Mahusiano 9 Kati Ya 10 Yamevunjika Kwenye Zama Hizi. Wewe Ni Mmoja Wao…?

Ndoa nyingi zimevunjika ,mahusiano mengi yamezorota, ukaribu nao umepungua.

Zama hizi zimekuwa na changamoto ya mahusiano mengi kuvunjika kuliko zama zilizopita.

Watu wamekuwa wanalalamika kwamba ndoa za sasa hazidumu na hata mahusiano baina ya watu yana changamoto nyingi.

Hayo ni kweli na mafuriko ya taarifa tuliyo nayo sasa yana mchango mkubwa kwenye kudorora na hata kuvunjika kwa mahusiano mengi.

Kujenga mahusiano yoyote yale , kuna hitaji kazi na muda. Katika zama hizi , muda ni kitu hadimu sana, hivyo mahusiano yanakosa muda yanayohitaji ili kukua , kitu kinacho pelekea mahusiano hayo yavunjike.

Urahisi wa mawasiliano pia umepelekea watu kutokuweka umakini kwenye mahusiano yao, hasa ya mapenzi kwa sababu wanajua wanaweza kupata mtu mwingine wakati wowote.

Kipindi cha nyuma haikuwa rahisi kuwasiliana na watu kama sasa, hivyo mtu alitumia muda wake kwa mpenzi au mweza aliye naye.

Tunaona jinsi ugomvi mkubwa kwenye mahusiano ya kimapenzi au ndoa unavyoanzia kwenye simu, pale mmoja anapokuwa na mawasiliano na mtu mwingine ambayo yana ashiria mahusiano ya kimapenzi.

Simu zetu pia zimekuwa na nguvu ya kuwaleta karibu walio mbali na kuwapeleka mbali walio karibu.

Angalia watu wanapokutana, hata kama hawajaonana kwa muda mrefu , dakika chache za mwanzo watajuliana hali, lakini baada ya muda kila mtu atainama kwenye simu yake na hakuna mazungumzo ya maana yatakayofanyika .

Kukosekana kwa muda wa kuwa na mazungumzo ya kina baina ya watu kumechangia sana mahusiano kudorora na hata kuvunjika.

Kutumia muda mwingi kwenye taarifa kuliko ana kwa ana pia imechangia mahusiano kuzorota na kuvunjika.

Kipindi cha nyuma watu walikuwa na muda wa kuzungumza ana kwa ana kujadili changamoto zao mbalimbali. Lakini zama hizi wanakwepa mazungumzo ya ana kwa ana na kutumia mazungumzo ya simu au mitandao ya kijamii.

 Ni vigumu sana kutatua hali ya kutoelewana kupitia mazungumzo ya simu au mtandao.

Ni dhahiri kwamba teknolojia mpya, hasa simu janja na mitandao ya kijamii, vimekuwa tatizo kubwa kwa wengi. Kila mtu analalamika jinsi vitu hivyo vinavyochukua muda mwingi, na kuchangia mahusiano mengi kuzorota na kuvunjika kabisa.

Wanaotengeneza na kuendesha teknolojia hizo hawajali kuhusu hilo, kwani kadiri unavyozitumia kwa muda mrefu, ndivyo wao wanavyopata faida.

 Hivyo wamejipanga kuhakikisha watumiaji wanaendelea kuwa wafungwa kwenye teknolojia hizo.

Na kwa kuwa teknolojia hizi ni mpya, hakuna mwenye uzoefu wa jinsi ya kukabiliana nazo, hivyo watu wanaingia kwenye teknolojia hizo mpya kwa kuhadaiwa watanufaika sana, lakini kinachotokea ni wanageuzwa kuwa wafungwa.

Leo nina habari njema kwako, habari hizo ni kupatikana kwa mwongozo wa kuzitumia teknolojia hizi mpya vizuri na ukombozi wa ufungwa ambao teknolojia hizo zimetengeneza kwako.

Nimekuandalia kitabu kinachoitwa EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI, kitabu kinachokuonesha jinsi teknolojia mpya zinavyokufanya mtumwa na njia za kuondoka kwenye utumwa huo.

Kupitia kitabu hiki utajifunza mambo saba makubwa ambayo yatakufanya uwe huru na utumie teknolojia hizi kwa manufaa makubwa kwako.

Moja utajifunza jinsi ubongo wako unavyofanya kazi na namna teknolojia mpya zinavyotumia ubongo huo kukufanya kuwa mtumwa.

Mbili utajifunza kuhusu zama tunazoishi sasa, zama za maarifa na taarifa lakini ambazo zimegeuka kuwa zama za usumbufu. Utajifunza zama hizi za usumbufu zimetengeneza makundi makubwa mawili, wachache wanaonufaika sana, kama Mark Zuckerberg ambaye ni mmiliki wa Facebook na wengi ambao ni kama watumwa wa wachache hao wanaonufaika.

Tatu utajifunza jinsi ya kujua kama tayari umeshanasa na kuwa mtumwa wa teknolojia hizo mpya. Unaposoma hapa unaweza kusema wewe hujawa mtumwa, unatumia kwa kupanga mwenyewe, lakini nikuambie kitu kimoja, kwa sehemu kubwa sana umeshakuwa na utaziona dalili kwa kusoma kitabu hiki.

Nne utajifunza jinsi ya kuondoka kwenye utumwa wa kidijitali ambao umeshaingia.

Tano utajifunza falsafa mpya ya kuendesha maisha yako kwa uhuru katika zama hizi za usumbufu.

Sita utajifunza jinsi ya kutumia akili yako kuvunja uraibu wowote ambao umeshajijengea.

Saba utajifunza sababu kumi kwa nini unapaswa kuondoka kwenye mitandao yote ya kijamii sasa hivi.

Mwisho kabisa utajifunza njia za kutumia kufanya maamuzi iwapo utumie huduma ya kidijitali. Utajifunza jinsi ya kutumia vigezo vitatu vya AFYA, UTAJIRI na HEKIMA katika kuchagua na kutumia teknolojia mpya, ambazo zitakuwa na manufaa kwako badala ya kukufanya mtumwa.

Tuko kwenye vita, adui mkuu anajua yuko vitani ila wanaolengwa hawajui. Hivyo unapaswa kuwa na maandalizi mazuri ya kupambana na vita hii ili uweze kutoka salama na siyo kuwa mfungwa.

Pata na usome kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI ili upate mbinu za kupambana kwenye vita hii na kutoka ukiwa mshindi. Kitabu hiki kimechapwa kwa nakala ngumu (hardcopy).

Kitabu kinauzwa TSH elfu 20 (20,000/=) na ili kukipata wasiliana na 0752 977 170 na utaletewa au kutumiwa kitabu popote ulipo Tanzania na Afrika Mashariki.

OFA: Ukinunua LEO kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI, utapata fursa ya kujiunga na chaneli ya SOMA VITABU TANZANIA.

Unachotakiwa kufanya ni kutuma ujumbe mfupi unaosomeka “NIUNGE” kwenda namba 0752977170, baada ya kununua kitabu chako.

MUHIMU; Kama utanunua na kusoma kitabu hiki na ukaona hakina manufaa yoyote kwako, unaruhusiwa kukirudisha na ukarejeshewa fedha zako. Hivyo chukua hatua sasa, huna cha kupoteza lakini una mengi ya kupata, yatakayokuweka huru kwenye zama tunazoishi sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post