%UFUNGUO WA MAFANIKIO.

%Ufunguo Wa Mafanikio.

Rafiki yangu,

Kuweka bidii kwenye kile unachokifanya ndio ufunguo wa mafanikio yako, hivyo usipoweka bidii ujue kufeli ni swala la kugusa tu..

Inawezekana ni vitu vingi sana umevisikia kuhusu mafanikio Lakini bidii ni mkubwa wao.

Huu hapa ni mfano mdogo sana juu ya kuweka bidii kwenye kile unachokifanya.

Angalia mwenyewe hapa chini.

Kwenye wilaya ya  KYELA Mkoani Mbeya, kulikuwepo na mkulima mmoja wa makamo aliyejulikana kwa jina maarufu kama MZEE MWAKIPESILE ni MZEE mwenye umri wa miaka 68 ambaye alibarikiwa shamba kubwa sana la mpunga na pia alibarikiwa watoto wa tatu (3) wa kiume ambao ni vijana wenye nguvu lakini hawapendi na hawataki kufanya kazi.

Walifahamika kama Erick ,Millard na Baraka,  mkulima huyu alifanikiwa sana, nikisema alifanikiwa sana ninamaansha kwamba alikuwa anavuna matani kwa matani ya mpunga kila mwaka kwa sababu shamba lake lilikuwa na rutuba ya kutosha, mbali na hivyo alitia bidii sana kwenye kilimo hali hiyo ikapelekea mpaka wanakijiji wenzake wakawa wanamuonea gere (wivu).

Ina kuaje?

Hivyo ndivyo walivyokuwa wakiulizana iweje kila siku yeye tu, hali ya wivu iliwaingia kiasi kwamba wakawa wanahisi jamaa anatumia imani za kishirikina.

 Lakini hakusikiliza kelele zao.

Kama mkulima mwenye mafanikio makubwa na mwenye umri mkubwa akaanza kuingiwa na wasi wasi juu ya hatma ya watoto wake watatu (3).

Baada ya kuhisi kuumwa hali iliyompelekea kupata maumivu makali, gafla aligundua kifo kipo karibu kumchukua.

Na kabla maji hayajazidi unga, aliwaita watoto wake wote watatu (3) na kuwaambia,

NANUKUU” Watoto wangu wapendwa nimewaita hapa kwa sababu nahisi maumivu makali naona kifo kipo karibu nami lakini kabla sijawaaga naomba niwashirikishe siri ambayo itawatajirisha kwa haraka, sikilizeni kwa makini Kuna hazina nimeificha kwenye shamba la mpunga hivyo kuipata hazina hiyo ni sharti mlime shamba ili mkutane na hiyo hazina sio kinyume na hivyo,

… baada ya mimi kufariki,

Mnanielewa? Watoto wakajibu kwa huzuni NDIO tunakuelewa BABA.”

Kesho yake Baba yao akaaga dunia (akafariki) baada ya watoto kumaliza kutoa heshima za mwisho.

Watoto wakaanza kulima shamba lote la mpunga ndani ya siku 7 za juma, lakini hakuna chochote walichoambulia, hata hivyo kulima shamba lao kuliwapelekea kuvuna matani kwa matani ya mpunga  na matokeo yake walipata pesa nyingi sana,

Ambazo hawakuwahi kuzipata hapo kabla, kwa sababu walikuwa ni vijana wavivu sana hivyo hawakuwahi kufanya kazi yoyote ya kuwaingizia kipato, ni vijana ambao walikuwa wakisubiri tu kupewa fedha na baba yao.

Mara ya kwanza, walivyopewa ile siri na mzee  wao,hawakuelewa chochote mpaka pale walipovuna na kuuza mpunga wao ndipo wakaja kuelewa kilealichokuwa akimaansha baba yao.

Kipato kikubwa walichokipata  kimewafanya kuja kuelewa kile ambacho baba yao alichokuwa akimaansha,

TUNAJIFUNZA KWAMBA;  Kuweka bidii kwenye kile unachokifanya mara zote hulipa, hivyo Ndoto haiwezi kutimia kwa miujiza unapaswa utie bidii kweli kweli mpaka itimie.

Ili ndoto yako iweze kutimia unapaswa uvuje jasho haswa na uweke juhudi  kweli kweli kwenye kile unachoifanya , kinyume na hivyo utafeli.

Lakini pamoja na hayo yote hayo,

Bidii pekee haitoshi  pale ambapo itaambatana na MAARIFA, inakuwa ni MOTO WA KUOTEA MBALI.

Na maarifa sahihi siku zote yanapatikana kwenye vitabu vizuri,

Kwa Mfano Leo Hii Ukisome vitabu Hivi (8) Vizuri Vitaharakisha Safari Yako Ya Mafanikio , na hivyo utafikia Ndoto Zako Ukiwa Hujachoka Kama Watoto Wa Mzee MWAKIPISILE,

Hahaaaa…

Karibu Ufungue Ukurasa Mpya.

1.       KITABU; ELIMU YA MSINGI YA FEDHA.

2.       KITABU; ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA.

3.       KITABU; UNA NGUVU YA KUTENDA MIUJIZA.

4.       KITABU; EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI.

5.       KITABU; KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO.

6.       KITABU; TABIA ZA KITAJIRI.

7.       KITABU; BIASHARA NDANI YA AJIRA.

Na,

8.       KITABU; MWONGOZO WA MAISHA YA MAFANIKIO.

Fanya hivii,

Chagua kitabu chochote hapo juu, Kisha tuwasiliane kwa kupiga simu 0752977170.

 Karibu Sana,

Nakupenda Sana.

Kutoka Kwa Shabiki Yako Namba 1,

AmryRamadhani|CopywriterOfSomaVitabuTanzania|

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post

Ni Upendo Tu!Ni Upendo Tu!

Ni Upendo Tu! Rafiki Yangu Mpendwa, Vp Hali Yako? Nakuhakikishia ukiisoma hii meseji fupi mpaka mwisho, …utajipenda sana. “Vifaranga hushuhudia upendo wa kweli kutoka kwa mama yao pale atakapokuwa anahangaika