Acha Kujilinganisha Na Wengine Chukua Hatua Sasa.

Mitandao ya kijamii ambayo ni moja ya njia kuu ya kusambaza habari imechochea sana kuongezeka kwa msongo wa mawazo kwa watu wengi.

Hii ni kwasababu mitandao hiyo imekuwa inawachochea watu kuweka maisha yao kwenye mitandao hiyo.

Sasa kwa kuwa ni tabia yetu binadamu kupenda kuonesha mambo yetu ni mazuri kuliko yalivyo , watu wengi huweka maisha ambayo siyo halisi.

Mfano mtu anaweza kuwa na changamoto nyingi kwenye maisha yake , lakini akachagua kuweka picha nzuri za wakati ana furaha kwenye mitandao ya kijamii.

 Mtu mwingine kwa kuona wenzake kila wakati anaweka picha nzuri akiwa na furaha na maeneo ya kifahari , anaona mtu huyo ana maisha mazuri kuliko yeye.

Hali hiyo ya kujilinganisha imekuwa chanzo cha msongo wa mawazo kwa wengine.

Kibaya zaidi ni kwamba ulinganisho ambao mtu anafanya siyo sahihi , maisha ambayo watu wanayaweka mitandaoni ni tofauti kabisa na maisha yao halisi.

Imegundulika chanzo cha ulinganisho huo ni matumizi ya teknolojia mpya hasa hasa mitandao ya kijamii.

Na kwa kuwa teknolojia hizi ni mpya, hakuna mwenye uzoefu wa jinsi ya kukabiliana nazo, hivyo watu wanaingia kwenye teknolojia hizo mpya kwa kuhadaiwa watanufaika sana, lakini kinachotokea ni wanageuzwa kuwa wafungwa.

Leo nina habari njema kwako, habari hizo ni kupatikana kwa mwongozo wa kuzitumia teknolojia hizi mpya vizuri na ukombozi wa ufungwa ambao teknolojia hizo zimetengeneza kwako.

Nimekuandalia kitabu kinachoitwa EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI, kitabu kinachokuonesha jinsi teknolojia mpya zinavyokufanya mtumwa na njia za kuondoka kwenye utumwa huo.

Kupitia kitabu hiki utajifunza mambo saba makubwa ambayo yatakufanya uwe huru na utumie teknolojia hizi kwa manufaa makubwa kwako.

Moja utajifunza jinsi ubongo wako unavyofanya kazi na namna teknolojia mpya zinavyotumia ubongo huo kukufanya kuwa mtumwa.

Teknolojia mpya zimetengenezwa kwa namna ambayo zitajenga uteja/uraibu kwenye ubongo wako. Kwa kujua njia hiyo utaweza kuepuka kuingia kwenye utumwa wa teknolojia hizo.

Mbili utajifunza kuhusu zama tunazoishi sasa, zama za maarifa na taarifa lakini ambazo zimegeuka kuwa zama za usumbufu.

Utajifunza zama hizi za usumbufu zimetengeneza makundi makubwa mawili, wachache wanaonufaika sana, kama Mark Zuckerberg ambaye ni mmiliki wa Facebook na wengi ambao ni kama watumwa wa wachache hao wanaonufaika.

Tatu utajifunza jinsi ya kujua kama tayari umeshanasa na kuwa mtumwa wa teknolojia hizo mpya. Unaposoma hapa unaweza kusema wewe hujawa mtumwa, unatumia kwa kupanga mwenyewe, lakini nikuambie kitu kimoja, kwa sehemu kubwa sana umeshakuwa na utaziona dalili kwa kusoma kitabu hiki.

Nne utajifunza jinsi ya kuondoka kwenye utumwa wa kidijitali ambao umeshaingia.

Baada ya kuona jinsi ambavyo umenasa kwenye utumwa huo, utajifunza njia za kujinasua. Hapa utajifunza jinsi ya kuizidi ujanja simu janja yako.

Tano utajifunza falsafa mpya ya kuendesha maisha yako kwa uhuru katika zama hizi za usumbufu. Pamoja na kujifunza kuhusu zama hizo na jinsi ya kuondokana na utumwa wake, usumbufu wake hautaisha, teknolojia mpya zinaendelea kugunduliwa kila siku na zikiwa na ushawishi mkubwa.

Hivyo unahitaji kuwa na falsafa unayoitumia kuchagua huduma za kidijitali utakazochagua kutumia kwa manufaa yako.

Sita utajifunza jinsi ya kutumia akili yako kuvunja uraibu wowote ambao umeshajijengea. Kama tulivyoona, huduma za kidijitali zinatumia jinsi ubongo unavyofanya kazi kukuingiza kwenye utumwa. Hivyo wewe unapaswa kuutumia ubongo wako vizuri kuondoka kwenye utumwa huo.

Saba utajifunza sababu kumi kwa nini unapaswa kuondoka kwenye mitandao yote ya kijamii sasa hivi. Hizi ni sababu ambazo zimechambua jinsi matumizi ya mitandao ya kijamii yalivyo na athari kwenye akili yako, utulivu wako, mahusiano yako, uchumi wako na hata imani yako.

 Kwa kuzijua sababu hizi kumi, utajionea mwenyewe jinsi ulivyorudi nyuma tangu umeanza kutumia mitandao hiyo na hivyo kuachana nayo ili kuepuka madhara yake.

Mwisho kabisa utajifunza njia za kutumia kufanya maamuzi iwapo utumie huduma ya kidijitali. Utajifunza jinsi ya kutumia vigezo vitatu vya AFYA, UTAJIRI na HEKIMA katika kuchagua na kutumia teknolojia mpya, ambazo zitakuwa na manufaa kwako badala ya kukufanya mtumwa.

Tuko kwenye vita, adui mkuu anajua yuko vitani ila wanaolengwa hawajui.

Hivyo unapaswa kuwa na maandalizi mazuri ya kupambana na vita hii ili uweze kutoka salama na siyo kuwa mfungwa.

Pata na usome kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI ili upate mbinu za kupambana kwenye vita hii na kutoka ukiwa mshindi. Kitabu hiki kimechapwa kwa nakala ngumu (hardcopy).

Kitabu kinauzwa tsh elfu 20 (20,000/=) na ili kukipata wasiliana na 0752 977 170 na utaletewa au kutumiwa kitabu popote ulipo Tanzania na Afrika Mashariki.

MUHIMU; Kama utanunua na kusoma kitabu hiki na ukaona hakina manufaa yoyote kwako, unaruhusiwa kukirudisha na ukarejeshewa fedha zako. Hivyo chukua hatua sasa, huna cha kupoteza lakini una mengi ya kupata, yatakayokuweka huru kwenye zama tunazoishi sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post