100% Jinsi Ya Kusoma na Kukumbuka Kitabu chochote Kile Ndani Ya Masaa 24 TU!…

100% JINSI YA KUSOMA NA KUKUMBUKA KITABU CHOCHOTE KILE NDANI YA MASAA 24 TU!…

Rafiki Yangu Msomaji,

Je umewahi kusoma kitabu lakini muda mfupi baadaye ukasahau kabisa yale uliyosoma?

Jibu ni ndiyo na siyo kwa sababu wewe ni msahaulifu sana, bali kwa sababu ndivyo binadamu tulivyo.

Tafiti zinaonesha huwa tunasahau nusu ya vitu tulivyosona saa moja baada ya kusoma.

Na tunasahau karibu robo tatu baada ya siku moja.

Hilo linatokea kwa sababu akili zetu huwa zinapokea taarifa nyingi kila wakati, inazichuja na kubakisha zile muhimu huku zikisahau zisizokuwa muhimu.

Unasahau vitu unavyosoma kwa sababu hujaifanya akili yako ione ni vitu muhimu vinavyopaswa kukumbukwa.

Ili kukumbuka yale unayosoma, kuna mambo sita ambayo mwandishi ametushitikisha.

Tumia Kanuni Hii Ya Ufupisho itakusaidia kukumbuka kile ulichojifunza…

Inaitwa FASTER ambapo ni kifupisho cha maneno Forget, Act, State, Teach, Enter, Review.

1. Sahau (Forget)

Kabla hujaanza kusoma, kuna vitu vitatu unapaswa kuvisahau.

Kwanza sahau yale unayodhani tayari unajua kuhusu kitu unachosoma. Soma ukichukulia ni kitu kipya

ambacho hukijui kabisa.

Mbili sahau usumbufu unaojaza akili yako, chochote kinachokupa wasiwasi au mawazo kiweke

pembeni ili akili iweke umakini kwenye kile unachosoma.

Tatu sahau ukomo ambao umekuwa unajiwekea, ona lolote lile linawezekana na hapo utasoma kwa

uhuru na kukubali.

2. Chukua hatua (Act)

Usisome kama darasani, ambapo unakaa na kusikiliza tu. Kujifunza kwa aina hiyo huwa kunachosha

na ndiyo maana watu hukosa umakini na kusinzia.

Unaposoma, chukua hatua mbalimbali. Andika vitu unavyojifunza, fanya mazoezi ya kile unachojifunza.

Kwa namna yoyote ile, chukua hatua kwenye kile unachojifunza, unakumbuka zaidi kwa kufanya.

3. Hisia (State)

Uelewa wako kwenye kile unachosoma unategemea sana hisia unazokuwa nazo.

Mambo yote unayokumbuka mpaka sasa ni kwa sababu ulijifunza ukiwa kwenye hisia fulani, iwe ni furaha au hamasa ya hali ya juu.

Jenga hisia chanya katika kile unachojifunza, kuwa na furaha, matumaini na hamasa kubwa kwenye kile unachojifunza.

Hisia hizo zitafanya uweke umakini zaidi na kukumbuka kwa muda mrefu.

4. Fundisha (Teach)

Unapojua kwamba utawafundisha wengine kile unachojifunza, unajifunza kwa umakini na kuelewa zaidi.

Kwa kila unachojifunza, chagua kuwafundisha wengine.

Hilo litabadili sana namna unavyojifunza.

5. Weka kwenye ratiba (Enter)

Huwezi kupata muda wa kujifunza kama huupangi kabisa kwenye ratiba yako.

Kila unapoianza wiki yako, pangilia kabisa muda wa wewe kujifunza kupitia usomaji wa vitabu.

Kila unapoianza siku yako, tenga muda ambao utakuwa tulivu na kujisomea.

Usijiambia ukipata muda utasoma kitabu, bali panga muda wa kusoma na tekeleza kama ulivyopanga.

Kwa kujifunza mara kwa mara utakumbuka yale unayojifunza.

6. Marejeo (Review)

Kila unapomaliza kusoma, fanya marejeo ya yale uliyojifunza katika kusoma huko.

 Jikumbushe yote uliyojifunza na kuondoka nayo katika kusoma kwako. Zoezi hilo linaifanya akili ione ni muhimu na kukumbuka hayo uliyorejea.

Na pia unapofika wakati mwingine wa kusoma, jikumbushe yale uliyojifunza wakati uliopita.

Zoezi hilo linazidi kukomaza kumbukumbu zako kwenye yale uliyojifunza.

Kwa kuchukua hatua hizi sita, utaweza kujifunza kwa kina na kuyakumbuka yale uliyojifunza kwa muda mrefu.

Uliza maswali sahihi.

Umewahi kugundua hili, ukijiuliza swali, unashangaa majibu yakijitokeza kila mahali.

Mfano ukijiuliza kwa nini watu wamevaa nguo nyekundu leo?

 Ghafla unaona nguo nyekundu kila mahali.

Siyo kwamba nguo hizo nyekundu zimetokea kwa wewe kuuliza, zilikuwepo muda wote, ila akili yako ilipuuza kwa sababu hakikuwa kitu muhimu.

Ulipoanza kuuliza hilo swali, akili yako ikajua ni kitu muhimu na hivyo kuweka umakini kwenye hilo.

Ndiyo maana ghafla umeanza kuona kile ulichouliza.

Hii inatuonesha jinsi akili yetu ilivyo na uwezo mkubwa wa kuleta kwetu kile tunachotaka.

Muhimu ni sisi kuuliza maswali sahihi.

Mara zote iulize akili yako utapataje kile unachotaka au utayafikiaje malengo yako.

Jiulize maswali chanya na akili yako itakuonesha fursa za kupata unachotaka au kufika unakotaka.

Maswali ya kujiuliza unapojifunza.

Unapojifunza kitu chochote kipya, jiulize maswali haya matatu;

Nawezaje kutumia hiki nilichojifunza?

Kwa nini nitumie hiki nilichojifunza?

Wakati gani nitumie hili nilichojifunza?

Maswali haya matatu yatakuonesha namna sahihi ya kunufaika na kila unachojifunza.

Hata hivyo leo unaweza kuanza kutumia kanuni hii rahisi kwa kusoma kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI, ili uweze kujitengenezea uhuru wako na kuweza kujitofautisha na viumbe wengine.

Na KWA SABABU Tunakupenda Sana, LEO Utawekeza Tshs 14,999TU! Badala Ya Tshs 20,000.

Ina maana leo utaongeza ubunifu wako na  ufanisi wako kazini kwa Tshs 14,999Tu!

Unachotakiwa kufanya sasa hivi ni kupiga namba hii 0752977170 bila kuchelewa kwa sababu  VIMEBAKI VITABU 19 TU! Na kimoja Tayari Kuwekewa ODA.

KUMBUKA; Hivi 18 vikiisha itabidi usubiri mpaka mwakani tena pale tutakapochapisha vingine.

Nikusii Rafiki Yangu UHURU WAKO UPO MKONONI MWAKO, na huwezi kuupata mpaka upate maarifa sahii na uchukue hatua.

Na kama bado hujapata zawadi yako ya KUKUZA BIASHARA  bonyeza hii link https://somavitabu.co.tz/zawadi/ .

Karibu 0752977170.

Nakupenda.

Kutoka Kwa Shabiki Yako Namba 1 Tanzania,

AmryRamadhani|CopywriterOfSomaVitabuTanzania|

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post