9/10 Ukianza Kwa Kubadili Hiki Utakuwa Mtu Mwenye Ushawishi Mkubwa Sana.
Rafiki Yangu Mkubwa,
Ondoka Na Hii,
Ukiona bado hujafanikiwa ujue bado hujajua kuuza vizuri.
Ukiweza kuziishi hizi falsafa 5 basi utakuwa mtu mwenye ushawishi mkubwa sana.
Kwasababu kila kitu kwenye maisha huwa kina falsafa ambazo zinakiongoza.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye mauzo, kuna falsafa ambazo zinaongoza mauzo, ambazo mtu akizijua na akawa na mtazamo sahihi, ataweza kufanya mauzo makubwa.
Falsafa ndiyo inayojenga mtazamo ambao mtu anakuwa nao.
Mtazamo ni imani kuu ambazo mtu anakuwa nazo juu ya kitu fulani.
Mtazamo anaokuwa nao mtu ndiyo unaoathiri fikra anazokuwa nazo, fikra zinaathiri maamuzi ambayo yanaathiri matendo na hatimaye kuzalisha matokeo.
Matokeo ambayo mtu anapata ndiyo yanajenga maisha yake.
Hivyo kama unataka kubadili maisha yako, angalia matokeo unayoyapata.
Kama huyafurahii, angalia hatua unazochukua.
Kama huzifurahii angalia mtazamo ulionao na kama siyo mtazamo mzuri basi nenda kwenye falsafa uliyonayo.
Watu wengi wamekuwa wanahangaika kubadili maisha yao kwenye matokeo na wanaishia kubaki pale walipo.
Mabadiliko ya kweli na ya kudumu hayaanzii kwenye matokeo ya mwisho, bali yanaanzia kwenye mzizi mkuu ambao ni falsafa na mtazamo.
Huwezi kuyabadili maisha yako kama hutabadili falsafa na mtazamo ulionayo juu ya maisha na mafanikio.
Falsafa Tano (5) Muhimu Za Kujijengea Kwenye Mauzo.
Kuna falsafa nyingi ambazo zimekuwa zinatumika kwenye mauzo.
Hapa tunakwenda kujifunza falsafa tano ambazo tukizielewa na kuzifanyia kazi tutaweza kukaa vizuri kwenye mchakato wa mauzo na kuuza zaidi.
(1): Watu Hawapendi Kuuziwa, Bali Wanapenda Kununua.
Hii ndiyo falsafa ya kwanza na muhimu kuelewa ili uweze kufanikiwa kwenye mauzo.
Watu hawanunui kwa sababu wewe unauza, bali wananunua kwa sababu ya mahitaji yao binafsi.
Kwa lugha nyingine tunaweza kusema inapokuja kwenye kununua, watu ni wabinafsi.
Unaweza kuwa una uhitaji wa fedha sana, lakini watu hawatajali hilo na kununua unachouza.
Wajibu wako kama mtu wa mauzo ni kutengeneza mazingira yanayowafanya watu wapende kununua kwako.
Unatengeneza mazingira hayo kwa kugusa maslahi na mahitaji ya wateja unaowalenga na kisha kuwafanya waone wanachagua kununua wenyewe na siyo wewe unawalazimisha kununua.
(2): Wajali Wateja Wako Nao Wataijali Biashara Yako.
Kwa asili sisi binadamu ni wabinafsi, tunajali zaidi maslahi yetu kuliko ya wengine.
Unaweza kutumia tabia hii ya ubinafsi kuuza zaidi, kwa kuyaweka mbele maslahi ya wateja kabla ya maslahi yako.
Ukijali sana kuhusu wateja wako, ukayajua maslahi yao na kuwasaidia kuyatimiza, ukawapa thamani kubwa kuliko gharama wanayolipia,
…wateja hao watakulipa kwa kuijali biashara yako.
Watakuwa wateja waaminifu kwako, watanunua kwa wingi, kwa muda mrefu na pia watawaleta wengine nao wanunue.
Karibu Sana,
Rafiki Yangu, Namba Zilizobaki Ndizo Zitakazo Kuza Mauzo Yako Mpaka Ushukuru.
Namba Hizi Ni Namba 3, Namba 4 na Namba 5 Utazikuta Sura Ya Kwanza Ya Kitabu Hiki Kipya Cha * CHUO CHA MAUZO*
Kupata Kitabu Hiki Kipya Piga Simu 0752977170.
Utaletewa au Utatumiwa Popote Ulipo Ndani Ya Mipaka Ya AFRIKA MASHARIKI.
Kutoka Kwa Rafiki Yako, Anayekupenda Na Kukujali Sana.
Bwana AmiriRamadhani |CopywriterOfSomaVitabuTanzania| |Mjasiriamali Mjanja|