Tabia Zitakazo Kuua Mapema.

Tabia 3 zitakazokuua mapema.

Rafiki yangu mpendwa,

Huwa ninaamini kila mtu anaweza kuishi miaka mingi kuliko ilivyozoeleka.

Kuishi miaka zaidi ya 100 ni jambo linalowezekana kabisa.

Na hilo ndiyo lengo ambalo nimejiwekea kwenye maisha yangu, kuishi zaidi ya miaka 100. 

Ili kutimiza lengo hilo, nimekuwa nikitafiti na kujifunza kwa kina jinsi ya kuweza kuishi miaka mingi.

Tafiti za eneo hilo ni nyingi na zinaeleza mambo mengi, ule nini na usile nini na hata kiwango cha kile unapaswa kula.

Sasa unanijua mimi rafiki yako, huwa napenda kutafuta njia ya kurahisisha vitu ili iwe rahisi kuvitekeleza.

Kwa tafiti nyingi nilizosoma, nimegundua kuna mambo matatu ambayo ndiyo yanachangia vifo vya mapema kwa wengi.

Mambo hayo matatu ni;

1. Unywaji wa pombe.

2. Uvutaji wa sigara.

3. Uzito uliopitiliza.

Nikiyaelezea kwa ufupi sana, kama unataka kuishi miaka mingi;

1. Usinywe pombe.

Hapa najua kama ni mnywaji utanipinga sana. Utaniambia unakunywa kistaarabu na mengine kama hayo.

Na mimi sina la kukujibu zaidi ya kukuambia kila la kheri kwenye kuharakisha kifo chako.

2. Usivute sigara.

Hili sihitaji nguvu kukushawishi, unajua jinsi sigara ilivyo na madhara. Hivyo usivute wala kukaa karibu na mvutaji.

3. Usiwe na uzito mkubwa.

Ili kueleweka vizuri, uzito wako wa mwili usiziki kilo 75.

Unafanyaje kwenye hili la uzito?

Mambo mawili; ulaji na mazoezi.

A. Usile vitu vya sukari na wanga kwa wingi.

B. Fanya mazoezi ya mwili yanayokutoa jasho.

Ni hayo tu rafiki.

Kama yupo anayekuambia tofauti na hayo, au anaufanya mchakato kuwa mgumu zaidi ya hapo, jua kuna kitu anataka kukuuzia.

Unaona hapo, nimekupa kitu chenye thamani mno kwenye maisha yako, bila ya kulipia chochote.

Lakini nina swali kwako,

Kama kweli utajitahidi na kuishi miaka mingi, yatakuwaje kama utakuwa huna fedha za kutosha?

Pata picha una miaka 90 na huna akiba wala uwekezaji.

Hayo maisha yatakuwaje?

Naamini utatamani tu ufe, maana mateso ya kukosa fedha hutayaweza.

Na hapo sasa ndipo mimi nataka nikusaidie.

Nataka uweze kujijengea kipato, akiba na uwekezaji ambapo hata ukiishi miaka zaidi ya 100, unakuwa huru kifedha.

Kama upo tayari kwa mkakati huo wa kuwa huru kifedha ili maisha yako yawe marefu na tulivu, jibu ujumbe huu kwa maneno; UHURU 100.

Rafiki, hitaji langu kwako ni uishi zaidi ya miaka 100 huku ukiwa huru kabisa.

Najua hilo linawezekana.

Nijibu sasa UHURU 100.

UHURU 100.

Ishi zaidi ya miaka 100 huku ukiwa na UHURU wa kifedha.

Hongera kwa kupenda kujua kuhusu UHURU 100.

Hiki ni kifurushi cha maarifa yatakayokuwezesha kuishi miaka zaidi ya 100 huku ukiwa na UHURU WA KIFEDHA.

Maana haina maana kuishi miaka mingi huku ukiwa masikini.

Ni kurefusha tu mateso ya maisha.

Kifurushi hiki kina vitabu vifuatavyo ambavyo vinakwenda kukupa maarifa na hatua sahihi za kuchukua.

1. ELIMU YA MSINGI YA FEDHA

Hiki kinakupa maarifa ya kuongeza kipato, kuweka akiba na kuwekeza. Haya ni muhimu sana katika kujenga utajiri na uhuru wa kifedha.

2. ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA.

Hiki kinakupa maarifa ya kuanzisha na kukuza biashara inayoweza kujiendesha yenyewe bila kukutegemea. Hilo ndiyo linakupa uhuru wa kuingiza kipato bila hata ya kufanya kazi.

3. TABIA ZA KITAJIRI.

Hiki kinakupa maarifa ya tabia sahihi unazopaswa kuziishi kila siku ili uweze kuwa na mafanikio makubwa.

4. KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO.

Hiki kinakupa maarifa ya mambo ya kuzingatia kwenye kila siku yako tangu unaamka mpaka kulala ili iwe siku bora na ya mafanikio.

Kuna mengi ya kiafya hapa kuhusu ulaji, mazoezi na kupumzika.

Jipatie vitabu hivi leo ili uweze kuishi miaka mingi ukiwa na uhuru wa kifedha.

Kwa kuwasiliana nasi 0752 977 170 kupata vitabu vyako.

Rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,

Kocha Dr. Makirita Amani.

Karibu sana rafiki yangu.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post