Je Tunakwama Wapi? Iweje Tujue Kilicho Sahihi Kufanya, Lakini Hatukifanyi?

Ni nani asiyejua kwamba ukila vyakula vya wanga kwa wingi unaongeza uzito na kukaribisha magonjwa sugu kama presha na kisukari?

Ni nani asiyejua kuvuta sigara kuna madhara makubwa kiafya?

Ni nani asiyejua kwamba matumizi ya simu wakati wa kazi kunapunguza umakini na ubora wa kazi ambayo mtu anafanya?

Ni nani asiyejua kwamba kuzurura kwenye mitandao ya kijamii  siku nzima kunakufanya ujisikie wivu na hata vibaya unapoangalia maisha ya wengine , lakini pia unajua wanayoweka mitandaoni  siyo kweli?

Rafiki, kila mtu anajua madhara ya kufanya vitu hivyo , na vingine vingi.

Kila mtu anajua kitu sahihi cha kufanya ili kuwa na maisha bora, kuanzia kwenye afya, mahusiano, kazi na hata biashara.

Lakini pamoja na kujua kilicho sahihi kufanya, bado wengi hawafanyi.

Yaani unajua kabisa kipi sahihi kufanya , lakini hufanyi!  Unaweza kushangazwa na hilo?

Huwa tunakosea sana tunapodhani kwamba kujua kilicho sahihi kufanya ndiyo tumemaliza kila kitu.

Hii siyo kweli, na kama ushahidi unavyoonesha, kila mtu anajua cha kufanya , lakini wengi hawafanyi.

 Swali la kujiuliza ni je tunakwama wapi? Iweje tujue kilicho sahihi kufanya , lakini hatukifanyi?

Jibu la swali hili na hatua za kuchukua  nimekuwekea kwenye kitabu kipya cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI.

Mpaka sasa kimesaidia mamia ya watu waliokisoma na kila siku watu wanatoa shuhuda, kama wewe ni mmoja wao soma ukurasa wa 65, kama bado uja pata nakala yako ya kitabu wasiliana na namba 0752977170, utaletewa au utatumiwa popote ulipo ndani ya AFRIKA MASHARIKI.

Kupitia kitabu hiki utajifunza mambo saba(7) makubwa ambayo yatakufanya uwe huru na  kuondokana na usumbufu unao kuingiza kwenye utumwa.

Moja utajifunza jinsi ubongo wako unavyofanya kazi na namna teknolojia mpya zinavyotumia ubongo huo kukufanya kuwa mtumwa.

Teknolojia mpya zimetengenezwa kwa namna ambayo zitajenga uteja/uraibu kwenye ubongo wako.

 Kwa kujua njia hiyo utaweza kuepuka kuingia kwenye utumwa wa teknolojia hizo.

Mbili utajifunza kuhusu zama tunazoishi sasa, zama za maarifa na taarifa lakini ambazo zimegeuka kuwa zama za usumbufu. Utajifunza zama hizi za usumbufu zimetengeneza makundi makubwa mawili, wachache wanaonufaika sana, kama Mark Zuckerberg ambaye ni mmiliki wa Facebook na wengi ambao ni kama watumwa wa wachache hao wanaonufaika.

Tatu utajifunza jinsi ya kujua kama tayari umeshanasa na kuwa mtumwa wa teknolojia hizo mpya.

 Unaposoma hapa unaweza kusema wewe hujawa mtumwa, unatumia kwa kupanga mwenyewe, lakini nikuambie kitu kimoja, kwa sehemu kubwa sana umeshakuwa na utaziona dalili kwa kusoma kitabu hiki.

Nne utajifunza jinsi ya kuondoka kwenye utumwa wa kidijitali ambao umeshaingia.

 Baada ya kuona jinsi ambavyo umenasa kwenye utumwa huo, utajifunza njia za kujinasua.

Hapa utajifunza jinsi ya kuizidi ujanja simu janja yako.

Tano utajifunza falsafa mpya ya kuendesha maisha yako kwa uhuru katika zama hizi za usumbufu.

Pamoja na kujifunza kuhusu zama hizo na jinsi ya kuondokana na utumwa wake, usumbufu wake hautaisha, teknolojia mpya zinaendelea kugunduliwa kila siku na zikiwa na ushawishi mkubwa.

Hivyo unahitaji kuwa na falsafa unayoitumia kuchagua huduma za kidijitali utakazochagua kutumia kwa manufaa yako.

Sita utajifunza jinsi ya kutumia akili yako kuvunja uraibu wowote ambao umeshajijengea. Kama tulivyoona, huduma za kidijitali zinatumia jinsi ubongo unavyofanya kazi kukuingiza kwenye utumwa.

 Hivyo wewe unapaswa kuutumia ubongo wako vizuri kuondoka kwenye utumwa huo.

Saba utajifunza sababu kumi kwa nini unapaswa kuondoka kwenye mitandao yote ya kijamii sasa hivi. Hizi ni sababu ambazo zimechambua jinsi matumizi ya mitandao ya kijamii yalivyo na athari kwenye akili yako, utulivu wako, mahusiano yako, uchumi wako na hata imani yako. Kwa kuzijua sababu hizi kumi, utajionea mwenyewe jinsi ulivyorudi nyuma tangu umeanza kutumia mitandao hiyo na hivyo kuachana nayo ili kuepuka madhara yake.

Mwisho kabisa utajifunza njia za kutumia kufanya maamuzi iwapo utumie huduma ya kidijitali.

Utajifunza jinsi ya kutumia vigezo vitatu vya AFYA, UTAJIRI na HEKIMA katika kuchagua na kutumia teknolojia mpya, ambazo zitakuwa na manufaa kwako badala ya kukufanya mtumwa.

Tuko kwenye vita, adui mkuu anajua yuko vitani ila wanaolengwa hawajui.

Hivyo unapaswa kuwa na maandalizi mazuri ya kupambana na vita hii ili uweze kutoka salama na siyo kuwa mfungwa.

Pata na usome kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI ili upate mbinu za kupambana kwenye vita hii na kutoka ukiwa mshindi. Kitabu hiki kimechapwa kwa nakala ngumu (hardcopy).

Kitabu kinauzwa TSH elfu 20 (20,000/=) na ili kukipata wasiliana na 0752 977 170 na utaletewa au kutumiwa kitabu popote ulipo Tanzania na Afrika Mashariki.

 Kwa sababu ya maombi ya watu wengi Leo tunatoa OFA kwa watu hamsini(50) wa kwanza, ukinunua LEO kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI, utapata fursa ya kujiunga na chaneli ya SOMA VITABU TANZANIA.

Unachotakiwa kufanya ni kutuma ujumbe mfupi unaosomeka “NIUNGE” kwenda namba 0752977170, baada ya kununua kitabu chako.

Vigezo na masharti kuzingatiwa.

MUHIMU; Kama utanunua na kusoma kitabu hiki na ukaona hakina manufaa yoyote kwako, unaruhusiwa kukirudisha na ukarejeshewa fedha zako.

Hivyo chukua hatua sasa, huna cha kupoteza lakini una mengi ya kupata, yatakayokuweka huru kwenye zama tunazoishi sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post