Biashara Inayolipa Kwa Sasa.

Hii ndiyo biashara itakayokupa faida ya kudumu.

Nina mtaji wa fedha kiasi Fulani, lakini sijui ni biashara gani nifanye?

Hili ni swali ambalo linaulizwa na watu wengi. Karibu kila mtu anayeingia kwenye biashara huwa anauliza swali hili.

Swali jingine maarufu ni Biashara ninayofanya hainilipi vizuri, ni biashara gani nzuri ninayoweza kufanya?

Hili ni swali ambalo linaulizwa na watu ambao tayari wapo kwenye biashara.

Japokuwa tunapenda mtu atuambie ni biashara gani yenye faida tunayoweza kufanya na sisi tuanze tu kuifanya, hakuna biashara moja ambayo inaweza kuwa nzuri kwa watu wote.

Watu tunatofautiana, mtu mmoja kufanikiwa , haimaanishi kila mtu ataweza kufanikiwa, haimaanishi na wewe pia ukiingia kwenye biashara hiyo utafanikiwa kama wengine walivyofanikiwa.

Biashara Fulani kuwa inafanya vizuri na watu wengi kuifanya, ni kielelezo kizuri kwamba katika eneo hilo ambalo biashara hiyo inafanywa kuna soko la biashara hiyo.

Lakini haikuhakikishii kwamba na wewe ukiingia kwenye biashara hiyo utafanya vizuri.

Kwa sababu kwa asili, binadamu hatupendi kuumiza akili zetu, watu wengi hukimbilia kufanya biashara ambayo inaonekana kuwa na faida kwa wengi.

Jambo la kushangaza ni pale ambapo wengi wanaoingia kwenye biashara hii wanashindwa kupata mafanikio na wengine wanaishia kushindwa kabisa.

Hakuna biashara ambayo ni sahihi kwa kila mtu kuifanya na kama akiweza kuingia tu kwenye biashara hiyo basi mafanikio kwake ni laima.

Ingekuwa kuna biashara ya aina hiyo, tusingeona matatizo ambayo watu wanayopitia sasa kwenye biashara zao.

Mtu angekazana apate mtaji kwa njia yoyote na kuingia kwenye biashara hiyo ambayo ni ya uhakika.

Kwa sababu hakuna biashara hii ambayo ni sahihi kwa wote, kila mtu ana biashara ambayo ni sahihi kwake.

Je wewe ni biashara gani sahihi kwako kufanya?

Unahitaji kuijua ili upeleke nguvu na juhudi zako huko na uweze kufikia mafanikio makubwa kupitia biashara.

Biashara ambayo ni sahihi kwako kufanya ni ile biashara ambayo inatokana na kitu unachokipenda au unachokijua vizuri.

Kwa kufanya biashara inayotokana na kitu unachopenda au unachojua, kunakupa nafasi ya wewe kufurahia biashara hiyo, kuwa na shauku ya kuweka juhudi na ubunifu zaidi na kuwa na hamasa ya kuleta mabadiliko.

Ni aina hii ya biashara ambayo itakufanya uendeshe biashara yako sio kwa mazoea ila kuangalia mahitaji na kuangalia unapoweza kuboresha zaidi.

Katika biashara ya aina hii unaweza kuifanya hata kama haikupi faida kwa sababu unajisikia kuna kitu kikubwa ambacho unatakiwa kukitoa kwa wengine.

Unaona kile ambacho unafanya sio kutoa tu huduma au biashara kwa wengine kwa sababu watakupatia fedha ila pia unafanya hivyo kwa sababu unajua kupitia bidhaa au huduma unayotoa, kuna watu wengi ambao matatizo yao yanatatuliwa.

Kwa upande mwingine unapoingia kwenye biashara kwa sababu tu itakupatia faida, una nafasi kubwa sana ya kushindwa au kukimbia.

Hii ni kwa sababu hakuna biashara inayokwenda kama mipango yake ilivyowekwa.

Kuna nyakati ambazo utakutana na changamoto nyingi zinazoweza kuleta msukosuko mkubwa kwenye biashara hiyo.

Sasa kama kilichokusukuma wewe ni faida tu, utakuwa tayari kukimbia ili kuokoa fedha zako au kutafuta biashara nyingine ambayo itakupatia faida unayohitaji.

Unapokuwa kwenye biashara unayoipenda au ambayo inahusika na kitu unachokijua , wakati kama huo unautumia kujifunza zaidi na kufanya mabadiliko kwenye baadhi ya maeneo ambayo huenda hufanyi vizuri.

Unapovuka changamoto za aina hii unakuwa bora sana na ndio unakuwa mwanzo wa wewe kufikia mafanikio makubwa.

Watu wengi wamekuwa wakihama hama biashara na mwishowe kushindwa kuona mafanikio halisi waliyoyapata kupitia biashara.

Hii inatokana na wao kutokujua biashara sahihi kwako kufanya na hivyo kupoteza muda mwingi kwenye biashara ambazo sio sahihi kwao.

Jinsi unavyojua mapema biashara sahihi kwako kufanya ndivyo inavyokuwezesha kufikia mafanikio kupitia biashara hiyo mapema.

Hii ni kwa sababu mafanikio yoyote yanahitaji muda, hivyo ukijua mapema utaweka juhudi mapema na utaanza kuyavuna matunda mapema pia.

Ila unapochelewa kujua biashara sahihi kwako unazidi kupoteza muda na hivyo kushindwa kufikia mafanikio makubwa kupitia biashara.

Hakuna biashara moja sahihi kwa kila mtu kufanya, ila kuna biashara sahihi kwa mtu fulani kufanya.

Biashara sahihi kwako kufanya ni ile inayotokana na vitu ambavyo unavipenda na pia unavijua au una uzoefu navyo.

Na pia biashara hii unakuwa tayari kuifanya hata kama hupati faida kubwa hasa mwanzoni.

Kama tayari nipo kwenye biashara na naona sio sahihi kwangu ndio matumaini yangu yameishia hapo?

Jibu ni hapana, bado una matumaini makubwa sana kwenye biashara hiyo.

Ila utahitaji kufanya mabadiliko makubwa kwa sasa ili uweze kubadili mtazamo wako kwenye biashara hiyo, kuibadili biashara yenyewe na kuweza kufikia mafanikio makubwa.

Jambo la kwanza muhimu kabisa kufanya ni kutafuta kitu chochote kizuri ambacho unakipenda kupitia biashara hiyo, na kitu hicho kisiwe fedha.

Kama unauza magari ona kwamba unawasaidia watu kurahisisha kusafiri kwao.

Kama unauza vyakula, ona kwamba unawasaidia watu kuondokana na njaa na kupata afya bora.

Kwa biashara yoyote angalia kwa undani ni kitu gani kizuri unachofanya na kitakachoweza kukusukuma zaidi ili uendelee kutoa huduma bora zaidi.

Jambo la pili muhimu kufanya ni kujua vizuri ile biashara amabyo unaifanya.

Kama upo kwenye biashara ya magari kujua vizuri kila aina ya gari ambayo unauza na jinsi inavyoweza kumsaidia mteja wako.

Hakikisha mteja anapokuwa na swali lolote linalohusiana na biashara yako unaweza kumjibu kwa usahihi.

Hakikisha mteja hakuoni wewe kama mfanyabiashara tu, ila aweze kukuona kama mshauri wake mzuri katika biashara hiyo unayofanya.

Kwa kupata kitu unachokipenda kwenye biashara unayofanya sasa na kuijua biashara kwa undani na jinsi inavyowasaidia wengine kutatua changamoto zao mbalimbali, utaweza kujenga mapenzi makubwa kwenye biashara uliyonayo na hayo yakapelekea wewe kufanikiwa kwenye biashara hiyo.

Mafanikio kwenye biashara yatakuja kama utakuwa unafanya biashara ambayo ni sahihi kwako.

Tumeshaona kwamba biashara ambayo itakuletea mafanikio ni ile biashara ambayo ni sahihi kwako kufanya.

Pia tumeona biashara sahihi kwako kufanya ni ile ambayo inatokana na kitu ambacho unakipenda na pia unakijua au una uzoefu nacho.

Ili ujue biashara ambayo utaingia na uweze kupata mafanikio, unahitaji kuja na wazo bora la biashara.

Rafiki ata wewe leo hii unaweza kupata wazo bora la biashara kwa kutumia ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA, ambayo itakufundisha hatua kwa hatua jinsi ya kupata wazo bora la biashara na jinsi ya kuboresha wazo lako la biashara.

Unachotakiwa kufanya sasa hivi ni kupiga simu 0752977170 , kupata ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post