomo yangu nilikuwa na hadithi nyingi ambazo nilisimuliwa na wazazi wangu na walimu wangu kuhusu uzuri wa ajira.
Ni kweli nilijituma hasa kuhakikisha nafikia lengo hilo la kupata sifa ya kuajiriwa.
Ni kweli kila kitu huwezi kukijua kwa kuangalia kwa wengine tu kuna baadhi ya ukweli huwezi kuujua mpaka uingie ndani.
Mwishoni mwa mwezi Mei 2015 nilipata kazi ya kujitolea kufundisha kwenye kituo cha huduma ya mtoto chini ya shirika la COMPANSSION INTERNATIONAL TANZANIA.
Hili ni shirika linalosaidia watoto wanaoishi maisha magumu na Yatima na kushirikiana na makanisa ya kiinjili.
Nilianza maisha yangu ya kazi huku nikiwa na matarajio makubwa kwamba baada ya miezi michache ningepata ajira serikalini ambapo ndiyo yalikuwa malengo yangu.
Kwa kipindi cha miaka miwili ya kazi nilikuwa nmechoka, nalaumu mwajiri wangu haongezi mshahara na malalamiko mengine mengi.
Gharama za maisha zilikuwa juu na huku nikitegemea chanzo kimoja cha kipato.
Nilikuwa nashindwa kulipa hata kodi ya chumba.
Hapo nilihangaika kufanya Biashara ya mtandao ambayo nilikuwa siijui nikaishia kutapeliwa.
Ni katika hali hiyo ngumu ndipo nikawa natembelea mtandao wa facebook nikitafuta njia mbadala ya kuingiza kipato.
Hapa sasa ndipo MPENYO wangu ulipoingia baada ya kukutana na VIDEO YA KOCHA Dr. MAKIRITA AMANI ikisema Kama Unatumia Smartphone Au Simu Janja Na Hakuna Kipato cha Ziada Unachoingiza Basi Unafanya Makosa Makubwa Sana.
Hapo Ilikuwa Mwaka 2017.
Nikampigia simu na akanipa maelekezo kupata MAFUNZO.
Mwezi june 2017 tarehe 30 nilifanya maamuzi ya kufanyia kazi ushauri wake kwa kulipa ada ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA ili niweze kushiriki semina ya ELIMU YA MSINGI YA FEDHA ni kupitia kushiriki semina hiyo, niliweza kupata fursa ya kununua vitabu vya kocha kwa bei ya ofa kwa ajili kwa kuwa nilikuwa nimeshiriki semina hiyo bora.
Miongoni mwa vitabu hivyo kimoja wapo ni BIASHARA NDANI YA AJIRA.
Ni kupitia kusoma kitabu hicho ndiyo nilipata mwanga mkubwa kuhusu kufanya biashara ukiwa ndani ya Ajira.
Kumbuka kuwa wakati wote huo sikuwa na biashara yoyote na nmetoka familia maskini sana ambayo shughuli kuu ni kilimo cha mkono tena kilimo cha mazoea.
Maarifa ya Kocha yana nguvu sana, nilibadili mtazamo, na kuanza kujiwekea malengo makubwa.
Mambo Niliyojifunza Kwenye Kitabu Cha BIASHARA NDANI YA AJIRA!…
Kwenye kitabu hiki nmejifunza mengi yaliyobadili kabisa mtazamo wangu kuhusu biashara, baadhi ya mambo hayo ni;
- Kuanza Biashara Kwa Sasa ni Rahisi Kuliko Kipindi Cha Nyuma.
- Maamuzi Sahihi Ya Kufanya Kabla Ya Kuacha ajira Na Kuingia Kwenye Ajira.
3. Namna Bora ya Kutumia Muda Wangu Vizuri Niweze Kuanza Biashara Nikiwa Bado Nipo Kwenye ajira.
4. Fursa Kubwa ya Kupata au kuongeza mtaji kwenye Biashara.
5. Uhakika wa Kipato Pale Unapokuwa Unaanza Biashara Ili Kuiacha Biashara Ikue.
6.Madhara ya Chanzo Kimoja cha Kipato.
7. Wakati Sahihi Wa Kuondoka Kwenye Ajira.
8. Biashara Inahitaji Muda Kukua Hivyo Uvumilivu Unahitajika.
9. Ubaya wa Kipato Kimoja.
Hatua Nilizochukua Baada ya Kusoma Kitabu Hiki Cha BIASHARA NDANI YA AJIRA!…
Baada ya kusoma kitabu hiki nilichukua hatua ya kuanza biashara ya kuuza na kununua sabuni za kuogea.
Sababu hizi nilikuwa nazinunua elfu 21 boksi na kuziuza kwa wafanyakazi wenzangu kwa sh 1,500 kwa kila sabuni.
Boksi moja lina idadi ya sabuni 24. Baada ya mauzo nilikuwa Napata sh. 36,000/=.
Hiyo haikutosha nikamwomba mwajiri wangu wa kazi niwe natumia kamera ya ofisini kupiga picha za biashara na nikaweza kuongeza kipato change toka laki 2 hadi laki 5 kwa mwezi.
Ingawa Biashara hizi hazikudumu lakini zilitosha kunionesha ukweli kwamba Biashara ndiyo njia ya uhakika ya kuingiza kipato kisicho na kikomo.
Changamoto Ninazokutana nazo!…
- Kukosa muda wa mapumziko. Hapa unapoanza Biashara huku ukiendelea na Aajira utahitaji kujitoa sana na kuacha mambo mengi uliyokuwa unafanya kabla ya kuwa na Biashara.
- Kutengwa, Baada kuanza Biashara niliacha hadithi za Ajira bora kitu ambacho kilinifanya kutengwa na marafiki zangu.
- Kubezwa, Wafanyakazi wenzangu walikuwa wananicheka kwa kuwa nilikuwa nafanya Biashara ambazo zilionekana kutokuwa na hadhi.
- Maamuzi mabovu ya kuacha Ajira bila maandalizi mwaka 2018. Hii ni moja ya changamoto kubwa katika maisha yangu bila kuwa na msaandalizi bora. Na kwenda kwenye kilimo cha tikiti maji.
- Kukosa mtaji hasa baada ya kuacha Ajira.
- Biashara ya kilimo kushindwa vibaya.
Pamoja na changamoto hizo bado niliamini kwamba lazima nianzishe Biashara.
Kama Waswahili Wanavyosema Penye Nia Pana Njia.
Mafanikio Yangu Kwa Kuanzisha Biashara Huku Nikiendelea Na Ajira!…
Disemba 2018 nilianza Biashara ya duka la mahitaji ya nyumbani na kiwanda kidogo cha chaki.
Karibu mwaka sasa nimeweza kusimamia na kuendesha Biashara hizi mbili tofauti na sasa zinaendelea vizuri. Nimeongeza vyanzo vya KIPATO kutoka kipato kimoja hadi vyanzo vitatu vya kipato.
Nmeajiri watu wawili hadi sasa. Hakika nashukuru Mungu kwa kunikutanisha na Kocha Dr. Makirita Amani. Sehemu Pekee Ya Kutoa Msaada Kwa Maendeleo Ya Jamii ni Kuwa na Biashara.
Mwalimu Tumaini, Akamalizia Kwa Kutoa Ushauri Unaosomeka Hivii…
Ushauri Wangu Kwa Wale Wote Waliopo Kwenye Ajira na Hawana Njia Nyingine Ya Kuwaingizia Kipato!…
Rafiki yangu mpendwa uliyepo kwenye Ajira , kama tunavyojua wote kwamba sasa zama zimebadilika, kutegemea mshahara pekee kama chanzo cha kipato hakuwezi kukufanya uishi maisha yenye uhuru wa kifedha na kuwa na maisha bora kwani kila wakati gharama za maisha zinapanda kila siku na thamani ya fedha inashuka kila mwaka.
Ninachotaka kukushauri ni wewe kuhakikisha unakipata kitabu hiki ili uweze kujionea mengi mazuri yaliyopo kwenye kitabu hiki ya kukusaidia kuanzisha BIASHARA.
Kama Umekuwa Unatamani Kuanzisha Biashara Na Changamoto Mbalimbali Zinakuzuia Kuanza Majibu Yapo Ndani Ya Kitabu Hiki Cha BIASHARA NDANI YA AJIRA.
Sisemi Usome tu Kisha ufurahie Kujifunza Maarifa Haya Bora Pekee Bali CHUKUA HATUA.
Mwalimu Tumaini, Kwenye Barua Yako Akamalizia Kwa Kusema…
“Usipochukua Hatua Hakuna Kitakachobadilika”
Bado Ni OFA Ya Watu 100 Wa Kwanza!…
Wekeza LEO Tsh. 19,999 tu! OKOA 80K.
UEPUKE FEDHEA YA KUDHARAULIKA…
Rafiki Yangu Mpendwa, Wasiliana Nami Kwa Kupiga Simu Namba 0752977170. Ujipate Nakala Yako LEO. UEPUKE FEDHEA YA KUDHARAULIKA…
Kutoka Kwa Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Bwana Rama, Copywriter Wa SOMA VITABU TANZANIA.
0752977170.