Una Yatumiaje Masaa 24 Ya Siku?.

Una Yatumiaje Masaa 24 Ya Siku?…  

Rafiki Yangu, Vp Hali Yako?

Ukweli ni kwamba siku ya leo umezawadiwa masaa 24.

Nikikuuliza Mpaka Saa Hii Umeyatumiaje Hayo Masaa 24 Utanijibuje?

Sema Usiwe na wasi wasi, vuta pumzi ningojee…

Nipo hapa kwa ajili ya kukukumbusha tu na hivyo ukipata maarifa sahihi utakumbuka si ndio?

Angalia mwenyewe hapo chini.

Jinsi unavyoyatumia masaa yako kila siku.

Wewe mwenyewe shahidi.

Siku moja ina masaa 24 pekee, imekuwa hivi tangu enzi na enzi.

Na nina uhakika ya kwamba itaendelea kuwa hivi kwa muda mrefu ujao.

Kwa hali ilivyo sasa, sioni dalili zozote za kuweza kutengeneza masaa ya ziada.

 Hivyo haya ndiyo masaa tuliyonayo na tutaendelea kuwa nayo.

Hivyo tunavyosema kwamba muda hautoshi, siyo kwamba tunataka muda uongezwe, bali kuna tatizo kubwa zaidi ndani ambalo tunalificha.

Tatizo hilo ndilo tunakwenda kulimulika hapa ili tuweze kumalizana nalo kabisa.

Tatizo la muda linaanzia kwenye matumizi yetu ya muda.

 Linaanzia kwenye vipaumbele vyetu na jinsi tunavyoitumia kila dakika ya muda wetu.

Ikiwa tutaweza kusimamia hili vizuri.

 Ikiwa tutaweza kudhibiti matumizi yetu ya muda, tutaona ni jinsi gani ambavyo tuna muda mwingi wa kuweza kufanya chochote tunachotaka kufanya.

Kama unataka kupinga kwamba huna matumizi mabaya ya muda.

 Hebu tufanye mahesabu kidogo, maana ukiangalia msitu kwa mbali huwezi kujua kuna miti mingapi,

…ila unapoingia katikati ya msitu, unaacha kuona msitu na badala yake unaona mti mmoja mmoja.

Sasa karibu tuone mti mmoja mmoja kwenye matumizi ya muda wako.

Njia bora ya kuanza kuuangalia muda wako kwa undani ni kutumia wiki moja.

 Ambapo wiki ina siku 7, Jumatatu mpaka Jumapili.

 Kwa masaa 24 ya siku moja, ukizidisha kwa siku saba unapata masaa 168 kwa wiki nzima.

 Sasa hebu tuchambue matumizi haya ya masaa 168 kwa wiki moja.

Kwa waajiriwa mara nyingi kazi utafanya masaa 8 mpaka kumi kwa siku, na utafanya siku tano au sita kwa wiki.

Hivyo tuchukulie kiwango cha juu cha masaa 10 (japo kuna wanaofanya masaa 8) na tuchukulie kiwango cha juu cha siku sita kwa wiki (japo kuna wanaofanya siku 5),

… tunapata wiki moja ya kazi inachukua masaa 60 (hapa kuna ambao wanatumia masaa 40 au 50 pekee).

 Tukirudi kwenye benki yetu ya masaa 168 kwa wiki, tukitoa masaa 60 tunakuwa tumebakiwa na masaa 108.

 Sawa, sasa kuna kitu kingine muhimu sana ambacho ni kulala, lazima kila mtu alale, na kiwango cha chini kinachoshauriwa kiafya ni angalau masaa 7 kwa siku.

 Hivyo tukizidisha masaa 7 kwa siku 7 tunapata masaa 49.

Ondoa masaa 49 kwenye salio la masaa yako ya wiki ambapo ulikuwa na 108 utabaki na masaa 59.

Haya una masaa 59 kwenye mkono wako, umeshaondoa kazi na umeshaondoa kulala.

Sasa kuna muda wa wewe kula, kusafiri kwenda na kurudi kazini, kupumzika na kukaa na wale ambao ni wa muhimu kwako.

Kwa wastani tuweke masaa matatu kila siku.

Kwa wale ambao kusafiri kwenda na kurudi kazini kunachukua zaidi ya saa moja kwa siku, baadaye nitakushauri jinsi ya kuutumia muda huo kibiashara,

… hivyo usianze kukataa hapa kwamba masaa matatu kwa siku hayakutoshi kwa hayo mengine.

Masaa matatu kwa siku kwa siku saba tunapata masaa 21, tulikuwa na salio la masa 59 tukitoa masaa 21 tunapata masaa 38.

Hapa una masaa 38 ya kwako wewe mwenyewe kila wiki, au tufanye kwa kiwango cha chini sana, masaa 30 kila siki, ambayo haya huna kazi, hulali, wala hukai na wale ambao ni wa muhimu kwako.

Haya ni masaa ambayo ninaweza kusema bila ya shaka kwamba kama huna biashara au uzalishaji mwingine wowote, umekuwa unayapoteza.

Kama nilivyokuambia awali, ukiangalia msitu kwa mbali utaona ule ni msitu tu, lakini ukiingia ndani ya msitu utaona miti tofauti.

Tukichukua masaa 30 kila wiki, tukazidisha kwa wiki 52 zilizopo kwenye mwaka tunapata masaa 1560 tukiyagawa kwa masaa 24 ya siku moja tunapata siku 65.

 Yaani kila mwaka unapoteza miezi miwili bila ya kujua unaifanyia nini.

Na tukiamua kuyagawa masaa 1560 unayopoteza kila mwaka kwa masaa 10 ya kazi kwa siku tunapata siku za kikazi 156.

 Hebu piga hesabu kwa siku unalipwa kiasi gani na zidisha kwa 156, utaona fedha nyingi unazopoteza kila mwaka.

Tuachane na hesabu sasa turudi kwenye uhalisia, nakiri kwamba kuna mambo mengi yanaweza kujitokea kwenye kila wiki ambayo yataathiri muda wako.

Lakini jambo moja ambalo utakubaliana na mimi ni kwamba kila siki una muda mwingi ambao unapotea bila ya wewe kufanya chochote cha msingi.

Huu ndio muda ambao nataka wewe uujue kwanza unapotelea wapi, na uanze kuutumia kufanya jambo lolote ambalo litakuweka kwenye nafasi nzuri ya kuanza biashara yako.

 Hata kama unapata saa moja pekee kwenye siku yako.

Kama ukiweza kuipangilia saa hii vizuri utaweza kusimamisha biashara yako baada ya muda.

Na tena ukitumia muda ambao umekuwa kazini, kama ni miaka 10, unafikiri ungechagua kufanya kitu kwa saa moja kila siku kwa miaka kumi leo ungekuwa wapi?

Na kama hupendi majuto yawe sehemu ya maisha yako.

Basi nakushauri urudie kusoma vitabu hivi viwili (2);

1.       BIASHARA NDANI YA AJIRA, TOLEO LA PILI. Tshs 19,999Tu! Bila Ya Kutolea.

2.       KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO. Tshs 19,999Tu! Bila Ya Kutolea.

Na amini hutojutia.

Na kama bado hujavisoma, usiwe na wasi wasi kwa sababu utaletewa au utatumiwa vitabu vyako popote ulipo ndani ya AFRIKA MASHARIKI.

Na Piga simu 0752977170.

Kupata Vitabu Vyako Viwili (2).

#Uaminifu Ndio Silaha Yetu.

Karibu Sana.

Shabiki Yako Namba 1.

Nakupenda.

Wako| AmryRamadhani|CopywriterOfSomaVitabuTanzania|

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post