Siku Ya Wapendanao; Utaacha Kuogopa Na Utaanza Kufurahia Maisha Yako…

Soma Vitabu, [2/14/2023 6:12 AM]
SIKU YA WAPENDANAO;  Utaacha Kuogopa Na Utaanza Kufurahia Maisha Yako Sasahivi …

Rafiki Yangu,

Je mpaka sasa unahofu na yajao?

Ikiwa mpaka sasa unahofu na yajao sikufichi unaendelea kuyapoteza maisha yako,

Kwasababu hauna umiliki wa kesho yako, wakati ulionao ni sasa hivi nasio kesho wala kesho kutwa.

Mara nyingi umekuwa unakosa AMANI  kwasababu ya kuhofia yajao.

Najua una ndoto kubwa sana, lakini ukiangalia na kufikiria juu ya ndoto yako unaona nikama bado upo usingizini.

Wala hata usiwe na usiwe ni hali ya kawaida sana, ambayo hata mashujaa wengi wakubwa kama Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere, nelson Mandela , obama n.k walishaipitia na wakaibuka washindi.

Hivyo kama kuna kitu umepanga kukifanya leo , basi kifanye leo leo usisubiri kesho kwasababu ukingoja kesho utakuwa umechelewa.

Na kama utakuwa msikivu na mvumilivu basi nakuahidi dakika moja ijayo utaacha kuogopa na utaanza kuyafurahia maisha yako.

Na Leo utajifunza kupitia huyu MFANYABIASHARA MKUBWA,

Hii ilitokea Mwaka 2003 Nairobi Kenya,
Huyu mfanyabiashara alipambana sana usiku na mchana kuhakikisha anaingiza pesa nyingi sana kwaajili yake na familia yake.

Siku mmoja akiwa ofisini kwake alimuita mhasibu wake na akampa majukumu mawili ,

1.  Ampigie hesabu za fedha zote anazomiliki sasa,

2.  Hesabu atakazopata amwambie je zitamtosha yeye na familia yake miaka 10 ijayo ikitokea hatafanya kazi tena.

Baada ya kupita wiki moja Mhasibu alirudi na majibu na cha kusikitisha zaidi majibu yalikuwa tofauti na MFANYABIASHARA alivyo tegemea,

Majibu yalikuwa ni KIASI CHA FEDHA UNACHOMILIKI SASA HAKIWEZI KUKUFIKISHA MIAKA 10 IJAYO,

Na kwakua MFANYABIASHARA alikuwa anajiamini sana, na kwa nje alionekana ni mtu aliyefanikiwa sana pale mtaani kwao.

Aliheshimika sana, LAKINI baada ya kujua uhalisi ulivyo, kuanzia hapo akawa ni mtu wa kufikiria sana,

KUHUSU MIAKA 10 IJAYO, na hali hiyo ilimuogopesha sana akajawa na hofu mwisho wa siku akawa ni mtu wa KUUMWA UMWA.

Akienda kuchukua vipimo majibu yanakuja HANA UGONJWA WOWOTE,

Kwahiyo akaendelea kuumwa ugonjwa usiojulikana,

…baada ya muda kupita rafiki yake wa siku nyingi alipata taarifa akaenda kumuona ,

Huku akimuomba amwambie kilichomsababishia hali hiyo,

Basi bana MFANYABIASHARA akafunguka mwanzo mwisho,

Ndipo hapo Rafiki yake akagundua tatizo linalomsibu,

Alimuonea huruma sana,

Na kwakuwa anampenda akamuondoa wasiwasi na akamshauri chakufanya ili kutoka kwenye hali hiyo,

Na akampa habari njema kwamba kuna MZEE MWENYE HEKIMA AMEKUJA KUWATEMBELEA,

…na atakaa kwa siku 5 TU!

Akaendelea kumwambia…

Ni Mzee Mwenye Hekima sana endapo utampelekea chakula tu basi atakusaidia kutatua changamoto zako.

Siku iliyofuata Alfajiri Mfanyabiashara akaenda kumtembelea akiwa na vyakula vyingi,

Lakini Mzee Mwenye Hekima hakujali kabisa kuhusu vyakula vyingi alivyoletewa,

Zaidi ya kumkaribisha na kumwambia amechelewa kuleta chakula na kuna mtu tayari ameshaleta chakula,

…hivyo afanye kurudi navyo,

Na kwakuwa alichokuwa anahitaji wakati huo ni kupata suluhisho la changamoto zake, akawa mpole na mdogo kama piritoni.

Mzee akasimamia msimamo wake hatopokea chakula chake, na hanaga utaratibu wa kupokea vyakula viwili ndani ya siku moja,

Mfanyabiashara akamwambia basi atamuachia ili akihifadhi kwaajili ya kesho,

MZEE akasema hapana,
SIIOGOPI KESHO, SIIOGOPI KESHO.

Akaendelea kumwambia leo ni yetu, kesho tutaikabili ,

…hivyo kesho tutaikabili kwa jinsi itakavyokuja.
Maneno hayo yalimshangaza sana Mfanyabiashara,

Mfanyabiashara akamuuliza HUOGOPI KESHO HAKATI KESHO HAUTAKUWA NA CHAKULA?

Mzee akatabasamu,
Na kumwambia Mungu Aliyekupa Chakula Leo , Basi Atakupa Chakula Na Kesho,

…hivyo ninaiishi sasahivi, na siiogopi kesho.
Baada ya Mfanyabiashara kuambiwa maneno hayo,

Alijiona mpumbavu sana,

Akajiuliza kimoyo moyo inakuwaje mtu ambaye hajui kesho atakula nini na bado haogopi vipi kuhusu mimi ambaye ninaogopa miaka 10 ijayo,

Ndipo hapo Mfanyabiashara akaelewa kwamba hapaswi kushindwa kushukuru na kufurahia maisha sasa kwa kuyaogopa mambo ya miaka 10 ijayo.

Kwahiyo Unajifunza Kwamba;

Soma Vitabu, [2/14/2023 6:12 AM]
Pamoja Na Kuwa Na Ndoto Kubwa Unazozipigania Haupaswi Kuiogopa Kesho Yako,

…Licha Ya Changamoto Unazopitia,

…Hivyo Unapaswa Kuiishi Leo Kwa Ukamilifu Wake Huku Ukifurahia Hatua Ndogo Ndogo Unazopiga Kila Siku.

Muhimu Ni Kushukuru Kwa Hatua Ndogo Ndogo Unazopiga Kila Siku.

Rafiki Yangu,
Ikiwa lile lengo lako la KUONGEZA KIPATO CHAKO MARA 4 ZAIDI MWAKA HUU 2023,

Unalo Basi Nakushauri Usiache Kukisoma Kila Siku Kitabu Hiki Cha CHUO CHA MAUZO,
…na kama bado hujakipata, basi usiwe na wasiwasi tuwasiliane kwa namba hii 0752977170,

Piga Simu Sasahivi 0752977170,

Utakipata Kwa AFUU (29,999)Tu Badala Ya Thamani Yake Halisi AFUU 50.

Na Utaletewa Au Utatumiwa Popote Ulipo Ndani Ya AFRIKA MASHARIKI.

NA KWASABABU LEO NI SIKU YA WAPENDANAO,
Nitakuzawadia Na Kitabu Hiki Cha WEWE NI MSHINDI

KUMBUKA; Hii OFA ITAISHA TAREHE 15|03|2023 SAA 4 USIKU.

Imetoka Kwa Rafiki Yako Anayekukubali Sana,

Bwana Amiri Ramadhani

|CopywriterOfSomaVitabuTanzania||MjasiriamaliMjanja|

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post