Unasumbuka Na Ufanisi Kazini…?

Leo nimeamua nikusogezee mada hii kwenye macho yako kwani imekuwa changamoto na kuathiri utendaji kazi wa watu wengi.

 Ukweli ni kwamba akili zetu sisi binadamu ni kitu cha ajabu sana, ni kitu ambacho kina nguvu ya kufanya makubwa kuliko tunavyoweza kutegemea.

Lakini cha kushangaza ni kwamba, mtu anaweza kuitawala akili yake akafanya makubwa, au akatawaliwa na akili yake na kuwa mtumwa maisha yake yote.

kuhusu ubongo wa binadamu ni kwamba una nguvu za ajabu lakini watu wengi hutumia sehemu ndogo sana ya nguvu hiyo.

Asilimia kubwa ya watu huishia kufanya mambo ya kawaida, hivyo hupata matokeo kawaida na kuishi maisha ya kawaida (routine life).

Lakini kundi lingine ni watu ambao ni asilimia ndogo ambao hufikia viwango vya juu vya ufanisi/ nguvu za ubongo wao.

Kundi hili hufanya mambo makubwa na huwa na maisha tofauti na kundi la kwanza.

Tofauti ipo kwenye namna tunavyotumia bongo zetu, uamuzi upo mikononi mwako.

Ujenge au ubomoe.

Uzuri mpaka hapa umeshajua upo kundi gani.

Kama tayari tuendelee…

Ubongo wetu unaweza kutunza taarifa  mbalimbali kwa muda,  ambazo baadae huenda kwenye subconscious mind.

Ili taarifa zivuke kwenye subconscious mind, hupita kwenye mfumo RAS ( Recuticular Activating System) ambapo taarifa huchujwa.

Ili kundi lingine huruhusu vitu vya kimazingira kuingia ambavyo huathiri maamuzi na kisha utendaji.

Kwa bahati mbaya huwezi kufikia viwango vya juu vya ufanisi ikiwa muda mwingi umezungukwa na usumbufu.

Hivyo unapaswa uwe na ufahamu juu ya vitu gani vinavyokuletea usumbufu na kuweza kuvidhibiti mara moja.

Kuna maelfu ya watu walipitia hali kama hii na wakafanikiwa kutoka mimi ni miongoni mwao, hata wewe leo hii unaweza kutoka kwenye hali hii.

Unachopaswa kufanya sasa ni kusoma SURA YA PILI Ya kitabu kipya kinachoitwa EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI.

Mpaka sasa kimesaidia maelfu ya watu waliokisoma na kila siku watu wanatoa shuhuda, kama wewe ni mmoja wao soma SURA YA PILI, kama bado uja pata nakala yako ya kitabu wasiliana na namba 0752977170, utaletewa au utatumiwa popote ulipo ndani ya AFRIKA MASHARIKI.

Unavyozidi kuchelewa kuchukua hatua ndivyo unavyozidi kupoteza rasilimali muda.

Kupitia kitabu hiki utajifunza mambo saba(7) makubwa ambayo yatakufanya uwe huru na  kuondokana na usumbufu unao kuingiza kwenye utumwa.

Moja utajifunza jinsi ubongo wako unavyofanya kazi na namna teknolojia mpya zinavyotumia ubongo huo kukufanya kuwa mtumwa.

Teknolojia mpya zimetengenezwa kwa namna ambayo zitajenga uteja/uraibu kwenye ubongo wako.

 Kwa kujua njia hiyo utaweza kuepuka kuingia kwenye utumwa wa teknolojia hizo.

Mbili utajifunza kuhusu zama tunazoishi sasa, zama za maarifa na taarifa lakini ambazo zimegeuka kuwa zama za usumbufu.

Utajifunza zama hizi za usumbufu zimetengeneza makundi makubwa mawili, wachache wanaonufaika sana, kama Mark Zuckerberg ambaye ni mmiliki wa Facebook na wengi ambao ni kama watumwa wa wachache hao wanaonufaika.

Ndani ya sura hii utajifunza jinsi ya kufikia viwango vya juu vya ufanisi.

Tatu utajifunza jinsi ya kujua kama tayari umeshanasa na kuwa mtumwa wa teknolojia hizo mpya.

 Unaposoma hapa unaweza kusema wewe hujawa mtumwa, unatumia kwa kupanga mwenyewe, lakini nikuambie kitu kimoja, kwa sehemu kubwa sana umeshakuwa na utaziona dalili kwa kusoma kitabu hiki.

Nne utajifunza jinsi ya kuondoka kwenye utumwa wa kidijitali ambao umeshaingia.

 Baada ya kuona jinsi ambavyo umenasa kwenye utumwa huo, utajifunza njia za kujinasua.

Hapa utajifunza jinsi ya kuizidi ujanja simu janja yako.

Tano utajifunza falsafa mpya ya kuendesha maisha yako kwa uhuru katika zama hizi za usumbufu.

Pamoja na kujifunza kuhusu zama hizo na jinsi ya kuondokana na utumwa wake, usumbufu wake hautaisha, teknolojia mpya zinaendelea kugunduliwa kila siku na zikiwa na ushawishi mkubwa.

Hivyo unahitaji kuwa na falsafa unayoitumia kuchagua huduma za kidijitali utakazochagua kutumia kwa manufaa yako.

Sita utajifunza jinsi ya kutumia akili yako kuvunja uraibu wowote ambao umeshajijengea. Kama tulivyoona, huduma za kidijitali zinatumia jinsi ubongo unavyofanya kazi kukuingiza kwenye utumwa.

 Hivyo wewe unapaswa kuutumia ubongo wako vizuri kuondoka kwenye utumwa huo.

Saba utajifunza sababu kumi kwa nini unapaswa kuondoka kwenye mitandao yote ya kijamii sasa hivi. Hizi ni sababu ambazo zimechambua jinsi matumizi ya mitandao ya kijamii yalivyo na athari kwenye akili yako, utulivu wako, mahusiano yako, uchumi wako na hata imani yako. Kwa kuzijua sababu hizi kumi, utajionea mwenyewe jinsi ulivyorudi nyuma tangu umeanza kutumia mitandao hiyo na hivyo kuachana nayo ili kuepuka madhara yake.

Mwisho kabisa utajifunza njia za kutumia kufanya maamuzi iwapo utumie huduma ya kidijitali.

Utajifunza jinsi ya kutumia vigezo vitatu vya AFYA, UTAJIRI na HEKIMA katika kuchagua na kutumia teknolojia mpya, ambazo zitakuwa na manufaa kwako badala ya kukufanya mtumwa.

Tuko kwenye vita, adui mkuu anajua yuko vitani ila wanaolengwa hawajui.

Hivyo unapaswa kuwa na maandalizi mazuri ya kupambana na vita hii ili uweze kutoka salama na siyo kuwa mfungwa.

Pata na usome kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI ili upate mbinu za kupambana kwenye vita hii na kutoka ukiwa mshindi. Kitabu hiki kimechapwa kwa nakala ngumu (hardcopy).

Kitabu kinauzwa TSH elfu 20 (20,000/=) na ili kukipata wasiliana na 0752 977 170 na utaletewa au kutumiwa kitabu popote ulipo Tanzania na Afrika Mashariki.

 Kwa sababu ya maombi ya watu wengi Leo tunatoa OFA kwa watu hamsini(50) wa kwanza, ukinunua LEO kitabu cha EPUKA UTUMWA WA KIDIJITALI, utapata fursa ya kujiunga na chaneli ya SOMA VITABU TANZANIA.

Unachotakiwa kufanya ni kutuma ujumbe mfupi unaosomeka “NIUNGE” kwenda namba 0752977170, baada ya kununua kitabu chako.

Vigezo na masharti kuzingatiwa.

MUHIMU; Kama utanunua na kusoma kitabu hiki na ukaona hakina manufaa yoyote kwako, unaruhusiwa kukirudisha na ukarejeshewa fedha zako.

Hivyo chukua hatua sasa, huna cha kupoteza lakini una mengi ya kupata, yatakayokuweka huru kwenye zama tunazoishi sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published.

Related Post