Imegundulika, Uraibu Wa Matumizi Ya Teknolojia Mpya Ni Chanzo Cha Sonona (depression) Kwa Wengi.

Ulishawahi kufikiria Hili Lingetokea?

Mtaalamu ALBERT EISNTEIN alishawahi kusema” Hatuwezi kutatua tatizo kwa kutumia kiwango kilekile cha uwezo wetu wa kufikiri tulichokuwa nacho wakati tunapata tatizo hilo”.

Ukweli ni kwamba kila changamoto inayokukabili leo inahitaji uwezo mkubwa zaidi wa kufikiri au maarifa ili uweze kuitatua.

Kinachofanya changamoto iwe ngumu, sio kwa sababu ya jinsi ilivyo bali kwa sababu ya uwezo mdogo wa maarifa uliyonayo.

Tafiti zinaonesha kwamba, uraibu wa mitandao ya kijamii kimekuwa chanzo kipya cha ugonjwa wa sonona  (depression) kwa wengi.

Kwa mfano mtu anapoweka picha au ujumbe wake, halafu watu wasiupende au wakaweka maoni mabaya, huku mwingine akiweka ujumbe au picha anapata likes nyingi au maoni mengi, inapelekea watu kuanza kujilinganisha na kuona wao hawajakamilika.

Wengine wanapoona wenzao wanaweka picha za kuonesha maisha yao ni mazuri, wakila vyakula vizuri, wakiwa maeneo ya starehe, wanaona wenzao wana maisha mazuri huku wao wakiwa na maisha mabaya, wasijue kwamba kila mtu anapenda kuweka picha za mambo mazuri , lakini yale mabaya hawaweki, na kila mtu ana mambo yake mabaya.

Swali la kujiuliza kuanzia sasa ni ; Je, kuna maarifa gani natakiwa kuongeza katika eneo hili ili niweze kukabiliana na changamoto hii na kuishinda?

Jibu ni rahisi unahitaji kuwa na maarifa sahihi  juu ya matumizi ya teknolojia hizi mpya.

Na kwa kuwa teknolojia hizi ni mpya, hakuna mwenye  uzoefu wa jinsi ya kukabiliana nazo , hivyo watu  wanaingia kwenye teknolojia hizo mpya kwa kuhadaiwa watanufaika sana, lakini kinachotokea ni wanageuzwa kuwa wafungwa.

Leo nina habari njema kwako, habari hizo ni kupatikana kwa mwongozo wa kuzitumia teknolojia hizi mpya vizuri na ukombozi wa ufungwa ambao teknolojia hizo zimetengeneza kwako.

Nimekuandalia kitabu kinachoitwa EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI, kitabu kinachokuonesha jinsi teknolojia mpya zinavyokufanya mtumwa na njia ya kuondoka kwenye utumwa huo.

Mpaka sasa kimesaidia maelfu ya watu waliokisoma na kila siku watu wanatoa shuhuda, kama wewe ni mmoja wao soma ukurasa wa 129 , kama bado uja pata nakala yako ya kitabu wasiliana na namba 0752977170, utaletewa au utatumiwa popote ulipo ndani ya AFRIKA MASHARIKI.

Unavyozidi kuchelewa kuchukua hatua ndivyo unavyozidi kupoteza rasilimali muda.

Kupitia kitabu hiki utajifunza mambo saba (7) makubwa ambayo yatakufanya uwe huru na  kuondokana na usumbufu unao kuingiza kwenye utumwa.

Moja utajifunza jinsi ubongo wako unavyofanya kazi na namna teknolojia mpya zinavyotumia ubongo huo kukufanya kuwa mtumwa.

Teknolojia mpya zimetengenezwa kwa namna ambayo zitajenga uteja/uraibu kwenye ubongo wako.

 Kwa kujua njia hiyo utaweza kuepuka kuingia kwenye utumwa wa teknolojia hizo.

Mbili utajifunza kuhusu zama tunazoishi sasa, zama za maarifa na taarifa lakini ambazo zimegeuka kuwa zama za usumbufu.

Utajifunza zama hizi za usumbufu zimetengeneza makundi makubwa mawili, wachache wanaonufaika sana, kama Mark Zuckerberg ambaye ni mmiliki wa Facebook na wengi ambao ni kama watumwa wa wachache hao wanaonufaika.

Ndani ya sura hii utajifunza jinsi ya kufikia viwango vya juu vya ufanisi.

Tatu utajifunza jinsi ya kujua kama tayari umeshanasa na kuwa mtumwa wa teknolojia hizo mpya.

 Unaposoma hapa unaweza kusema wewe hujawa mtumwa, unatumia kwa kupanga mwenyewe, lakini nikuambie kitu kimoja, kwa sehemu kubwa sana umeshakuwa na utaziona dalili kwa kusoma kitabu hiki.

Nne utajifunza jinsi ya kuondoka kwenye utumwa wa kidijitali ambao umeshaingia.

 Baada ya kuona jinsi ambavyo umenasa kwenye utumwa huo, utajifunza njia za kujinasua.

Hapa utajifunza jinsi ya kuizidi ujanja simu janja yako.

Tano utajifunza falsafa mpya ya kuendesha maisha yako kwa uhuru katika zama hizi za usumbufu.

Pamoja na kujifunza kuhusu zama hizo na jinsi ya kuondokana na utumwa wake, usumbufu wake hautaisha, teknolojia mpya zinaendelea kugunduliwa kila siku na zikiwa na ushawishi mkubwa.

Hivyo unahitaji kuwa na falsafa unayoitumia kuchagua huduma za kidijitali utakazochagua kutumia kwa manufaa yako.

Sita utajifunza jinsi ya kutumia akili yako kuvunja uraibu wowote ambao umeshajijengea. Kama tulivyoona, huduma za kidijitali zinatumia jinsi ubongo unavyofanya kazi kukuingiza kwenye utumwa.

 Hivyo wewe unapaswa kuutumia ubongo wako vizuri kuondoka kwenye utumwa huo.

Saba utajifunza sababu kumi kwa nini unapaswa kuondoka kwenye mitandao yote ya kijamii sasa hivi. Hizi ni sababu ambazo zimechambua jinsi matumizi ya mitandao ya kijamii yalivyo na athari kwenye akili yako, utulivu wako, mahusiano yako, uchumi wako na hata imani yako. Kwa kuzijua sababu hizi kumi, utajionea mwenyewe jinsi ulivyorudi nyuma tangu umeanza kutumia mitandao hiyo na hivyo kuachana nayo ili kuepuka madhara yake.

Mwisho kabisa utajifunza njia za kutumia kufanya maamuzi iwapo utumie huduma ya kidijitali.

Utajifunza jinsi ya kutumia vigezo vitatu vya AFYA, UTAJIRI na HEKIMA katika kuchagua na kutumia teknolojia mpya, ambazo zitakuwa na manufaa kwako badala ya kukufanya mtumwa.

Tuko kwenye vita, adui mkuu anajua yuko vitani ila wanaolengwa hawajui.

Hivyo unapaswa kuwa na maandalizi mazuri ya kupambana na vita hii ili uweze kutoka salama na siyo kuwa mfungwa.

Pata na usome kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI ili upate mbinu za kupambana kwenye vita hii na kutoka ukiwa mshindi. Kitabu hiki kimechapwa kwa nakala ngumu (hardcopy).

Kitabu kinauzwa TSH elfu 20 (20,000/=) na ili kukipata wasiliana na 0752 977 170 na utaletewa au kutumiwa kitabu popote ulipo Tanzania na Afrika Mashariki.

 Kwa sababu ya maombi ya watu wengi Leo tunatoa OFA kwa watu hamsini(50) wa kwanza, ukinunua LEO kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI, utapata fursa ya kujiunga na chaneli ya SOMA VITABU TANZANIA.

Unachotakiwa kufanya ni kutuma ujumbe mfupi unaosomeka “NIUNGE” kwenda namba 0752977170, baada ya kununua kitabu chako.

Vigezo na masharti kuzingatiwa.

MUHIMU; Kama utanunua na kusoma kitabu hiki na ukaona hakina manufaa yoyote kwako, unaruhusiwa kukirudisha na ukarejeshewa fedha zako.

Hivyo chukua hatua sasa, huna cha kupoteza lakini una mengi ya kupata, yatakayokuweka huru kwenye zama tunazoishi sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post

9 December 2022.9 December 2022.

9 December 2022. Rafiki Yangu, Kuna changamoto tano (5) kubwa zinazokuzuia kufanikiwa. 1. Fedha, madeni na uwekezaji. 2. Mshahara kutokutosheleza. 3. Biashara kuwa na changamoto. 4. Kukata tamaa. 5. Simu