Siri Iliyomsaidia Rafiki Yangu Kuondoka Kwenye Madeni.

Siri Iliyomsaidia Rafiki Yangu Kuondoka Kwenye Madeni.

Madeni ni utumwa , hii ni kauli inayoudhi na inayoumiza  ambayo wengi hawapendi kuisikia, lakini kama ilivyo ukweli wowote, unaumiza lakini kuukataa hakuubadilishi.

Madeni ni utumwa kwa sababu unapokuwa na madeni, unakosa uhuru wa kutumia fedha yako. Ukishakuwa na deni ina maana kipato chochote unachopata, kinakwenda kulipa deni, hivyo huwezi kukitumia kama unavyotaka wewe.

Pia madeni ni utumwa kwa sababu anayekudai anakuwa na usimamizi mkubwa juu yako.

Ni kama vile unamfanyia kazi mtu anayekudai, kwa sababu usipomlipa, anayo njia ya kukutishia au kukudhalilisha kwa kushindwa kufanya hivyo.

 Kwa mfano kama umeweka nyumba au gari lako kama dhamana ya mkopo, dhamana hiyo inakuwa kitu cha kukunyanyasa wewe.

Kwa sababu utakaposhindwa kulipa mkopo , unapoteza kile ulichoweka dhamana.

Madeni ni utumwa kwa sababu unakuwa unawafanyia wengine kazi, hasa inapokuja kwenye madeni mabaya. Umekopa laki moja lakini unapaswa kulipa laki moja na riba juu.

Hii riba ndiyo njia ya kuwafanyia kazi wale ambao wamekukopesha fedha.

Madeni ni utumwa kwa sababu unaadhibiwa kwa kukopa.

Najua kama upo kwenye madeni utajiambia lakini mikopo imekusaidia, ila ukikaa chini na kupiga mahesabu ya riba ulizolipa, au unazolipa kwenye mikopo , utaona namna gani unaadhibiwa.

Na yote hiyo inatokana na kukosa nidhamu kwenye fedha. Hivyo kila unapofikiria madeni, pata picha moja kwenye akili yako, utumwa wa kujitakia, ambapo wewe mkopaji unatumikishwa na Yule aliyekukopesha.

Madeni Mazuri Na Madeni Mabaya.

Kuna aina kuu mbili za madeni, kutokana na manufaa ya madeni hayo kwa yule mtu anayekopa.

Aina Ya Kwanza Ni Madeni Mazuri.

Haya ni madeni amabyo yanakuwezesha wewe kupiga hatua kwenye maisha, madeni ambayo yanakuongezea wewe kipato na kukufikisha kwenye uhuru wa kifedha.

Madeni haya ni yale ambayo unayachukua kwa ajili ya kuzalisha zaidi, yanatengeneza faida na unaweza kuyarudisha pamoja na riba na ukabaki na faida wewe.

Kwenye madeni haya, mkopo unachukua wewe, ila wanalipa wengine, hulipi wewe moja kwa moja, hivyo unaepuka kuwa mtumwa wa mkopo huo.

Aina hii ya madeni ipo kwa watu wachache sana, wale watu ambao wanaendesha biashara zenye faida tayari, na hivyo wanachukua mkopo rahisi, ambao wameshapiga mahesabu yake na kujua mpaka wanalipa mkopo na riba, basi wanakuwa wamebakiwa na faida.

Nirudi, ni wachache sana wapo kwenye kundi hili la mikopo, wengine wengi, hata kama wanachukua mkopo wa kibiashara, wamekuwa wanalipa kiasi kikubwa zaidi kwenye riba kuliko faida wanayotengeneza.

Aina Ya Pili Ni Madeni Mabaya.

Haya ndiyo madeni hasa ambayo asilimia 99 ya watu wanayo, ni madeni mabaya kwa sababu mtu anaishia kulipa fedha nyingi kuliko ambazo ametumia.

Unakopa na unaishia kurudisha mkopo na riba kubwa.

Haya ni madeni ambayo unakopa na kulipa wewe mwenyewe, kutokana na kipato chako, na hakuna namna yoyote unazalisha kile unachokopa ili kupata faida.

Aina ya madeni haya ni madeni yoyote unayoyafanya kwa kutumia mshahara wako kama mfanyakai, au kwa kutumia mali yako nyingine yenye thamani.

Mikopo kwa ajili ya kupata chakula, kulipa ada, kulipa kodi za nyumba, kununua mavazi, kufanya sherehe, yote hayo ni madeni mabaya.

Kuchukua mkopo kwa ajili ya kununua gari ya kutembelea, au kujenga nyumba ya kuishi, ambayo ipo nje ya uwezo wako kwa wakati huo, ni mkopo mbaya.

Najua hapo kwenye mkopo wa nyumba, unaweza usielewe, kwa sababu huenda umeaminishwa kwamba kwa sababu nyumba itakuwa ni yako basi mkopo huo ni mzuri.

Lakini kama utapiga mahesabu na gharama zikawa zipo nje ya uwezo wako kwa kipindi hicho, ni mkopo mbaya

Kama makato ambayo unakatwa kwa ajili ya mkopo wa nyumba, ni zaidi ya mara mbili ya kodi unayoweza kulipa kama umepanga, na mkopo huo ni zaidi ya miaka 10, huo ni mkopo mbaya sana kwako.

Pamoja na ubaya wa mikopo hii, bado watu wengi huwa hawaoni wala hawasikii, hebu niambie, umekopa shilingi laki moja kwa ajili ya chakula, ukarudisha shilingi laki moja na elfu kumi, ile elfu kumi inatoka wapi? Mfukoni kwako.

Kwa hiyo unakopa laki moja, unapata chakula, au unanunua nguo , halafu unakuja kulipa ile laki moja , na elfu kumi juu.

Yaani ni sawa na anayekukopesha anakuambia, wewe si unataka nguo na huna fedha, sawa, nakupa fedha ukanunue nguo, halafu nitakuadhibu kwa shilingi elfu kumi. Na wewe unamwambia hakuna shida, nipe tu.

Ni jambo la kushangaza, lakini ndiyo maisha ambayo watu wanaishi kila siku.

Eneo hili la madeni linawatesa wengi, na nimejifunza mengi sana hapa kwa sababu siku za nyuma niliwahi kufanya biashara ya kukopesha watu kwa muda mfupi.

Wateja wazuri wa biashara hii ni waajiriwa ambao wanakipato cha uhakika kila mwezi. Watu hao wanakopa kwa sababu hata ambazo hazipaswi mtu akope.

Unakuta mtu anakopa kwa sababu ana harusi, au anakopa alipie watoto ada ya shule, au anakopa alipe kodi.

 Ni jambo linalowaumiza wengi sana, kwa sababu wanarudisha mkopo huo na riba, wakati hakuna chochote wanazalisha.

Kuna rafiki yangu mmoja nilikuwa namkopesha siku za nyuma, wakati bado nafanya biashara hiyo, mshahara wake ulikuwa mkubwa sana, ukilinganisha na mishahara ya kawaida ya wafanyakazi wa kitanzania.

 Hivyo alikuwa anakopa kiasi kikubwa pia, mwisho wa mwezi ukifika unarudisha mkopo na riba.

Hazipiti siku tano, anakutafuta tena kwa kutaka mkopo mwingine. Kuna wakati mpaka nikawa namwonea huruma, maana nilikuwa naona kama anaishia kuwa ananigawia sehemu ya mshahara wake wa kila mwezi, kwa sababu tu ya kukosa nidhamu.

 Lakini hata ukimshauri bado mambo ni yale yale.

Hivyo eneo hili la madeni, ni eneo muhimu mno kulifanyia kazi. Kwa sababu wengi wanaingia kwenye madeni wasiyoyaelewa vizuri, na pia wasiyoyahitaji.

Nimewahi kukutana na kijana ambaye alilazimika kuchukua mkopo, kwa sababu marafiki zake wote kazini wamechukua mkopo.

Na wakamwambia usipochukua mkopo lolote likitokea kwenye kazi utakosa kila kitu. Sababu ya hovyo mno ya kuingia kwenye madeni. Wengine wamekuwa wakichukua mikopo kwa sababu wameambiwa wanakopesheka. 

Hii ni kauli ambayo imewaingiza wengi kwenye matatizo.

 Kitu ambacho watu hawaelewi ni kwamba, benki au taasisi ya kifedha inapokuambia kwamba unakopesheka, hawamaanishi mkopo utakuwa mzuri kwako, bali wanachomaanisha ni kwamba mkopo wanaokupa, wana uhakika wa kuurudisha.

Hivyo eneo la madeni, kama tayari umeshaingia, ni eneo la kufanyia kazi haraka na uondoke. Kama bado, usijaribu kwa namna yoyote ile kuingia kwenye madeni, jipange vizuri kama utakavyojifunza hapo chini.

Kama tayari umeshaingia kwenye madeni, unachohitaji sasa hivi ni kutoka.

Kilichomsaidia rafiki yangu kutoka kwenye madeni ambayo yaliyokuwa yakimnyima usingizi mwaka jana, anakiri kwamba sio ujanja wake bali ni MAARIFA aliyoyapata Ndani ya kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, ambacho kilimfundisha hatua kwa hatua jinsi ya kuondoka kwenye madeni na jinsi ya kuepuka kuingia tena kwenye madeni.

Ata wewe leo hii unaweza kuondoka kwenye madeni yanayokunyima usingizi na kuepuka kuingia kwenye madeni , Kwa kupiga simu au kutuma ujumbe ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, kwenda namba 0752977170, SASA HIVI.

MUHIMU; Watu Kumi (10) wa mwanzo watapata OFA ya KUJIUNGA na CHANELI YA SOMA VITABU TANZANIA.

OFA HII ITAISHA TAREHE 21/06/2021, JUMATATU SAA SITA KAMILI MCHANA.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post