Nenda shule, soma kwa bidii na ufaulu vizuri.
Utapata kazi inayokulipa vizuri na utakuwa na maisha mazuri.
Huu ulikuwa ushauri maarufu na uliofanya kazi kwenye karne ya 20 na muongo wa kwanza wa karne ya 21.
Lakini sasa mambo yamebadilika kabisa,
Waliofuata ushauri huo ni wengi, wameenda shule, wamesoma kwa bidii,
Wakahitimu na ufaulu mkubwa, lakini kazi hakuna.
Karne ya 21 imekuwa na mapinduzi makubwa ya kiteknolojia kiasi kwamba nafasi za kazi ni chache kuliko wahitaji wanaozitaka nafasi hizo.
Hivyo licha ya juhudi mbalimbali zinazofanyika na serikali mbalimbali duniani,
Bado tatizo la kukosekana kwa ajira linaendelea kukua kila siku.
Pamoja na tatizo la kukosekana kwa ajira kuwepo,
Bado ushauri unaendelea na vyuo vinaendelea kuzalisha wahitimu anaotegemea kupata ajira.
Wanafunzi wanapohitimu na kukaa mtaani kutafuta kazi bila mafanikio,
Wanapewa ushauri mwingine ambao unawachanganya zaidi.
Wanaambiwa usisubiri tu kuajiriwa,
Jiajiri mwenyewe, anzisha biashara.
Hapo ndipo wanachanganyikiwa zaidi,
Mtu amekaa darasani kwa zaidi ya miaka 15 na miaka yote hiyo alikuwa anafundishwa kuja kuwa mwajiriwa.
Halafu amehitimu anaambiwa ajiajiri?
Mtu hana maandalizi yoyote katika kujiajiri au kuanzisha biashara,
Hivyo hata pale wanaposaidiwa mtaji wa kuanza biashara,
zinaishia kufa.
Ukweli ni kwamba, ushauri wa karne ya 20 haufanyi tena kazi kwenye karne ya 21 na watu hawajaandaliwa kukabiliana na mabadiliko haya.
Njia ya uhakika kabisa ya kuingiza kipato kwenye karne hii ya 21 ni kufanya biashara.
Njia hii haina ukomo kwenye ukuaji au kipato,
Lakini siyo njia rahisi ambayo mtu atafanikiwa kwa kuambiwa tu mara moja.
Unahitaji kupata mafunzo sahihi ndiyo uweze kufanikiwa kwenye kuanzisha na kukuza biashara inayokupa kipato kisicho na ukomo na pia kukupa uhuru wako.
Miaka 15 uliyokaa darasani, haikukufundisha hilo.
Lakini una bahati, kuna njia ya kujifunza yale ya msingi kabisa kuhusu biashara kwa njia rahisi,
Huku ukielewa na kuwa na hatua za kuchukua.
Njia hiyo ni kupitia kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA,
Hiki ni kitabu ambacho kinakufundisha kwa kina yale yote ya msingi unayopaswa kuyajua katika kuanzisha na kukuza biashara yako.
Na yale ya msingi kabisa ni;
Jinsi ya kupata wazo bora la biashara na la kipekee kwako, wazo ambalo halitakuwa na ushindani kutoka kwa wengine.
Jinsi ya kuandaa mchanganuo wa biashara yako,
Ambayo ndiyo ramani muhimu kwako kufanikiwa kibiashara.
Aina za mtaji unaohitaji kwenye biashara na jinsi ya kupata mtaji wa kuanza biashara.
Jinsi ya kuirasimisha biashara yako ili uifanye kisheria,
Kusajili jina la biashara au kampuni,
Kupata leseni na kulipa kodi sahihi kwa biashara yako.
Jinsi ya kutengeneza na kutoa thamani kwenye biashara yako na kutengeneza faida zaidi.
Mbinu za masoko na mauzo,
Kuweza kuwafika wateja wapya na kuwashawishi kununua unachouza.
Kujua mzunguko wa fedha kwenye biashara yako na jinsi ya kujilipa kutoka kwenye biashara hiyo.
Jinsi ya kutoa huduma bora kwa wateja ulionao kwenye biashara yako ili walete wateja wengi zaidi.
Changamoto zinazoua biashara nyingi na jinsi ya kuepusha biashara yako isife kwa changamoto hizo.
Hitaji la mafunzo kwako na wafanyakazi wa biashara yako ili iweze kukua zaidi,
Maana biashara haiwezi kukua kama wanaoifanya hawakui.
Yote hayo, unajifunza kwa kina na kujua hatua za kuchukua kwa kusoma kitabu kinachoitwa ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA.
Haijalishi umesomea nini au una kazi ya aina gani,
Karne ya 21 ni karne ambayo njia kuu ya kuingiza kipato siyo ajira tena bali biashara.
Hivyo iwe una kazi au huna, biashara ni muhimu uwe nayo.
Na kama tayari uko kwenye biashara, huenda unaifanya tu kwa mazoea,
Ni wakati sasa wa kupata msingi sahihi utakaokuwezesha kuifanya biashara hiyo kwa mafanikio makubwa,
Ili uongeze kipato chako na uwe huru zaidi.
Jipatie leo nakala yako ya kitabu cha ELIMU YA BIASHARA ili uweze kwenda na kasi hii ya karne ya 21.
Kitabu kinauzwa tsh elfu 20 (20,000/=) na ili kukipata wasiliana na 0752 977 170 na utaletewa au kutumiwa kitabu popote ulipo Tanzania na Afrika Mashariki.
MUHIMU; Kama utanunua na kusoma kitabu hiki na ukaona hakina manufaa yoyote kwako,
Unaruhusiwa kukirudisha na ukarejeshewa fedha zako.
Hivyo chukua hatua sasa, huna cha kupoteza lakini una mengi ya kupata.