Kwa Nini Usiwe na Furaha Muda Wote Baada Ya Kupata Kile Unachotaka…

Kwa nini Usiwe na Furaha Muda Wote Baada Ya Kupata Kile Unachotaka Kwenye Maisha Yako?…

Mpendwa Mpambanaji,

Kama unataka furaha itawale kwenye maisha yako huku ukiwa na amani ya moyo wako, basi makala hii itakuburudisha zaidi ya mirinda nyeusi baridi baada ya kunywa supu asubuhi.

Naelewa unavyojisikia na hayo sio makosa yako kabisa ni mfumo wa maisha tuliokuta upo katika jamii ambao kwa sasa umepitwa na wakati kwenye karne hii ya 21…

Furaha ni zao la ndani , kile ambaye amekuwa anaanza kufanya kitu chochote kwenye maisha yake kwa lengo la kupata furaha, amekuwa anaishia kujisikia vibaya baada ya kupata alichofikiri akipata kitampa FURAHA.

Wengi wanapokutana na hali hii huwa wanafikiri kuna shida kwenye kile walichopata, lakini ukweli ni kwamba shida haipo kwenye chochote unachotaka , basi shida ipo ndani yako.

Furaha ya kweli kwenye maisha ni zao la ndani, ni kitu kinachoanzia kwenye fikra zako na siyo matokeo ya kile unachopata.

Hata kama umepata kitu kikubwa na muhimu kiasi gani, furaha yake huwa ni ya muda mfupi tu, baada ya hapo unarudi kwenye hali yako ya kawaida.

Sasa unaweza ukawa unajiuliza nini kinasababisha hilo? Kwa nini usiwe na furaha muda wote baada ya kupata kila unachotaka?

Rafiki Yangu Mpambanaji, ubongo wetu huzalisha furaha kwa kutoa kemikali nne(4) . Kemikali hizi huzalishwa mara moja pale unapokamilisha kitu Fulani.

….lakini baada ya kuzalishwa, mwili huvunja kemikali hizi na ndiyo maana ile hali ya furaha inadumu kwa muda mfupi.

Ili uendelee kupata furaha hiyo, inabidi mwili uzalishe tena kemikali hizo za furaha, kitu ambacho kinakutaka ukamilishe kitu kikubwa kuliko kile cha awali.

…na hili ndiyo linapelekea wengi kujikuta kila wakati wanatamani vitu vikubwa zaidi, wakiamini kuvipata kutawapa furaha ya kudumu, lakini wakishavipata furaha inapotea baada ya muda mfupi.

Furaha ya kweli inaanzia ndani yako na siyo nje, ili kuwa na furaha ya kweli, kwanza lazima uielewe akili yako jinsi inavyozalisha furaha na kisha kuitumia vizuri kutengeneza furaha inayotegemea ndani yako na siyo nje.

…kwa mfano, badala ya kusubiri mpaka ukamilishe lengo kubwa ndiyo upate furaha, unagawa lengo hilo kwenye hatua ndogo ndogo za kuchukua kila siku, na kila siku unapokamilisha hatua uliyojipangia unapata furaha.

…kwa njia hii utakuwa na furaha inayodumu kila siku kwa hatua ndogo ndogo unazopiga badala ya kusubiri mpaka ukamilishe lengo moja kubwa, ambalo furaha yake itadumu kwa muda mfupi sana.

Hata hivyo, ubongo wako unazalisha kemikali nne (4) ambazo zinaleta furaha kwenye maisha yetu Kemikali hizi zinatofautiana kwa ufanyaji wake wa kazi, lakini mwisho wa siku zote zinaleta furaha.

…habari njema ni kwamba ili uweze kutengeneza furaha ya kudumu, unapaswa kuzalisha kemikali za furaha kwa njia ya asili na mara kwa mara.

Zipo tabia 18 za kuishi kila siku ambazo zitakuwezesha kuzalisha kemikali hizo kila siku na hivyo kuwa na furaha ya kudumu.

Bahati Iliojee!..Tabia zote 18 na namna ya kuziishi kila siku ili uwe na FURAHA YA KUDUMU, utazipata SURA YA PILI (2) Ndani Ya kitabu cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA.

…kama unataka furaha ikutawale kwenye maisha yako na usiku ulale fofofo kama mtoto mchanga huku ukitabasamu basi piga simu sasahivi au tuma meseji yenye neno “FURAHA” kwenda 0752977170.

KWASABABU leo ni KARUME DAY  Ukilipia kitabu chako cha UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA, nitakuzawadia kitabu cha SIMU YANGU OFISI YANGU.

Kumbuka; Thamani ya vitabu vyote viwili ni tshs 60,000K , na Kwasababu leo ni holiday utavipata vyote viwili kwa TSHS 19,999TU! Bila ya Kutolea. Una subiri nini tuwasiliane hapa 0752977170.

OFA HII INADUMU NDANI YA MASAA 24 BAADA YA HAPO INAEXPIRE.

MUHIMU; Endapo Utavisoma Ukaona Havija kusaidia ni ruksa kuvirudisha na hautaulizwa chochote. Kwahiyo hauna cha kupoteza una mengi ya kupata.

Shabiki Yako Namba Moja…

BwanaRama|CopywriterOfSomaVitabuTanzania|

Karibu, www.somavitabu.co.tz

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post